Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,932
- 31,178
Heshima sana wanajamvi,
Nayatazama mabadiliko madogo baraza la mawaziri kama sehemu ya mkakati wa kumwinua January Makamba kuelekea kileleni (IKULU) baada ya Wizara ya Nishati kumshinda. Kuendelea kumbakiza wizara hiyo hiyo ilikuwa ni kumharibia kisiasa.
Najua watu wengi wamekimbilia kushangaa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko,lakini nyuma ya pazia WAZEE wa Msoga Camp safari hii hawataki kukosea kama ilivyokuwa kipindi kile cha 2015.Mzee Magufuli hakuwa chaguo lao mazingira au kivumbi cha Lowassa kiliwasababishia kufanya maamuzi bila hesabu sahihi.
January Makamba anaandaliwa maandalizi kabambe bila WAZEE wa Kanda pendwa kushtuka.Mchezo unaochezwa ni kuanzisha cheo kisichokuwepo kikatiba cha NAIBU WAZIRI MKUU kwa lengo la kuwazubaisha WAZEE wa Kanda pendwa kwamba kumbe wao ni sehemu ya walamba asali,hawana haja ya kulalamika wametengwa, hawapendwi, si sehemu ya watoto pendwa.
Vurugu za chama kileeeee kule kanda pendwa hakika kuwastua wapanga mikakati umuhimu wa kumwandaa mwanasiasa kutokea huko kwa lengo la kumtumia baadae kutimiza malengo yao hasa ahadi ya kuhakikishiwa nafasi ya Mzee wa Korosho.
January Makamba kapelekwa pale Foreign Affairs kupata uzoefu baada ya kushindwa vibaya sana Nishati.Katuachia mgao wa umeme,kashindwa kupanga na kupangika mfumo mzima wa manunuzi ya mafuta.Kaondoka Nishati hali ikiwa tete.
Mtangulizi wake Kalemani kasambaza umeme wa REA karibu vijiji vyote kaingia January REA hakuna kila kitu shabala bagala.NISHATI ilimshanda Makamba hana ujuzi zaidi ya kubebwa na mfumo wa walamba asali.