Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Mafanikio yako yanategemea sana mtazamo wako. Wazo hili nililipata katika uzoefu wa Richard Yu. Alikimbia China ya Kikomunisti, akaanza maisha upya Marekani (yeye na wazazi wake), na baadaye akajenga biashara kadhaa zenye mafanikio—ikiwemo online school (shule ya kidigitali).
Safari yake inatufundisha jambo moja kuu:
Hakuna anayekuja kukufanyia sehemu yako. Mafanikio yako yanategemea maamuzi yako, vitendo vyako, na uvumilivu wako.
Huenda unasoma maneno haya na unahisi kukwama. Zingatia mabadiliko 7 ya mtazamo yatakayosaidia kuondokana na imani potofu na kuanza kujenga maisha unayoyatafuta.
Lakini failure (kushindwa) ni mwalimu mzuri. Na ni sehemu ya mafanikio. Mhenga moja akasema "I win, I earn, I fail, I learn. Either way, I move forward".
Anza leo. Chukua hatua moja, halafu nyingine.
Usisubiri ruhusa. Usisubiri uhakika.
Badilisha fikra zako—na maisha yako nayo yataanza kubadilika.
Signed,
Amba Jnr.
Safari yake inatufundisha jambo moja kuu:
Hakuna anayekuja kukufanyia sehemu yako. Mafanikio yako yanategemea maamuzi yako, vitendo vyako, na uvumilivu wako.
Huenda unasoma maneno haya na unahisi kukwama. Zingatia mabadiliko 7 ya mtazamo yatakayosaidia kuondokana na imani potofu na kuanza kujenga maisha unayoyatafuta.
Badiliko #1: Tambua "Kwa Nini" Yako
Tafiti zinaonyesha kuwa watu huhamasiswa na mambo mawili:- Kukimbia maumivu (mwanadamu kawaida ana uwezekano mara mbili wa kukimbia maumivu kuliko kuitafuta raha).
- Kusaka furaha.
- Ukipata kalamu na karatasi (na dak 2 tu za ziada), hebu jaribu zoezi lifuatalo:
- Andika vitu 5 ambavyo ungevifanya endapo ungepata kipato kinachoendana na ndoto zako.
- Andika vitu 5 ambavyo kamwe hutaki familia yako wavipitie.
- Tafuta mtu mmoja ambaye utapambana kwa ajili yake(mwenzi, mtoto, mzazi, au hata wewe mwenyewe - kwa mujibu wa maisha unayoyatafuta ya baadaye).
Badiliko #2: Dhamiria kuwa Mtendaji
Njozi/ndoto zako hazitakufaa bila vitendo.- Unaweza kusoma vitabu vyote, ukapata ushauri wote (kama huu nnaotoa), ukatazama video za motiveshno wote unaowajia (Nanauka and the team), na kuhudhuria semina zote za nguvu—lakini kama hutaweka ulichojifunza kwenye matendo, hakuna kitakachobadilika.
- Wewe ndiye unayepaswa kuchukua hatua ya kwanza, kisha ya pili, kisha ya tatu. Na kuendelea hivyo.
Badiliko #3: Hakuna "Faza" Anayekuja Kukunusuru
- Hakuna mshauri, kozi, au bahati njema itakayorekebisha maisha yako kwa maajabu ya ghafla (na sikatai kuwa miujiza na maajabu yapo).
- Mafanikio yanatokana kwa kujikubali kikamilifu—kukubali kuwa kuna wakati maishani umefeli, na kukubali kuinuka tena, kujaribu tena, na kupigana tena ili kufikia mafanikio unayoyatafuta.
- Kulaumu wengine kunakufanya ukwame. Hata kama maisha ya hapo awali yalikuwa ya kawaida sana, au wazazi hawakukubeba kama ulivyotarajia, ni wakati wa kujitegemea. Lawama haitasaidia chochote.
Badiliko #4: Kubali Kushindwa
Jamii inatufundisha kuwa kushindwa ni kitu kibaya. Hasa mfumo wetu wa elimu imewafundisha vijana kuwa "Someni, mwisho wa kusoma, utapata kazi nzuri sana" (huo ni wimbo wa msanii fulani). Tena nikiwa shule waliwekaga passmark. 75. Ukipata 30, unalamba stiki 45. (Ntaleta kisa siku nyingine),Lakini failure (kushindwa) ni mwalimu mzuri. Na ni sehemu ya mafanikio. Mhenga moja akasema "I win, I earn, I fail, I learn. Either way, I move forward".
- Kuzidiwa na wasiwasi na mshikamano = ukuaji.
- Kila kosa ni somo. Trust the process. Jifunze kitu
- Badilisha mtazamo: Unapotaka kukata tamaa, jiulize swali: "Kosa hili linanifundisha nini?"
Badiliko #5: Huwezi Kufanikiwa Pekee Yako
Kujitenga kunaua maendeleo yako.- Ikiwa unajisikia umekwama, tafuta jamii ya watu wanaowaza kama wewe (mentorship group).
- Jizingire na watu wanaokukabili na kukusaidia.
- Jifunze kutoa kabla ya kupokea—mafanikio hufuata wale wanaowainua wengine. Usiwe mroho/mbinafsi wa kutaka kufanikiwa mwenyewe.
Badiliko #6: Kuna Nguvu katika Udhaifu Wako
- Kwa wengi hii ni ngumu kumeza. Jifunze kukiri kuwa hujui kila kitu.
- Jifunze kuomba msaada unapokwama—Atakaye kusaidiwa hujifunza kuondoa aibu.
- Kiburi kinazuia ukuaji; unyenyekevu ni silaha yako ya kupiga hatua unapohisi umepungukiwa katika maeneo fulani.
Badiliko #7: Kujilinganisha na Wengine Kunaua Maendeleo
- Usilinganishe ukurasa wa 1 wa maisha yako na ukurasa wa 20 wa mtu mwingine.
- Mtu pekee unayepaswa kujilinganisha naye ni wewe. Tathmini historia yako, na tambua mabadiliko yote (hata kama ni madogo) uliyopitia.
- Jifunze kuwapongeza wengine wanapofanikiwa. Badala ya kujaribu kuwashusha, watakie mema tu.
- Jifunze kutoka kwa wengine (hasa kanuni za maendeleo), lakini panga safari yako kivyako. Vidole havilingani...
Hitimisho
Baada ya kusoma haya yote, jambo moja linabaki wazi: una uwezo mkubwa zaidi kuliko unavyofikiri. Lakini uwezo huo hautaonekana hadi ubadilishe mtazamo wako, fikra zako, na udhamirie kuwa mtendaji.Anza leo. Chukua hatua moja, halafu nyingine.
Usisubiri ruhusa. Usisubiri uhakika.
Badilisha fikra zako—na maisha yako nayo yataanza kubadilika.
Signed,
Amba Jnr.