Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

Hujaenda na wakati swety Lady,
Chadema wakisusia kuangalia TBC ni credit kwa ITV, star tv etc. TBC itakosa biashara kwa sababu wateja watapungua.
Pili, King cobra wa Zambia aliomba TV ya Isiseme cho chote kuhusu mikutano yake wakati anagombea. Wao wakagoma na kuendelea kumchafua. Leo ni Rais wa Zambia. Vigogo wengine walijiuzulu bila kufukuzwa baada ya Rais mpya kuingia. Je, walijua hilo? TBC lazima wasome alama za nyakati.

Well said M/Kiti
 
Nimebarikiwa na kuridhika sana na maazimio haya.

By the way is JK ok? This country is running on auto-pilot mode far too long. The CC should really take a look on the matter in its coming convention.
 
Hivi kuna ving'amuzi vipi mpaka sasa ukitoa startimes coz wanapatia hela kwenye migongo yetu wananchi halafu tbc inatangaza ujinga. King'amuzi kipi ambacho kina local channels za ukweli ili nimuweke mtu wa vyuma chakavu standby(king'amuzi cha startimes nakipiga shoka)
 
TBC nilishasusa zamani binafsi lakini rasmi sasa napiga marufuku mwanafamilia yangu yeyote kukuta ameifungua TV au radio hiyo! Wanatumia kodi zetu kwa manufaa ya CCM!

Mi leo naonda kuvuruga codes za TBC kwenye receiver yangu, ili hata watoto wakitaka kuangalia nikiwa sipo washindwe...
 
MUNGU AKUBARIKI SANA M/KITI WANGU MBOWE! I feel proud to have a such powerfull and determined leader like you!
 
Hujaenda na wakati swety Lady,
Chadema wakisusia kuangalia TBC ni credit kwa ITV, star tv etc. TBC itakosa biashara kwa sababu wateja watapungua.
Pili, King cobra wa Zambia aliomba TV ya Isiseme cho chote kuhusu mikutano yake wakati anagombea. Wao wakagoma na kuendelea kumchafua. Leo ni Rais wa Zambia. Vigogo wengine walijiuzulu bila kufukuzwa baada ya Rais mpya kuingia. Je, walijua hilo? TBC lazima wasome alama za nyakati.


Duh hii nimeipenda, sasa TBC wakae mkao maana wakiendeleza umafia wao wajue hawana chao tena nchi ikikombolewa.
Inasikitisha sana watu wanapoacha kutumia akili zao badala yake wanakuwa kama Nyumbu, hivi wanadhani upotoshaji na upendeleo wa dhahiri wanaoufanya hauonekani?

Wengi tulishaisusia TBC kitambo ila ni vizuri sasa waonje matunda ya unafiki wao.
 
Mh.mwigulu mziki wako unataka kuwashwa tafadhali jiandae kuucheza,uliuomba mwenyewe sasa m4c wanakuletea, makamanda wote wAtakuwepo chopa,pikipiki,magari yote ya matangazo,mkuu lissu pia ndani eeee muumba kama ikiwezekana pitishia pembeni kiama hiki kwa chemba,.. Amen.
 
Tbc ni uchafu, la msingi CDM fanyeni namna wananchi tupate decorder ambazo hazina huu uchafu wa tbc


Kusema kweli, hiyo azimio namba 6 mimi nimeipenda sana. TBC lazima warudi kwenye weledi wake vinginevyo wataumia. Maana wanapiga propaganda kupita kiasi.
 
TBC inapotosha watu kuanzia kwenye sensa hadi matukio ya polisi.

VIVA CDM.

ila speech ya rais hawakosi kuionesha hata iweje na huirudia kila wakati, wakati habari zingine za muhimu pia hawaoneshi kabisa. au huonesha kwa magumashi, mfano migomo ya wanfunzi, mikutano ya kisiasa haswa ya vyama pinzani na habari chungu nzima huzizima. kwa kweli TBC itatudumaza tusipokuwa makini, mimi nikitaka habari hukomaa na vyombo vingine na baadae nikijisikia huitazama kuona je wameonesha au gumashi kama siku zote na ninakuta ni full gumashi
 
Kuna Jamaa mwingine wa shy town Anitwa Godwin makomba,inabidi chadema wamchunguze hayuko sawa na Ikibidi wamvue uanachama,hivi majuzi aliongoza msafara kwenda Dodoma kumpongeza masele kupata uwaziri ili hali yeye alikuwa mstari wa mbele kwenda mahakamani Tabora kupinga ubunge wake,pili kulikuwa na tetesi Kuwa alikuwa anavujisha nyaraka za kisheria za kesi husika,zinatafutiwa majibu na ccm kabla hata ya kufika mahahama kuu,tatu Kama katibu wa wilaya chadema anaweza kwenda Dodoma kufanya sherehe ili Hali yeye ni kiongozi,kwa kitendo hicho wanachama wajifunze nini kwa viongozi wao?
 
ushauri wangu kwa CDM maazimio waliyoyatoa wayasimamie wayapiganie hadi kieleweke wakiishia katikati halafu ikawa ziiiiiiii hata sisi wananchi tutakufa moyo kama ni kweli wako makini wafanye tuone wasimuogope mtu wala kitu.mapambano hadi mwisho.
 
Ni katibu aw wilaya ya shinyanga vijijini ambako kwasasa kumeanza kuibuka migogoro ya viongozi ,naweza kumuunganisha na migogoro Hiyo pia,kabla ya yeye kwenda huko hakukuwa na matatizo hata kidogo,kitendo hicho na kifananisha na usaliti wake aw kuvuruga chama mkoani shy,kwa bahatti nzuri wadau walimdaka akiwa pia na mwiguru nchemba pale Dodoma
 
Azimio la kwanza mpaka mwisho1-9 utagundua walikutana watu makini kwa maamuzi makini! cha msibngi ni Umma tu-support kwa hali na mali kwa nguvu zetu zote.
 
halafu wakomae mtu kama tendwa ni hatari sana kwa demokrasia endelevu. huwezi kumuweka kada wa chama kusimamia usajili wa vyama vyote huu ni ugomvi au wanataka CDM watoe matusi ili ssa wapate sababu muafaka ya kukifuta chama. msajili wa vyama anatakiwa kuwa neutral na akitaka kuadhibu chama fulani kwa kosa fulani basi afanye hivyo sio kosa hili huyu anaadhibiwa au anataka kuadhibiwa huyu anaachwa. nani asiyejua kuwa wakati wa sensa ccm walikuwa wanafanya chaguzi na mikutano ya kisiasa au hicho sio chama cha siasa,ila CDM kuenda kujifungulia tawi kosa la jinai, wamwage petrol wenyewe wawashe moto wenyewe halafu watake kufuta chama cha CDM eti kinachochea vurugu, ccm wajue muda ukifika umefika tu, sasa muda wa watu kukitema chama chao na kushabikia kingine umefika. waisome namba waache kuwatumia watu kama mahakama msajili wa vyama,polisi na majeshi mengine na vyombo vya habari kama TBC kutaka kulazimisha mambo.
 
Kuisusia TBC safi sana, kilio chetu wengi wetu JF kimesikika, kutumia helcopter na kupita kitongoji kwa kitongoji badala ya vijiji kwa mkoa wa Singida huo ni ujumbe tosha kwa Mwiguru Nchemba

Na ni matumizi mabaya ya raslimali na kumuongezea umaarufu Mwigulu kwa sababu it is easier kwake kujinadi kuwa yeye ndiye Kiboko ya CDM.
 
Kuna namna yeyote ya kuiondoa TBC kutoka kwenye DSTV? Sitaki ninapotafuta channels nyingine nione hata hilo neno TBC. Nifanyeje pia kuiondoa TBC kwenye Star Times? Mimi sitaki hata nilione hilo neno TBC, linanitia kinyaa na hasira kiasi kwamba nawachukia hata wafanyakazi wote wanaofanya kazi TBC. Najua wapo wasiopenda bali wanaganga njaa lakini jitahidi kutafuta kazi sehemu nyingine maana kufanya kazi na juha nawe utaunganishwa. Siku nchi hii itakapojikomboe, TBC ifutwe na shirika jipya lianzishwe, shirika litakalokuwa na uzalendo siyo hili linawatumikia baradhuli.

Mie naangaliaga TBC alhamisi kwa sababu ya Ze komedi kopi na kupest zaidi ya hapo hata wakiifunga kabisa poa tu.
 
Hiyo ni siasa au uhuni?

MKUU ZOMBA

jifunze kutofautisha kati ya siasa na uhuni. ebu tufafanulie wana jf apo uhuni upo kipengele kipi?
kumbuka hayo ni maazimio ya chama cha siasa cha chadema. ok?
kama unaona ni uhuni unaweza toa ushauri wako unaoona utakuwa na manufaa kwa wananchi wote.


KUMBUKA SISI SOTE NI NDUGU TATAIZO NI CCM.



:focus:
Hongera makamanda, hujuma kwetu mwiko. hii tbc nasi tulishaisusa kitambo huku kitaa.
 
Back
Top Bottom