Safi sana maamuzi ya kamato yametulia, yanaonyesha umakini na watu wanaojali. Wasioogopa wala kuuangalia uso wa mtu kwa upendeleo. Sisiem imefondoa kitengo cha propaganda kutoka kwa H. tambwe na kukiamishia kwa Tv ya taifa inayoendeshwa kwa kodi zetu. Hii inauma sana na kuanzia leo baada ya tamko ni marufuku nyumbani kwangu kwa namna yeyote ile kutizamwa TBC Tv ama Radio. PolisiCcM mmeua sana mkishirikiana na Green guard lakini sasa hii damu ya mwandishi Mwangosi haitaenda bure. Sasa imefungua ukurasa mpya wa vuguvugu la mabadiliko na hivyo baragumu imeeisha pulizwa hakuna kurudi nyuma. Tumegandamizwa vya kutosha, tumenyanyaswa vya kutosha, tumegeuzwa watumwa katika nchi yetu wenyewe, tunauawa kama mbwa barabarani na wale tuliowaamini, sasa tunasema basi.
FREEDOM IS COMING TOMORROW!!
.