Maaskofu wamuasa Rais Samia Suluhu kuhusu haki na ustawi

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,223
2,000
Mie sikuona kama walikuwa waoga maana walisema ukweli MTUPU hadi wengine kuanza kutishiwa kuhusu uraia wao na baadhi hadi hii leo passport zao wamenyang’anywa.
Magufuli siku zake za mwisho za uhai alijua anakufa na dalili zilionekana wazi kwa wote kuona ndo maana watu walianza kuulizia aliko hasa baada ya kutoonekana kanisani lakini si Serikali wala hawa wajinga wa CCM waliweza kutoa jibu sahihi. Baada ya kifo ulimwengu uneambiwa kuwa hospitalini karibu na kitanda chake cha kifo kulikuwa na Viongozi wa Dini wakiwemo Maaskofu na Mapadre kwa Wakristo na Masheikhe ikiwa ni pamoja na Mufti. Tunaambiwa Viongozi hawa wa Dini walisali na kuimba nae na kuwa Wakristo walimpaka Mafuta matakatifu na kupewa Komunio ya mwisho kwa hiyo hii ina maana kuwa walikuwa wa mwisho kumuona na kuzungumza nae akiwa hai. Viongozi wa Serikali na Chama na ndugu zake walikuwa wapi wakati huo wa mwisho? Pili, hawa Viongozi wa Dini wengi hivi walijuaje hali ya Rais na walifikafikaje Hospitali wakati Nchi nzimà ilikuwa hajui alipo? Mwisho nani aliwakusanya na kuwaandaa wakamuage Rais? Siku za mwongo ni fupi!
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,787
2,000
Ni lazima Viongozi wote wa dini zetu washikamane na kuwa na sauti moja katika kuhakikisha haki na usawa vinaheshimiwa nchini bila kujali itikadi zetu. Tukumbuke haki huinua Taifa na kuleta maelewano yenye tija kwa Taifa.
Kwa speed tuliyoanza nayo kwa vijembe sijui mmh Ni Mungu tu akaonekane zaidi!
 
  • Love
Reactions: BAK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,621
2,000
Akifanya mchezo nchi itawaka moto na wengi hawako tayari kuona dhuluma na udhalimu wa jiwe unaendelea nchini. Ageuze mwelekeo kwa kuongoza kwa haki, kuheshimu raia, upinzani, katiba, mahakama, bunge na pia kuhakikisha matakwa ya Watanzania ya kupata Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi yanatimizwa kabla ya 2025.
Kwa speed tuliyoanza nayo kwa vijembe sijui mmh Ni Mungu tu akaonekane zaidi!
 

ngome1838

JF-Expert Member
Feb 20, 2019
750
1,000
Dini zimekuwa chanzo cha uonevu na ubaguzi kwa Marne nyingi.Historian ya dunia na mabaya yake yote nyuma yake zipo dini.Rejea yaliyoyotokea Pre-enlightenment period na kuendelea.Dunia pasipo dini tungekuwa salama zaidi.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,621
2,000
Watu wanashangaza sana wanasahau kama hawa Viongozi wa dini ni Watanzania na wana haki kama Watanzania na pia Viongozi wa dini kutoa kauli zao kuhusu mwelekeo wa Nchi.
Hawampangii wanamkumbusha wajibu wake km alivyoapa kulinda katiba y nchi. Ukiwa Rais huongozi tu kwa utashi wako.
 

EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
6,434
2,000
Hivi huo uamsho morovian ndio kitu gani hiko?,nilijua morovian lakini huo uamsho umetoka wapi kama kuna uelewa naomba anieleweshe
 

BIGGAG

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
448
1,000
Naona madume yameanza kumtisha mama yetu.

Namuombea ujasiri, nimatumaini yangu kua hatayumbishwa kwani yeye mwenyewe leo kasema ni Raisi mwenye maumbile ya kike! Tutafakari.

Kama hiyo haki inayozungumziwa ndio hiyo ya kuwadhulumu mama ntilie na machinga na wengine Kama hao,au kuwatukuza wafanyabiaashara wezi Basi ishindwe.

Msije mkamyumbisha mama yetu yakatokea yale ya nchi ile ya asia alipewa nobel prize ya haki za binadamu baadae akapewa kuongoza nchi yake, wazee wakashindwa kumwelewa wakachukua nchi na Sasa ni vurugu tupu huko.

Historia inaonyesha viongozi wa dini kwenye siasa huwaponza kondoo wao ama kwa kufaham au kwa kuto kufaham.
Rejea utumwa ulivo simamiwa na dini za uislamu na kikristo kuiumiza africa, ukoloni na wamissionari, nk. Si ajabu hata Sasa wakati wa ukoloni wa kiteknologia viongozi wengi wa dini wakaipoteza jamii Kama ilivo historia

Si semi tuwapuuze Ila tuwe makini na ushauri wao.

Maoni binafsi.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,036
2,000
Maaskofu wasije kuwa wameeanza matamko yao kwa kuwa Rais wa sasa ni Muislamu, mbona wakati wa utawala wa Hayati Magufuli hawakuwa wakimshauri masuala ya kufuata haki na utii wa sheria na katiba.
We kichwani mind.u acha kujipumbaza Hawa maaskof wamepambania haki mwanzo mwisho Hadi mpuuza haki Mauri yakamfika Sasa Ni wakati wa kuijenga Tanzania ambayo Rais anaogopa cheo chake kuliko Rais anayependa kuogopwa
 

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
9,019
2,000
Mambo hayahaya ndio mliyafanya mkadhani mnamsaidia Magufuli kumbe ndio mnamtengenezea anguko lake ujinga sana mnafanya nyie mataga mnadhani mnamlipia kisasi JPM kumbe mnamchonganisha na wananchi wake nao wakalia kwamba serikali yao inawaonea vilio vikasikika mbinguni Sasa anzeni Tena kutengeneza anguko la mama kwa kumchonganisha na watu wake na hao viongozi wa dini watu wakilia Tena kwa Mungu wao msijesema sio wazalendo.
Akili ndogo
 

DUMU

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
338
500
Hawa ni kati ya viongozi wa chache wa dini waliokuwa mstari wa mbele muda wote kuelezea hisia na matamanio ya Watanzania . Hawa hawapo kwenye lilekundi la mapambio
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom