Maaskofu wamuasa Rais Samia Suluhu kuhusu haki na ustawi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,702
2,000

Maaskofu wamuasa Rais Samia kuhusu haki na ustawi​


MAASKOFU wa makanisa mbalimbali Tanzania wamempa ushauri Rais Samia Suluhu Hassan juu ya namna nzuri ya kuongoza nchi kwa haki na ustawi.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Dar es Salaam wa Kanisa Katiloki, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, Jumamosi iliyopita alisema kazi ya urais si ndogo, ni jukumu zito ambalo linambebesha wajibu wa kuwahudumia kwa usawa raia wote.

“Najua kuwa Mama Samia alishirikiana kwa karibu na Magufuli wakati akiwa makamu wake wa rais, hivyo hatuna wasiwasi kuwa anaielewa nchi, anaifahamu na anajua vipaumbele vyake hivyo ataviendeleza kwa juhudi, yale yote mema ambayo yalikuwa yakishughulikiwa na Magufuli.”

“Lakini kwa sababu nimesema jukumu la kuongoza nchi ni jukumu zito, nawaalikeni wote tumuweke katika sala, tumpe ushirikiano na kushikamana naye katika kutafuta ustawi na maendeleo ya kila raia wa nchi hii,” alisema Ruwa’ichi.

Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania kufuatia kifo cha John Magufuli, aliyekuwa mtangulizi wake. Alifariki Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama, Dar es Salaam.

IMG-20210322-WA0288.jpg

(Askofu Bagonza)
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, amemshauri Samia kuiogopa na kutetemekea nafasi hiyo “kama sisi raia tunavyomuogopa na kumtetemekea mtu aitwaye rais.”

“Rais asiyeuogopa urais ni hatari kwa nchi na kwake mwenyewe binafsi. Rais asiyeuogopa urais lakini anataka aogopwe, ni hatari na msiba usiokwisha kwa Taifa lolote,” alisema askofu huyo.

Askofu Bagonza alimshauri Rais Samia “kuwapumzisha kazi” wote wenye hulka na rekodi ya kukanyaga sheria na katiba kwa kisingizio cha uzalendo.

“Hawa watu ni hatari kwa rais kuliko walivyo hatari kwa nchi. Rais wetu aimbe wimbo wa haki tu ili kuondoa kila chembe ya ubaguzi,” aliongeza Askofu Bagonza.

Aliwashauri wasaidizi wa Rais Samia kumsaidia kufanya kazi zake salama na kwa mamlaka ambayo hayaonei mtu yeyote.

Askofu Emmaus Mwamakula, Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki ,amemshauri Rais Samia kusikiliza maoni ya makundi mbalimbali nchini yanayodai Katiba mpya na kujenga mazingira ya kuanza upya kwa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ili Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike kwa haki na salama.

Mwamakula ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani, amemshauri Rais Samia kuacha vyombo vya habari kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na vyombo vya dola.

Askofu huyo anasema ni vyema uongozi wa Rais Samia uangalie namna ya kurekebisha mazingira ya wafanyabiashara ili wasinyanyaswe wala kutishwa na maofisa wa serikali.

“Tunashauri utawala mpya ufungue majadiliano na maridhiano na viongozi wa vyama vya upinzani kuhusu malalamiko yao na kuwapa nafasi ya kufanya kazi zao za siasa kwa uhuru,” aliongeza askofu huyo.

IMG-20210322-WA0287.jpg
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,702
2,000
Ni lazima Viongozi wote wa dini zetu washikamane na kuwa na sauti moja katika kuhakikisha haki na usawa vinaheshimiwa nchini bila kujali itikadi zetu. Tukumbuke haki huinua Taifa na kuleta maelewano yenye tija kwa Taifa.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,349
2,000
Maaskofu wasije kuwa wameeanza matamko yao kwa kuwa Rais wa sasa ni Muislamu, mbona wakati wa utawala wa Hayati Magufuli hawakuwa wakimshauri masuala ya kufuata haki na utii wa sheria na katiba.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,702
2,000
Huoni aibu kusema uongo!? 😳😳😳
Maaskofu wasije kuwa wameeanza matamko yao kwa kuwa Rais wa sasa ni Muislamu, mbona wakati wa utawala wa Hayati Magufuli hawakuwa wakimshauri masuala ya kufuata haki na utii wa sheria na katiba.
Maaskofu wasije kuwa wameeanza matamko yao kwa kuwa Rais wa sasa ni Muislamu, mbona wakati wa utawala wa Hayati Magufuli hawakuwa wakimshauri masuala ya kufuata haki na utii wa sheria na katiba.
 

John Prand

Member
Sep 24, 2017
45
125
Hao wanaojiita maaskofu ndio walipotufikisha hapa. Dini za wakoloni na bado wanatuambia tudharau asili yetu.

badala waseme tuachane na hizo dini za wageni. Halafu wanavyojiita maaskofu waache na waje tujenge nchi.

hamna kitu kutoka kwa hawa wakoloni weusi wenye kofia ya dini za kikoloni.
 
Oct 27, 2020
97
400
Honestly kama kweli serikali ina nia ya kurudisha umoja wa watanzania na kuhakikisha mauza uza na misukosuko ya hii miaka michache iliyopita hayajirudii tena, basi waanzishe mchakato wa katiba mpya, itakayo zingatia uhuru, haki na uwajibikaji.

Lasivyo kama katiba hii hii itaendelea kutumika basi ipo nafasi ya kupitia misukosuko ile ile kwa kiongozi mwingine tena ajae.

Tusiendelee kuwa mateka wa hii katiba. Ambapo wananchi wamegeuzwa kuwa watazamaji tu na hawana mamlaka, hata nchi ikiwa inaendeshwa ndivyo sivyo.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,674
2,000
Maaskofu wapumbavu tu hao..kwanza tutaanza kuwadukua tuwajue na madem zao tuwaanike
Wanamfikia Gwajima kwa huo upumbavu? Mtu anayefikia mpaka hatua ya kujirekodi akifanya ngono!

Huku akitambua kabisa ni mume wa mtu, ni askofu ndani ya kanisa lake, na bado amepewa zawadi ya ubunge na msukuma mwenzake! 🤔
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,702
2,000
Acha uongo wako!!! Mbona walikuwa wanasema!!! Ulikuwa umetia pamba masikioni? 😳😳😳😳


Maaskofu Katoliki watoa waraka mzito
Dar es Salaam. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa waraka wa Kwaresima 2020 ambao mbali na masuala ya uinjilishaji, umezungumzia utawala wa kisiasa, wakisema unatakiwa ufanyike ndani ya mipaka ya sheria ya kimaadili.

Waraka huo wenye kichwa cha habari “Ujumbe wa Kwaresima 2020: Ufalme Wako Ufike”, umetolewa na maaskofu wote 33 wa majimbo ya kanisa hilo nchini Tanzania, wakiongozwa na Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga, rais wa TEC.

Tofauti na miaka mingine, waraka mpya umetumia mada za Kibiblia, za kijumla, ukigusia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya nchi bila ya kunyoosha kidole.

Alipoulizwa kuhusu waraka huo ambao umechapishwa kwa ukamilifu na tovuti ya Redio Vatican, katibu mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima alisema ni kweli umetolewa na baraza hilo na umeshasambazwa katika parokia za kanisa hilo nchini.

Mbona mliufyata kwa kipindi chote? Mlikuwa wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom