Maaskofu na Mashekhe: Tunataka tume huru ya Kijaji kuchunguza matukio yanayoendelea Tanzania kati ya Serikali na Chama cha Upinzani

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Wakiongea kupitia BBC maasikofu na wachungaji wamesema wanasikitishwa na hali inayoendelea Tanzania juu ya matukio ya watu kushambuliwa na hata kuvunjwa mikono. wanasema wanataka iundwe tume huru ya kijaji kwa kuwatumia majaji wastaafu.

Wanasema majaji wastaafu wanaweza kutokuwa na upendeleo wakitoa report yao pia wameonya iwapo haitafanyika na kutoa haki sawa kwa wote taifa litagawanyika

Wameongeza kuwa pamoja na kwamba sio watu wa siasa ila wanao wajibu wa kukemea maovu maana wanao umizwa ni moja ya waumini wao ivyo ni wajibu wao kuikumbusha serikali kama kuna mambo hayaendi vizuri wayarekebishe haraka wasisubiri mpaka amani itoweke.

Chanzo: BBC.

======

Kamati ya Kitaifa ya pamoja ya Maaskofu na Mashekhe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Tanzania wataka kuundwa tume huru ya kijaji, kuchunguza mvutano unaoendelea kati ya Serikali na Chama cha upinzani, kufuatia Sakata la wabunge wa CHADEMA kupigwa na kuumizwa huko Gereza la Segerea.

Wamesema jopo hili la majaji ndio linakwenda kumaliza minong'ono na chuki inayoendelea katika jamii.

 
Chadema mnataka kutupeleka kwenye udini na hao maaskofu wenu. Mkiambiwa na chama cha kidini mnakataaga lakini kila uchaguzi mnatumia udini na ukasikazini.

Hii coincidence vipi maaskofu wenye asili ya ukasikazini wanakuwa na stand moja na chadema? Hii ni conspiracy na ni udini plus ukabila
 
Chadema mnataka kutupeleka kwenye udini na hao maaskofu wenu. Mkiambiwa na chama cha kidini mnakataaga lakini kila uchaguzi mnatumia udini na ukasikazini. Hii coincidence vipi maaskofu wenye asili ya ukasikazini wanakuwa na stand moja na chadema? Hii ni conspiracy na ni udini plus ukabila
Wana ule mtindo wao wa kusema anaandika askofu fulan fulani, lakini cha ajabu sijawahi ona hayo wameandika wapi zaidi ya kuyaona kutoka kwa wafuasi wa chadema...
 
Chadema mnataka kutupeleka kwenye udini na hao maaskofu wenu. Mkiambiwa na chama cha kidini mnakataaga lakini kila uchaguzi mnatumia udini na ukasikazini. Hii coincidence vipi maaskofu wenye asili ya ukasikazini wanakuwa na stand moja na chadema? Hii ni conspiracy na ni udini plus ukabila
Hebu tuondolee utopolo wako hapa, Chadema inahusikaje hapa? Hivi huko CCM huwa mnakunywa maji ya chooni mbona kila anayesimama anatoa pumba tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema mnataka kutupeleka kwenye udini na hao maaskofu wenu. Mkiambiwa na chama cha kidini mnakataaga lakini kila uchaguzi mnatumia udini na ukasikazini. Hii coincidence vipi maaskofu wenye asili ya ukasikazini wanakuwa na stand moja na chadema? Hii ni conspiracy na ni udini plus ukabila
Mungu awabariki sana hao mababa Askofu.

formula ya October 2020 inazidi kunogeshwa zaidi na sasa itasomeka kama ifuatavyo:

CCM + polisi VS upinzani + umma + beberus + maaskofu.

upande wa CCM ukiondoa "polisi", nina uhakika "beberus" & "maaskofu" wataondoka automatically upande wa pili.

tukutane October.
 
Hawa ni kweli wanatimiza wajibu wao, ila wanapaswa kuwa kama viongozi wa dini wa Kongo. Wamepelekea kuishinikiza serikali kufuata mahitaji ya wananchi wa Kongo, hadi Kabira hakurudi tena madarakani. Hawa wa kwetu ni kama mbwa ambaye hana meno ana bweka tu haumi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona kila mnapofanya mikutano yenu au zizinduzi wa vimiladi vyenu,mnawatanguliza hao hao viongozi wa dini eti wawaombee dua,lakini wakiwakosoa mnasema eti wasichanganye dini na siasa,uzuri kwa sasa hivi kila mtu anaweza kutunza kumbukumbu.
 
Chadema mnataka kutupeleka kwenye udini na hao maaskofu wenu. Mkiambiwa na chama cha kidini mnakataaga lakini kila uchaguzi mnatumia udini na ukasikazini. Hii coincidence vipi maaskofu wenye asili ya ukasikazini wanakuwa na stand moja na chadema? Hii ni conspiracy na ni udini plus ukabila
Nadhani kuna watu wamekumbwa na uwendawazimu wa itikadi za kivyama.

Tatizo la watu kupigwa lisitazamwe kwa fikra duni za uhayawani wa ushabiki wa kivyama, bali litazamwe kwa hekima iliyo ya kweli.

Umtazame Halima Mdee na Bulaya na wengine, kama Watanzania. Kisha tujiulize:

1) Hawa walioumizwa walitenda kosa gani?

2) Kama kuna kosa walilolitenda, kosa hilo linastahili adhabu?

3) Kama walitenda kosa linalostahili adhabu, ni nani mwenye haki za kisheria kutoa adhabu? Ni Polisi, ni mahakama au ni magereza?

4) Kama walitenda kosa, ni hatua gani zilistahili kuchukuliwa? Ni kuvunjwa mikono na askari magereza, kufikishwa mahakamani au kuuawa na hao Askari magereza?

Maana haiingii akili, kwa mtu mwenye akili timamu, kuamini kuwa hao akina Dada wawili wasio hata na toothpick mkononi, walikuwa na nguvu za kuhatarisha usalama wa gereza zima na kundi la askari wote magereza waliopo Segerea, kiasi kwamba kulikuwa hakuna njia yoyote ya kistaarabu ya kuwadhibiti zaidi ya kuvunjwa mikono, kuwakanyaga matumboni na vifuani.

Taifa letu linapelekwa kwenye primitivity ambayo hata babu zetu hawakuwahi kuwa nayo. Hawa askari magereza walichokifanya, ustaarabu wao unazidiwa hata na fisi. Maana pamoja na kwamba fisi hana akili na ana tamaa ya kuoindukia lakini huwezi kuona fisi akimvunja au kumwua fisi mwenzie. Hawa askari hayawani hawana hata chembe ya ufahamu kuwa wale ni binadamu wenzao.

Tusishabikie matukio ya kijinga. Mambo yale yaliyofanywa na askari magereza yanaweza kuganyika kwenye jamii iliyokosa ustaarabu hata ule tu wa kufikia kiwango cha wanyama pori. Tusikubali usalama wa raia kuwekwa mikononi mwa majambazi.

Hawa askari magereza waliofanya upumb.avu ule wameliaibisha Taifa. Ule ni upumbavu ambao haustahili kufanywa kwa mtu yeyote, hata kwa mfungwa. Kama wametenda upumb.avu ule kwa raia wa kawaida, wafungwa huko magerezani wanafanywa nini?
 
mmh, Matendo yenu ya kinyama na kwa kauli zenu bayana haziwezi kuogopesha viongozi wa dini kuvikemea kwa kuwa wanatoka kaskazini. Siku zote ubaya na dhulma za haki wanaoanzisha ni ninyi sio upinzani.

Ni kauli nyingi za kijinga mmenena! Ni matendo mengi ya kinyama mmeyatenda! Na ni nia ovu nyingi zaidi mmezipanga!

Ni dhahiri Mungu ameanza kuwajibu na kuwadhihirisha kwa ubaya wenu sasa mmmeanza kujimaliza wenyewe kabla hao mnaowaita wapinzani hawajaanza kuwalipa kwa maovu mnayo watendea



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom