Maarifa ya Bure

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
348,109
Reaction score
1,249,102
Kama Ukichukua Tunda Bovu na Ukaweka Kwenye Tunda Nzuri Kipi Kinatokea ?? Fangasi Kwenye Tunda Bovu Itasambaa Mpaka Kwenye Matunda Mazuri na Kuharibu Yote. Hii Inatokea Pale Unapozungukwa Na Watu Wajinga.. Utakua Kama Wao.
 
“Mabawa madogo hayakuzuii kupaa” Waweza kuwa katikahali ngumu kwa sasa ama mambo yako hayaendi lakini ukiwa mtazamo chanya juu ya yanayojiri kwenye maisha yako lazima utapaa tu na kusonga mbele. Jioni njema
 
Kama Ukichukua Tunda Bovu na Ukaweka Kwenye Tunda Nzuri Kipi Kinatokea ?? Fangasi Kwenye Tunda Bovu Itasambaa Mpaka Kwenye Matunda Mazuri na Kuharibu Yote. Hii Inatokea Pale Unapozungukwa Na Watu Wajinga.. Utakua Kama Wao.View attachment 1352381
Usijadilisne na mjinga.

Atakushusha mpaka katika levo yake(ya ujinga)

Alfu atakushinda kwa uzoefu kwa sababu yupo katika nyadhifa yake anaielewa vyema.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anafahamika kwa jina la TIM. Tembo mwenye umaarufu mkubwa na kipenzi cha wengi amefariki akiwa na umri wa miaka 50. Tembo huyu alikuwa anapatikana katika mbuga ya wanyama ya Amboseli nchini Kenya. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na hifadhi ya wanyama pori nchini Kenya. Kwa sasa mabaki ya mwili wake yanapelekwa katika kituo cha makumbusho ya taifa Nairobi Kenya ili kuandaliwa kwaajili ya maonyesho na mafunzo.
 
“Mabawa madogo hayakuzuii kupaa” Waweza kuwa katikahali ngumu kwa sasa ama mambo yako hayaendi lakini ukiwa mtazamo chanya juu ya yanayojiri kwenye maisha yako lazima utapaa tu na kusonga mbele. Jioni njemaView attachment 1352386
Hakuna shida yenye kudumu.

Na hakuna raha yenye kudumu.

Maisha kama maisha ni raha na shida.

Ila maisha mazuri ni raha tupu na maisha magumu ni ugumu tupu.

Lakini kama unaishi basi jua raha ni zako na shida ni zako.

Hakika kila penye uzito basi mbele kuna wepesi,kama ambavyo kila penye kilima kikubwa basi mbele huko kuna mteremko mzuiri sana.

Ishi kwa kuchagua,usichague tu kuishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kupanga ni sehemu ya kuchagua!
 
BINADAMU ALIYE ZALIWA NA MIGUU MITATU FRANCESCO LENTIN Huyu Francesco Lentin alikuwa ni Raia wa Marekani alizaliwa tarehe 18/5/1889 huko Rosolini, Italy. Francesco Lentin alizaliwa akiwa na miguu Mitatu (3) yote ilikuwa inafanya kazi, alizaliwa akiwa na sehemu za siri za kiume mbili na zote zilikuwa zikifanya kazi na alikuwa na jumla ya vidole Vya miguu kumi na Sita (16). Francesco Lentin alikufa kwa ugonjwa wa mapafu, Florida Marekani tarehe 21/9/1966 akiwa na miaka 77.
 
Kama Ukichukua Tunda Bovu na Ukaweka Kwenye Tunda Nzuri Kipi Kinatokea ?? Fangasi Kwenye Tunda Bovu Itasambaa Mpaka Kwenye Matunda Mazuri na Kuharibu Yote. Hii Inatokea Pale Unapozungukwa Na Watu Wajinga.. Utakua Kama Wao.View attachment 1352381
Negative Energy ni diseas kama ilivyo magonjwa.

Ukikaa na marafiki 5 walalamikaji, broke jobless. Ukiwa hujui kulinda energy zako, after miezi kadhaaa utakuwa mmoja wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…