MAARIFA MBADALA: Tambua kitu sahihi kwa njia sahihi cha kufanya maishani

KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,822
2,290
View attachment 2295231

Habari ya Usiku wana JF,

Natumaini mko poa na wmaendelea vyema kabisa katika majukumu yenu na ratiba zenu za kila siku.

Kuna nyuzi nyingi sana zipo humu majukwaani zinazoelezea njia mbalimbali yakupamana na tatizo la ajira yakitolewa mawazo na miongozo mbalimbali ambayo huenda si kwa kila mtu inafanya kazi lakini huenda pia kuna wachache wao miongoni mwetu wamenufaika na hilo.

Ndio maana nami nikawiwa kidogo niweze kutoa yangu mawili matatu yanayoweza kuwasaidia watu kwa namna moja ama nyingi hata kama sio wote mmoja wawili miongoni mwetu wakinufaika basi jambo jema na la heri zaidi.

Jambo la kwanza kabla sijafika mbele nizungumze juu ya hili kuwa wengi sana biashara zao huwa zina tabia ya kufa mara kwa mara huwa hazisimami kabisa na sio hilo tu wengine wameweka mitaji mikubwa sana sana lakini mwisho wasiku wakaishia kuangukia pua, wala hawatamani tena kuweza kufanya jambo lolote tena katika mambo ya biashara nikama wamekata tamaa.

Sasa nitakalolizungumza leo linakuwa ni suruhisho kabisa kabisa tena kwa asilimia mia plus, mnaweza mkashangaa kidogo kwamba hakuna biashara isiyokuwa na hasara duniani kwanini wewe useme ni uhakika kabisa pasipo biashara kuanguka?

Jiulize jambo moja kwani ni kila mtu huanguka katika biashara? je kwani biashara ukifungua ni lazima hasara iwepo ili iwe biashara? jibu sio kweli hata kidogo, Japo wengine wamejitahidi kusali sana na kutolea sadaka juu ya biashara zao lakini haijawezekana kabisa, wengine wamejitahidi hata kuloga lakini haijawezekana kila baada ya muda inashuka kabisa biashara na inakosa kabisa nguvu yakusimama tena.

Sasa kuhusu shuguli au kazi za kufanya au ajira tunazokuwa nazo hapa duniani zimekaa sana katika ulimwengu wakiroho kuliko wa kimwili jinsi tunavyoona na kutarajia.

Kila mtu hupambana kwa namna ile inayokuwa inampendeza yeye binafsi na kuona kama hiyo ndio njia sahihi lakini katika hizo hizo sahihi haijarishi tumezipata kwa elimu au kwa kutokuwa na elimu bado huwa zinatuangusha.

Sasa kiroho iko hivi kila mwanadamu aliyepo hapa duniani amekwisha andaliwa kazi au majukumu yake yakufanya ambayo ndio sahihi kabisa kwa maisha yake hata akisema aanze nalo utotoni hadi anaingia kaburini haliwezi kufa hata siku moja, tuna watu wengi sana mbalimbali wako mitaani tunaishi nao huwa wanauwezo wakuona kabisa lakini ndio huwa hawawezi kukuambia sababu ya miiko ambayo wengi hatuijui, unaweza ukawa unakomaa zako na bodaboda ila kuna mtu anakuona unapaswa ufanye biashara ya chakula kwako ndio inakutoa kimaisha.

Huenda una phd zako uko zako katika ofisi kubwa unakaa nyumba nzuri na kausafiri kako unako ila kuna mtu anajua unapaswa uwe dereva ndio unaweza kutimiza haja zako zote unazokuwa unazihitaji katika maisha.

Sasa katika hayo yote je unadhani unaweza enda kokote kuzunguka upatiwe majibu hayo? jibu ni hapana sbaabu sio rahisi kupata mtu sahihi wakukusaidia kuweza kukuambia unapaswa kufanya nini, ila leo nitakupa njia sahihi yakujua ninini unapaswa kufanya katika suala la ajira ili uweze kupata suluhisho.

Unalopaswa kufanya jambo la kwanza kabisa angalia uapnde wa mababu zako, wao walikuwa wanafanya kazi gani, haijarishi ilikuwa kubwa au ndogo wewe ulizia tu hata kama alikuwa anafanya haimpi pesa kubwa ulizia tu hiyohiyo.

Mfano unaweza ambiwa babu yako alikuwa ni fundi viatu tu hapa mtaani alikuwa akipata mia mia zake hapa kwa uhalisia nipesa ambayo na biashara ambayo ni ndogo sana huenda hata mtaji wake haufiki elfu ishirini, lakini amini ninalokuambia ndugu chukua mahali fremu ukipenda hata mjini andika fundi viatu weka ofisi yako classic kabisa.

Nipo Hapa jamii forum ipo siku utakuja kunishukuru mimi sikujui ila utatamani hata unione unipe shukrani zako, pesa utakayoweza kupiga sio ya kawaida hata kidogo.

Hapo ni kwayule anayetafuta biashara au ajira yakuanza nayo ila kuna yule anayetaka kuwekeza biashara kubwa zaidi, nakuambia we fungua mahali kiwanda chako kwa mtaji wako anza kuunda viatu vya kawaida kabisa na product mbali mbali za miguuni, hiyo biashara yako itakavyotembea utaishia tu kusema kuna jamaa amekaa pale jf aliongea kiutani utani tu.

Hivyo ulizia biashara walizokuwa wanafanya babu zako huko nyuma chunguza chunguza uwezavyo utazikuta ziko nyingi sana tena sana tu chagua moja ianze kuifanya.

Pia sio lazima uwe na ujuzi wowote kuhusu hili, yaani siku unaanza kujifunza utashangaa kama ulikuwa unajua kabisa suala husika na unaliweza vyema japo pia unaweza weka watu wakafanya chini yako ili mradi liwe la kwako tu.

Watu mtajiuliza kwanini uangalie walichokuwa wanafanya babu zako?
Iko hivi utamaduni wakukumbuka na kuishi kwa kuwaenzi walliotutangulia wafrica wengi tulikwisha uacha zamani sana, niwachache mno wanofanya kwasasa, kinachotokea unapokuwa unafanya jambo walilokuwa wakilifanya mababu zako wao wanakuja timu nzima kuweka makao katika shuguli yako. Hautahitaji kuloga wala hakuna mchawi wakuchawia biashara yako, kwakupitia hilo wanafurahi na kujua kuwa unawakumbuka hivyo baraka zao zote wanazisimamia kwako na wanajitukuza kupitia wewe.

Na mara nyingi biashara zao au shuguli zao ni mambo ambayo unakuwa ukiyazarau wala hauyatilii mkazo wala kuona kama lina manufaa, fikiria leo unaambiwa babu yako alikuwa seremala na haujawahi kushika mbao hata siku moja wala kugonga msumari? na unaona kabisa mafundi seremala mtaani walivyojazana unajiwazia kabisa hauwezi kutoboa kupitia hapo.

Si hivyo tu lakini pia unaweza kuona ni biashara ambayo inafanywa na watu wahali ya chini sana sio mtu kama wewe nk lakini amini nakuambia hiyo ndio inaweza kuwa suluhisho lako la maisha.

Naishia hapa kukiwa na kazi yoyote babu yako alikuwa akifanya katika ukoo wako unashindwa kuitafasiri uifanye namna gani iweke katika maoni, nitakusaidia kuichanganua unapaswa kufanya nini.

Niishie Hapa Kwa Leo wenye Maswali Kalibuni Na maoni Pia
 
Hello habari.
1.Babu Zako wa upande upi wa baba au Mama?
Unaweza tazama pande zote mbili ukachagua kimoja unachokipenda, lakini kwa usahihi zaidi kujua wapi una bond kubwa angalia ni upande upi ambao unaona unapewa heshima kubwa na wale ndugu waliobakia,
huko unakopewa heshima kubwa ndiko unafuata zaidi.
Unaweza pendwa na kila mtu ila angalia upande wanaokuheshimu zaidi,
Hiyo hutokana na bond kuwa kubwa sababu yawewe kuwa na uhusiano zaidi na wazee kwa kujua ama kwa kutokojua
 
Back
Top Bottom