Maarifa Hatari: Embu tujifunze na kumjadili huyu Shetani vizuri

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,136
7,904
Kwanza naomba mods msihamishe uzi huu kwa kuupeleka kwenye jukwaa la dini maana nataka tumjadili huyu Shetani katika misingi ya maisha yetu ya kila siku na si katika misingi ya dini.

Naileta mada hii kwa tahadhari kubwa sana. Sina nia ya kumpromote huyu jamaa ila nadhani imefika wakati tumuangalie katika uhalisia. Siwezi kuimagine dunia bila kuwa na miongozo ya maisha yenye kusisitiza upendo, amani, mshikamano na umoja kati ya wanadamu. Miongozo yote hii tumeambiwa ndiyo njia ambayo Mwenyezi Mungu anataka tupite. Shetani kwa upande mwingine tumefundishwa, mambo yake na njia zake ni potofu, ovu na zitakazopelekea uangamie katika moto wa milele. Maandiko yameenda mbali zaidi na kutuambia tajiri atapata wakati mgumu sana kuuona ufalme wa Mungu. Hili jambo ukilifirkia vizuri, linafikirisha sana.

Kutokuwa na maarifa kumeelezewa katika maandiko kuwa ni kitu hatari na kibaya, lakini pia kuwa na maarifa na kwenyewe kumehusishwa na shetani kwa sababu kunaweza kumfanya mtu kuwa na majivuno na kwamba majivuno yanakuja kabla ya maangamizi. Kwa hiyo kiufupi maandiko yame discourage sana kuwa na maarifa kutokana na sababu nyingi ambazo ukiziangalia kweli zina mashiko.

Mimi nimeanza kufikiri kuna jinsi ambayo maandiko yamepotoshwa sehemu. Upotofu unaweza kuwa kwa njia ya kuficha taarifa muhimu kuhusu mtu au kitu fulani, taarifa ambazo kama ukiwa nazo zinaweza kubadili ufahamu wako kuhusu jambo hilo. Nayasema maneno haya kwa tahadhari kubwa naomba nieleweke vizuri. Nahisi kuna watu wamehodhi maarifa haya na wanayatumia kwa ajili ya ku control watu na dunia.

Tunaishi maisha ambayo hatujijui sisi ni nani, asili yetu, nguvu zetu na hata madhaifu yetu. Wakati huo huo ufahamu wa shetani ni mdogo saaana. Ukikaa ukafikiria jinsi gani hatumjui shetani utashangaa sana. Sun Tzu aliwahi kusema ili kumshinda adui yako inabidi kwanza ujijue wewe vizuri na umjue adui yako vizuri, hapo unajiweka katika nafasi ya kushinda vita. Kama Shetani ni adui yetu namba moja kama tunavyofundishwa, nadhani tuanze kwanza kufundishana ili mimi na wewe kila mmoja wetu ajijue YEYE NI NANI na pia kuwe na mafundisho ya kutosha na deep sana kuhusu Shetani.

Uzi huu ni wa maarifa hatari. Naomba tujadili mada hii kwa staha ili wote tutoke na kitu cha kutujenga katika maisha yetu hapa duniani.
 
Shetani yupo na kwa kweli kwa asili yake ni kiumbe mwenye nguvu nyingi mno kulinganisha na viumbe wengine wema na wabaya. Hata kati ya malaika shetani ni malaika wa daraja ya juu sana! Yapo madaraja 9 ya malaika (angelic hierarchies) or angelic choirs kama ifuatavyo:

Seraphims
Cherubim
Thrones
Dominions
Virtues
Powers
Principalities
Archangels
Angels

Shetani yupo katika kundi la pili la malaika yaani Cherubims (Makerubi)!!!

Kundi la pili kutoka mwisho ni malaika wakuu (archangels) mfano wao ni Michael, Gabriel na Rafael. Hawa tu wanatisha na wana nguvu za ajabu mno na hutawala juu ya makundi na makundi ya malaika!!

LAKINI USIOGOPE! Thanks to God! Shetani amefungwa sana hapo alipo yeye pamoja na malaika wenzake walioasi ambapo wengine nao ni mi-viumbe ya hatari iliyopo kwenye rank za juu sana na yenye uwezo wa kutisha!

Kwa kifupi jua kwamba Shetani na malaika zake hawajaachwa wafanye watakavyo ulimwenguni, God is in control. Pia jua kwamba pamoja na nguvu za ajabu walizopewa viumbe hawa, bado Mungu ni mkuu mno na hawezi kamwe kufananishwa hata kidogo na Maserafi (Seraphims)!!!

Sitazungumzia: Utukufu wa Mwanadamu na nafasi yake kati ya malaika. Ila Mungu asifiwe sana kwa jinsi alivyotuumba!!!

Mwisho: Jua pia kuna viumbe wengine walio pale Patakatifu pa Patakatifu juu ya majeshi ya malaika kama wale Wazee Wanne n..k. na kuna hatua zisizopimika kabla ya kumfikia boss mwenyewe; M.U.N.G.U.!!!
 
Mwanzo mzuri. Naweza tofautiana na wewe unaposema "shetani na malaika zake hawajaachwa wafanye watakavyo ulimwenguni". Mimi kuna mambo nimeshuhudia yaliyoniambia kuwa yuko active na ana nguvu na ushawishi mkubwa sana duniani. Hapa naongelea uwezo wa kuvuruga ufahamu wa mtu, kupotosha kile anachoona au kusikia, kuingia katika utashi wa mtu na kumfanya afanye jambo, aseme kitu au awe na mtazamo fulani ambao siyo sahihi.

Sina uhakika wa "timeline" ya matukio fulani katika maandiko ila hata maandiko yaliongelea kuhusu habari za Ayubu na kadhia alizopitia zinazoonyesha ushawishi wa shetani hapa duniani. Kwa kesi ya Ayubu, Mungu alibariki yale yatokee. Kama jambo lile limeongelewa na kuthibitishwa katika maandiko, je haina maana mambo hayo mengi yanafanyika hapa duniani? Kwa nini tunadhani ile ni kesi moja ambayo haijawahi kujirudia au hazipo kesi za namna hiyo za Shetani kumwandama mtu na kutekekeza kila kitu chake na Mungu akiwa pembeni bila kuingilia kati kumnusuru?

Ningependa uzi huu tumuongelee Shetani zaidi, yeye kama yeye na washirika wake. Tuongelee sifa zake, uwezo na nguvu zake, mbinu zake za ufanyaji kazi, mafanikio yake, mifumo au forms ambazo anaweza kujigeuza au kuingia na kufanya kazi.
 
lakini pia kuwa na maarifa na kwenyewe kumehusishwa na Shetani kwa sababu kunaweza kumfanya mtu kuwa na majivuno na kwamba majivuno yanakuja kabla ya maangamizi.
Siyo kweli kwamba mwanadamu hapaswi kuwa na maarifa ya juu.

Huo ni uongo mkuu wa Ukatoliki ulioenezwa kwa mamia ya miaka na kuwazuia watu wasisome vitabu, hasa Biblia, ili wasije wakaelimike na kuutambua ulaghai wao.

Pili, siyo maarifa pekee yanayomtia mtu kiburi na majivuno.

Kuna watu hupata kibri kwa sababu tu ya mwonekano, kabila, utaifa wake, fursa, umaarufu, nk.
Kwa hiyo kiufupi Maandiko yame discourage sana kuwa na maarifa kutokana na sababu nyingi ambazo ukiziangalia kweli zina mashiko.
Maandiko yapi? Mfalme Sulemani aliyekuwa na hekima na maarifa ya juu ameandika akisisitiza tumkamate sana elimu, wala tusimwache aende zake. Mithali 4:13.

Mtume Paulo aliyeandika sehemu kubwa ya Agano Jipya alikuwa msomi wa kiwango cha juu kwa wakati wake.
Mimi nimeanza kufikiri kuna jinsi ambayo maandiko yamepotoshwa sehemu. Upotofu unaweza kuwa kwa njia ya kuficha taarifa muhimu kuhusu mtu au kitu fulani, taarifa ambazo kama ukiwa nazo zinaweza kubadili ufahamu wako kuhusu jambo hilo.
Maandiko Matakatifu tangu Mwanzo hadi Ufunuo yako wazi kabisa kuhusu hali ya mwanadamu kwamba ni mdhambi kwa sababu ya kukubali kudanganywa na Shetani.

Kwamba njia pekee ya wokovu huja kupitia Mwana wa Mungu, Yesu Kristu. Yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima.

Neema Yake huleta ondoleo la dhambi. Hakuna jina lingine walilopewa wanadamu kwa kusudi la msamaha wa dhambi na uzima wa milele isipokuwa jina la Yesu Kristu.

Unaposema kuna jambo unahisi limefichwa, ni lipi hilo?
Tunaishi maisha ambayo hatujijui sisi ni nani, asili yetu, nguvu zetu na hata madhaifu yetu. Wakati huo huo ufahamu wa shetani ni mdogo saaana.
Sisi ni wanadamu. Tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Hiyo ndiyo asili yetu.

Kuhusu uwezo wetu, Biblia iko wazi kwamba bila Kristu sisi wanadamu hatuwezi kufanya neno lolote. Maana yake ni kwamba uwezo wetu unapatikana pale tunapomtegemea Mungu, na kukubali kuongozwa na misingi Yake.

Kuhusu madhaifu yetu, mara tunapojitenga na Mungu na kutegemea akili zetu wenyewe, basi Shetani anapata nafasi ya kutuangamiza. Mithali 3:5-8.
 
Nukta ya msingi ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa alio nao Shetani, bado hajaachwa kufanya atakavvyo 100%.

Kwa hiyo nguvu zake zimewekewa mipaka, na anatenda kile tu ambacho Mungu ameruhusu, na wala si zaidi ya hapo.
Kwa kifupi jua kwamba Shetani na malaika zake hawajaachwa wafanye watakavyo ulimwenguni, God is in control.
Mimi kuna mambo nimeshuhudia yaliyoniambia kuwa yuko active na ana nguvu na ushawishi mkubwa sana duniani.
 
Sisi ni wanadamu. Tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Hiyo ndiyo asili yetu.
Hiyo sentensi nadhani ina fumbo kubwa sana ambalo linaenda moja kwa moja kwenye moja ya maswali yangu ya msingi ya "MIMI NI NANI?" Tunaposema tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, je ina maana Mungu anafanana na mwanadamu? Lakini kwenye suala hilo siko sana kwenye muonekano, ninapohoji asili yetu nauliza swali deeper zaidi. Naongelea upande wa roho na nafsi. Naongelea uwezo wetu wa asili ni upi hasa. Nahisi binadamu amepoteza sana ufahamu wa asili yake na hii binafsi naona kama imeletwa na mafundisho ya elimu dunia na hata dini pia, respectfully.
 
Kuhusu madhaifu yetu, mara tunapojitenga na Mungu na kutegemea akili zetu wenyewe, basi Shetani anapata nafasi ya kutuangamiza. Mithali 3:5-8.
Huu ni uthibitisho wa mkanganyiko au uhaba wa maarifa ninaouongelea toka mwanzo. Muumba wetu ndiyo ametupa akili na uwezo wa kung'amua mambo, lakini hapa maandiko yanatu discourage tusitumie wala kutegemea "akili" zetu. Nadhani kula aina za "akili" ambazo maandiko hayajaweka wazi na inahitaji "akili kubwa" kuzitofautisha zile akili za kuzifuata na zile za kuwa makini nazo (uliniuliza swali kuhusu upotoshaji).
 
Nukta ya msingi ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa alio nao Shetani, bado hajaachwa kufanya atakavvyo 100%.

Kwa hiyo nguvu zake zimewekewa mipaka, na anatenda kile tu ambacho Mungu ameruhusu, na wala si zaidi ya hapo.
Ningependa tujikite katika huo uwezo mkubwa alio nao huyo shetani. Kwa mfano, je shetani kwa utashi wake anaweza kumpa mtu mafanikio hapa duniani au yeye ni muharibifu tu?

Hili ni swali la msingi sana naomba ulitafakari kabla haujalijibu na yoyote atakayependa kuchangia katika swali hili.
 
Tunaposema tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, je ina maana Mungu anafanana na mwanadamu?
Mwanadamu ndiye ameumbwa kwa ^sura na mfano^ wa Mungu. Mwonekano wa mwanadamu kimwili na kiroho viliumbwa katika namna ya kuakisi ule wa Mungu. Biblia inasema Mungu ni Roho. Yohana 4:24. Hatimaye watakatifu watakaokombolewa watapewa miili mipya. 1 Wakorintho 15:53.

Uwezo wa asili wa mwanadamu ni hulka ambayo ^ameikopa^ kutoka kwa Mungu. Adamu alipopuliziwa pumzi ya Mungu, mavumbi (mwili) ukahuishwa na kupata uhai; akili ikapata maarifa na utambuzi; akawa nafsi hai, yaani mwili wa mavumbi uliokamilishwa kwa nguvu ya pumzi ya Mungu. Mwanzo 2:7.

Maana yake nini? Ni kwamba uwezo wa mwanadamu ni hazina aliyo nayo kutoka kwa Mungu. Pasipo Mungu, mwanadamu si kitu. Bila Mungu, mwanadamu hawezi kuushinda uovu wala kumshinda Ibilisi Shetani.
Naongelea upande wa roho na nafsi. Naongelea uwezo wetu wa asili ni upi hasa. Nahisi binadamu amepoteza sana ufahamu wa asili yake na hii binafsi naona kama imeletwa na mafundisho ya elimu dunia na hata dini pia, respectfully.
^Amin, amin, nawaambieni, yeye aniaminiye Mimi [Kristu Yesu], kazi nizifanyazo Mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya.^ Yohana 14:12
 
Huu ni uthibitisho wa mkanganyiko au uhaba wa maarifa ninaouongelea toka mwanzo. Muumba wetu ndiyo ametupa akili na uwezo wa kung'amua mambo, lakini hapa maandiko yanatu discourage tusitumie wala kutegemea "akili" zetu. Nadhani kula aina za "akili" ambazo maandiko hayajaweka wazi na inahitaji "akili kubwa" kuzitofautisha zile akili za kuzifuata na zile za kuwa makini nazo (uliniuliza swali kuhusu upotoshaji).
Mwanadamu ni kiumbe mwenye utashi huru (free will). Hii ina maana kwamba anaweza kuchagua kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu au akafuata mwelekeo wa utashi wake mwenyewe.

Shetani yeye alichagua kufuata mwelekeo wa utashi wake mwenyewe, na matokeo yake ya uharibifu, mateso na mauti yanaonekana hadi leo.

Biblia inaposema ^wala msizitegemee akili zenu wenyewe,^ haina maana kwamba tusizitumie.

Maandiko hapa yanatuhadharisha tusizifanye akili zetu ndizo ziwe mwongozo wa maisha yetu.

Biblia, neno la Mungu, mapenzi ya Mungu, utashi wa Mungu, ndivyo havina budi kuwa kiongozi cha maisha yetu.

Tunapotambua hilo, na kudhamiria kwa dhati kufuata, kwa neema ya Kristu, basi mwelekeo wa akili zetu huwa salama salimini. Nje ya hapo hakuna usalama.

Halafu, ni uongo mkubwa sana wa Shetani kudhani kwamba Mungu ametuzuia maendeleo ya juu na kutuficha maarifa fulani tuwezayo kuyapata tu kwa kujiendea kadiri sisi tutakavyo.

Jaribio lake Shetani tangu kuasi hadi sasa limethibitisha, kwa mbegu ovu ambazo amepandikiza ulimwenguni na matunda yake, kwamba siyo salama hata kidogo mwanadamu kufuata utashi wake mwenyewe, huku akimpuuza Mungu.
 
Ningependa tujikite katika huo uwezo mkubwa alio nao huyo shetani. Kwa mfano, je shetani kwa utashi wake anaweza kumpa mtu mafanikio hapa duniani au yeye ni muharibifu tu?
Mbinu za Shetani za kumwangusha mwanadamu hazina idadi.

Kuna mikakati na mitego yake kulingana na makundi na aina ya watu anaowawinda.

Kwa wasomi, Shetani anaenda kisomi. Kwa wasiosoma, anatumia mradi unaoeleweka kwao kirahisi.

Kwa maskini, Shetani anatumia njia itakayowagusa na kuwavutia zaidi, na kuonekana kukidhi mahitaji yao ya wakati huo.

Kwa matajiri vilevile. Kifupi, Ibilisi ameandaa ^chambo^ mahususi kwa ajili ya kila mwanadamu . Kipo cha ^watoto^ na pia kipo cha ^watu-wazima.^
Hili ni swali la msingi sana naomba ulitafakari kabla haujalijibu na yoyote atakayependa kuchangia katika swali hili.
^Kisha Ibilisi akamchukua [Yesu] mpaka mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.^ Mathayo 4:8, 9.
 
Mwanzo mzuri. Naweza tofautiana na wewe unaposema "shetani na malaika zake hawajaachwa wafanye watakavyo ulimwenguni". Mimi kuna mambo nimeshuhudia yaliyoniambia kuwa yuko active na ana nguvu na ushawishi mkubwa sana duniani. Hapa naongelea uwezo wa kuvuruga ufahamu wa mtu, kupotosha kile anachoona au kusikia, kuingia katika utashi wa mtu na kumfanya afanye jambo, aseme kitu au awe na mtazamo fulani ambao siyo sahihi.

Sina uhakika wa "timeline" ya matukio fulani katika maandiko ila hata maandiko yaliongelea kuhusu habari za Ayubu na kadhia alizopitia zinazoonyesha ushawishi wa shetani hapa duniani. Kwa kesi ya Ayubu, Mungu alibariki yale yatokee. Kama jambo lile limeongelewa na kuthibitishwa katika maandiko, je haina maana mambo hayo mengi yanafanyika hapa duniani? Kwa nini tunadhani ile ni kesi moja ambayo haijawahi kujirudia au hazipo kesi za namna hiyo za Shetani kumwandama mtu na kutekekeza kila kitu chake na Mungu akiwa pembeni bila kuingilia kati kumnusuru?

Ningependa uzi huu tumuongelee Shetani zaidi, yeye kama yeye na washirika wake. Tuongelee sifa zake, uwezo na nguvu zake, mbinu zake za ufanyaji kazi, mafanikio yake, mifumo au forms ambazo anaweza kujigeuza au kuingia na kufanya kazi.
Shetani harandirandi mtaani kama watu wanavyofikiri, yupo locked up yeye na majeshi yake ila wameachiwa mwanya mdogo tu wa kupenyeza ushawishi kwa wanadamu. Atafanikiwa tu endapo mwanadamu amepoteza utukufu wake kwa kutenda dhambi vinginevyo labda Mungu aruhusu kwa makusudi maalumu shetani aingie kwenye maisha ya mtu.

Ni mpaka mwanadamu amruhusu shetani ndio atayaingikia maisha yake na kuyavuruga.

Waliojifungamanisha vizuri na Yesu wana nguvu na mamlaka kubwa juu ya shetani na majeshi yake!
 
Kwanza naomba mods msihamishe uzi huu kwa kuupeleka kwenye jukwaa la dini maana nataka tumjadili huyu Shetani katika misingi ya maisha yetu ya kila siku na si katika misingi ya dini.

Naileta mada hii kwa tahadhari kubwa sana. Sina nia ya kumpromote huyu jamaa ila nadhani imefika wakati tumuangalie katika uhalisia. Siwezi kuimagine dunia bila kuwa na miongozo ya maisha yenye kusisitiza upendo, amani, mshikamano na umoja kati ya wanadamu. Miongozo yote hii tumeambiwa ndiyo njia ambayo Mwenyezi Mungu anataka tupite. Shetani kwa upande mwingine tumefundishwa, mambo yake na njia zake ni potofu, ovu na zitakazopelekea uangamie katika moto wa milele. Maandiko yameenda mbali zaidi na kutuambia tajiri atapata wakati mgumu sana kuuona ufalme wa Mungu. Hili jambo ukilifirkia vizuri, linafikirisha sana.

Kutokuwa na maarifa kumeelezewa katika maandiko kuwa ni kitu hatari na kibaya, lakini pia kuwa na maarifa na kwenyewe kumehusishwa na shetani kwa sababu kunaweza kumfanya mtu kuwa na majivuno na kwamba majivuno yanakuja kabla ya maangamizi. Kwa hiyo kiufupi maandiko yame discourage sana kuwa na maarifa kutokana na sababu nyingi ambazo ukiziangalia kweli zina mashiko.

Mimi nimeanza kufikiri kuna jinsi ambayo maandiko yamepotoshwa sehemu. Upotofu unaweza kuwa kwa njia ya kuficha taarifa muhimu kuhusu mtu au kitu fulani, taarifa ambazo kama ukiwa nazo zinaweza kubadili ufahamu wako kuhusu jambo hilo. Nayasema maneno haya kwa tahadhari kubwa naomba nieleweke vizuri. Nahisi kuna watu wamehodhi maarifa haya na wanayatumia kwa ajili ya ku control watu na dunia.

Tunaishi maisha ambayo hatujijui sisi ni nani, asili yetu, nguvu zetu na hata madhaifu yetu. Wakati huo huo ufahamu wa shetani ni mdogo saaana. Ukikaa ukafikiria jinsi gani hatumjui shetani utashangaa sana. Sun Tzu aliwahi kusema ili kumshinda adui yako inabidi kwanza ujijue wewe vizuri na umjue adui yako vizuri, hapo unajiweka katika nafasi ya kushinda vita. Kama Shetani ni adui yetu namba moja kama tunavyofundishwa, nadhani tuanze kwanza kufundishana ili mimi na wewe kila mmoja wetu ajijue YEYE NI NANI na pia kuwe na mafundisho ya kutosha na deep sana kuhusu Shetani.

Uzi huu ni wa maarifa hatari. Naomba tujadili mada hii kwa staha ili wote tutoke na kitu cha kutujenga katika maisha yetu hapa duniani.
Habari yako imekaa kiimani zaidi.

Kwasababu habari ya Mungu na shetani ni hadithi tu

Hakuna Mungu, hakuna shetani katika ulimwengu halisi.

Yote haya ni mapokeo ya kidini yanayopandikizwa vichwani mwa waamini ili kuzifurahisha hisia zao.
 
Biblia inaposema ^wala msizitegemee akili zenu wenyewe,^ haina maana kwamba tusizitumie.

Maandiko hapa yanatuhadharisha tusizifanye akili zetu ndizo ziwe mwongozo wa maisha yetu.
Bado kauli hii ina ukakasi, nadhani na wewe unajua ila hautaki tu kukiri

Halafu, ni uongo mkubwa sana wa Shetani kudhani kwamba Mungu ametuzuia maendeleo ya juu na kutuficha maarifa fulani tuwezayo kuyapata tu kwa kujiendea sisi tutakavyo.
Hili si kweli, hata maneno yako yanakiri kwamba binadamu hatakiwi kufuata utashi wake mwenyewe ambayo kwa tafsiri nyingine utashi huo unaweza kuhusishwa na kutafuta maarifa na maendeleo.
 
Mbinu za Shetani za kumwangusha mwanadamu hazina idadi.

Kuna mikakati na mitego yake kulingana na makundi na aina ya watu anaowawinda.

Kwa wasomi, Shetani anaenda kisomi. Kwa wasiosoma, anatumia mradi unaoeleweka kwao kirahisi.

Kwa maskini, Shetani anatumia njia itakayowagusa na kuwavutia zaidi, na kuonekana kukidhi mahitaji yao ya wakati huo.

Kwa matajiri vilevile. Kifupi, Ibilisi ameandaa ^chambo^ mahususi kwa ajili ya kila mwanadamu . Kipo cha ^watoto^ na pia kipo cha ^watu-wazima.^
Kazi kweli kweli

^Kisha Ibilisi akamchukua [Yesu] mpaka mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.^ Mathayo 4:8, 9.
Bado haujajibu swali langu. Sijaongea mpaka umsujudie shetani, nimeongea kwa utashi wake mwenyewe hawezi kuleta hivyo?
 
Shetani harandirandi mtaani kama watu wanavyofikiri, yupo locked up yeye na majeshi yake ila wameachiwa mwanya mdogo tu wa kupenyeza ushawishi kwa wanadamu. Atafanikiwa tu endapo mwanadamu amepoteza utukufu wake kwa kutenda dhambi vinginevyo labda Mungu aruhusu kwa makusudi maalumu shetani aingie kwenye maisha ya mtu.

Ni mpaka mwanadamu amruhusu shetani ndio atayaingikia maisha yake na kuyavuruga.

Waliojifungamanisha vizuri na Yesu wana nguvu na mamlaka kubwa juu ya shetani na majeshi yake!
Hizi ni nadharia ambazo ndiyo zinatufanya tushindwe kuyaelewa haya mambo. Naomba turudi kwenye uhalisia wa kweli wa maisha
 
Habari yako imekaa kiimani zaidi.

Kwasababu habari ya Mungu na shetani ni hadithi tu

Hakuna Mungu, hakuna shetani katika ulimwengu halisi.

Yote haya ni mapokeo ya kidini yanayopandikizwa vichwani mwa waamini ili kuzifurahisha hisia zao.
Mada iko kiimani kwa kiasi fulani kwa kuanzia ila tunavyoendelea kuijadili najaribu kuwasisitizia wachangiaji wajikite katika uhalisia wa maisha na experience tunazoziona katika maisha yetu ili tumjue Shetani vizuri
 
Shetani Hayupo.

Shetani na Mungu ni fiction characters.

Hawapo.

God and Satan are Fiction characters Invented by religion.

Kwenye uhalisia shetani na Mungu Hawapo.
 
Shetani harandirandi mtaani kama watu wanavyofikiri, yupo locked up yeye na majeshi yake ila wameachiwa mwanya mdogo tu wa kupenyeza ushawishi kwa wanadamu.
Ni katika ile miaka elfu baada ya watakatifu kuingia mbinguni, ndipo Shetani atakuwa ^amefungwa asirande rande^ ili asiweze kumdanganya yeyote. Ufunuo 20:1-3.

Baada ya miaka hiyo elfu, ndipo ataangamia na kutoweka milele yeye, malaika zake waovu pamoja na wanadamu wafuasi wake ambao wamechagua kumfuata na kumtumikia, badala ya kumtii Mungu. Ufunuo 20:14.

Kabla ya muda huo, Shetani yuko kila mahali duniani alikotupwa (Ufunuo 12:9), Mikaeli alipomshinda vitani mbinguni.

Ibilisi yuko mitaani, nyumbani, kanisani, msikitini, kwenye baa, baharini, msituni, angani, na kila mahali duniani.
 
Back
Top Bottom