Kuwa na maarifa sio kujitambua

Nov 2, 2023
60
50
Maendelea ya mwanadamu yamebadilisha mfumo wake wa maisha imekuwa kila mtu ana hitaji maarifa katika utendaji wake wa kazi ili apate matokeo ya kufanikiwa. Kupata maarifa imekuwa kitu chakwanza kwenye ukuaji wa mtu yeyote. Tumekuwa bize na kutafuta maarifa ili kutimiza matakwa ya maisha yetu ya nnje tu, bila kujua tulivyo na ujinga wa kutojitambua undani wetu tulivyo ambao ndio wamuhimu zaidi katika kuishi kwetu kwa furaha na amani.

Tumeendelea na tumekuwa na maarifa sana, tumeweza kujua namna ya kurutubisha miili yetu vizuri na kufikiri tunaweza kupata matokea ya kujitambua kwa kuipa nishati akili kwa kula tu (chakula cha kuimarisha ubongo) ni tunajidanganya wenyewe. Ufahamu wa kujitambua ni jambo tofauti, ni kama una tengeneza gari kwa ubora mkubwa na kulipa nguvu kubwa lakini dereva ana ufahamu nalo lazima matokea yake yawe ni ajali na uharibifu mkubwa. Kulipa gari ubora na dereva lazima awe na ufahamu na gari ili afike salama.

Maana ya kuwa na maarifa ni kukuongezea mawazo kwenye akili yako yatayo kusaidia kuwazia na kufikiria katika utendaji wako kwenye mazingira yako. Tumekuwa tegemezi kwenye maarifa ya kupewa na kusahau wajibu wetu wakujitathmini wenyewe kwa kuwa yamekuwa ndio usalama wetu na faraja. Mtu ana jiona hana thamani kama hana maarifa yakujivunia kumpa usalama ajione na yeye ni wathamani.

Maarifa yana umuhimu katika utendaji wetu ila kujitambua nnje ya maarifa yetu kuna ulazima ili tuweze kuishi bila maarifa kutuletea madhara kwenye kuishi kwetu. Na hakuna tatizo maarifa yakitumika mahala pake. Ujinga si kutokuwa na maarifa, bali ni maarifa kukuendesha na kukupotosha kushindwa kujitambua. Tunaishi katika kutengana na kudharauliana kutokana na maarifa yetu kutofautiana.

Unachokosa sio maarifa ni ufahamu wakujitambua wewe kwanza na thamani yako. Maarifa ni kitendea kazi tu. Kwasababu ya ujinga wetu wa kutokujifahamu mwenendo wetu wa kimwili na kifikra inapelekea kutumia maarifa yetu vibaya kwa kuumiza wengine kwa kutuliza hisia zetu. Maarifa yametutengenezea vitu vingi vinavyo tuongezea uraibu wakushindwa kujitafakari wenyewe tunapopata changamoto na kukimbilia kupata tulizo huko.

Kitu cha ulazima katika akili ya binadamu yeyote kwanza ni kuwa na ufahamu wa akili yake yote kiutendaji na si kujaza maarifa mengi zaidi na zaidi. Maarifa yatakupa kuelewa kinachoendelea nnjee yako lakini ukweli halisi kukuhusu ufahamu wa ndani yako kujitambua ni lazima uwajibike na uweke maarifa yote pembeni uwe na utulivu wenye kufanya akili ijitambuwe yenyewe na kujielewa yenyewe.

Nb: Maarifa yanazidi kutuongezea vikwako kuweza kufikia kujitambua wenyewe undani wetu. Kitu kinachotuangamiza na kutukosesha furaha na amani ya maisha si kutokuwa na maarifa bali ni kuweza kujitambua undani wetu jinsi ya kuishi ndani ya ubinadamu wetu hasa hisia zetu.
 
Back
Top Bottom