Maandishi kwenye magari, tumefika huku?

Maandishi kwenye magari, tumefika huku?

emalau

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
2,775
Reaction score
3,109
Wadau jana mida ya saa moja jioni nilikuwa nikienda sehemu ya kupata moja moto moja baridi, nikiwa kwenye gari mbele yangu kuna basi moja lilikuwa mbele yangu, basi lenyewe bila kuficha ni la kampuni ya Mohamed classic.

Kilichonikera kwenye hilo basi ni bango au mudguard iliyokuwa na maneno makubwa ya ALSHABAB. Mtu akiandika maneno kama yale maana yake ni kwamba anaunga mkono wanachofanya magaidi wa alshaabab au inawezekana ni mmoja wao. Nikajiuliza je huko njiani yanakopita hakuna hata wana usalama wa kuwauliza?

Siku za nyuma pia niliwahi kuona pia pickup moja imeandikwa "Boko Haram".

Nimejaribu kuweka picha ingawa haionekani vizuri maana ilikuwa usiku

attachment.php
 

Attachments

  • maandishi.jpg
    maandishi.jpg
    52.1 KB · Views: 1,739
Mtu akisema kauli kama "nyoka huyo!!" Kawaida huwa hana maana mbaya.
Yawezeka alitaka watu wawajue vizuri Al shababu ili waweze kuepukana nao.
 
kuna lingine nililiona limeandikwa 'TUNAUZA BANGI'
 
Kuna hata timu ya mpira Uarabuni inaitwa jina hilo, nachoelewa majina hayo yana maana nzuri ila wayatumiyao for their evil motives ndo wanakosea
 
al sababy ni neno la kawaida ata kuna team inaitwa hivo misri,maana yake ni wababe
 
Huku kwetu lipo limeandikwa UTAKULA ULIPO PELEKA MBOGA,Lingine kukua kwa kifaranga sio huruma ya mwewe.
 
Jee ukikuta bus la tanga linaitwa ZAFANANA.ni la muarab kaoa mswahili waarab wenzake wakamtenga akaandika ma bus yake jina hilo
 
lipo moja limeandikwa UKIONA KAPOTEA KAMTAFUTE MAbWEPANDE, lingine JUA KALI MASTER, lingine ZIMA KIPISI MGAMBO ANAKUJA, lingine NJAA AINA BAUNSA, lingine TUKIKUMBUKA TULIKO TOKA BASI MASAI ATACHANA CHUPI, lingine BUBU UNAMFOKEA KIZIWI? lingine WATOTO WA JANGWANI, lingine .......
 
Jee ukikuta bus la tanga linaitwa ZAFANANA.ni la muarab kaoa mswahili waarab wenzake wakamtenga akaandika ma bus yake jina hilo

Mkuu hebu fafanua zaidi, sijaelewa kipi kimefanana
 
Back
Top Bottom