Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Anakua ni kero kwa wengi wanaotaka kufanya kazi
Na wanaopigaa Mipushapuu njiani ivyoo Na kuwatisha Watu ..hao hawazuii utulivu wa Watu Na kuzuia Kazi..Shirikisha kichwa cha juu Na CGA chini unapovamia mada
 
Tanzania siyo nchi Ya kwanza duniani kutumia polisi kuzuia maandamamo Yanayoruhusiwa au kutoruhusiwa kikatiba.ikumbukwe demokrasia yetu bado changa sana.ushauri wangu kwa wenye akili timamu siasa za nchi myingi za kiafrika hazidumu Ukuta ni suala la mpito tu kwenye serikali zetu za kiafrika na wanaonufaika ni wanasiasa na siyo waandamanaji.The choice is yours tarehe moko fuata unayoambiwa na wanasiasa au fuata akili yako.
 
Kwa taarifa yako, hakuna cha maandamano wala binamu yake maandamano. Hawa watu hawajaanza leo habari kama hizo, mwaka jana walisema watalinda kura lakini baada ya kupigwa marufuku hakuna aliyethubutu, pia BAVICHA walisema watakwenda Dodoma hatimaye wakaufyata. Baada ya kuona msimamo wa rais Magufuli, wameanza kuwatuma ili kutaka mazungumzo ya usuluhishi. Kibaya zaidi watu hawajahamasika kufanya maandamano.
Acha ujingaaa Wewe..hujui kitu nyamazaaa..Walisitisha Ya Dom ili iwe ya nchi mzima...Sasa kwa kunisaidia ingia mangekimambi_Instaa uone vijana wanavyofanya mazoezi msituni...ndo Utajua kama wanatania au wapo Serious. wait and see...Watu wapi serious Wewe unajifariji..si usubirii..Wewe unadhani Askari nchi nzimaa wanapenda kufanya hayo mazoezi..wameona hali si ya kupuuzia..Wangeyapuuzia Mimi ningeona kweli Chadema wapuuzi but sio wapuuzi hao ndo Maana unaona mapushapu mitaani
 
Hizo ni kelele tu hakuna atakae thubutu kuandamana siku hiyo, hawa chadema hawana ajenda ya maana tena wanachotafuta ni ku make headlines tu kwenye medani ya siasa. Wafanye wawezavyo hakuna serikali inayoweza kuchezewa kiasi hicho kama lowassa na sumaye wanawatuma viongozi masikini wa chadema kufanya upuuzi huu basi ngoja tuone
 
Hakuna maandamano watu washaanza kuomba po kijanja oh tupo tayari kwa mazungumzo Magu kimya kakaza mpaka mwisho anawasubiri mtie timu tarehe 1
So far naona kwa hii game inayoendelea ya Magu vs Chadema ni kama CDM kwa sasa wanaongoza 2-0

Nasema hivyo kwa kuwa argument kubwa ya CDM kutangaza harakati za Ukuta ilikuwa vitendo vya Magu kutoa matamko yanayoisigina Katiba ya nchi.

Hivi tokea harakati hizi za Ukuta zishike kasi, umewahi tena kumsikia Magu akitoa kauli zake za ajabu ajabu?

Nakumbuka kukurupuka kwake kwa mwisho kulikuwa ni kule kuwasihi waTz wafyatue watoto kadri waeezavyo.......

Bahati nzuri hata tamko hilo Mheshimiwa Ummy Mwalimu 'ameli-crush' kiaina baada ya kueleza kuwa mpango wa uzazi wa mpango uko pale pale na lile tamko la Mfalme la ufyatuaji watoto lilikuwa kama jokes tuu........
 
Jamaa yuko mbioni kuwa rais bomu kupita wote katika historia ya Tanzania!
It is very very true.

Kwa kila anayetafakari mambo kwa kina sana atakubaliana na analysis yako kwa 100%

So far Muhimili pekee ambao ambao nauona bado angalau Mheshimiwa wetu hajafanikiwa kuuteka kwa kiasi kikubwa ni Muhimili wa Judiciary........

Kwa kuwa tayari mhimili wa Bunge, kupitia yule mdada mteule wake aliyekalia kigoda wakati wote kipindi 'bulai' yuko kwenye matibabu India alishageuza vikao vya Bunge sawasawa na vikao vya NEC ya CCM.......

Watanzania tuendelee kumwomba Mungu huyo jamaa asifanikiwe 'kuuteka' mhimili wa Judiciary kama alivyofanikiwa 'kuuteka' mhimili wa Bunge, kwa kuwa ikifikia hatua hiyo maana yake Tanzania itakuwa inaelekea kuzimu........
 
Mkuu hata maandamano yasipokuwepo ila kwa rais tayari ameshafungwa speed gavana ya tabia zake. Ni kweli kwa sasa atakuwa mshindi lakini kwa namna moja ama nyingine tabia yake iko hadharani tayari. Watoto wa mjini wanasema message sent. Hivyo inatoa nafasi ya huko mbeleni akiendelea na tabia zake kupingwa kwa nguvu zaidi. Nikuhakikishie hata yeye amegundua kabisa kwamba cheo alichovaa sio cha kufanya ayatakayo kwani ameshajua dhahiri haongozi familia yake. Ni nadra kwa mkubwa kukiri hadharani ila kwa siku mbili hizi amepata mrejesho baada ya hao polisi kuuliwa amejua maamuzi yake yamepandikiza chuki kiasi gani na sio hofu kama alivyotarajia. Kwa bahati mbaya wanaomzunguka wanaoogopa kumwambia kwamba anavyoipeleka nchi sio. Nadhani unaona polisi wanavyojikakamua kutoa vitisho kwa umma, ila hata wao wanajua kwamba rais kawaweka kwenye wakati mgumu bila sababu ya msingi ila tu wakale wapi. Tutarajie viongozi wa dini watakaokutana naye pamoja na viongozi wengine watamwambia awe muangalifu kwani haiba yake kwenye jamii imeingia doa. Nataka nikuhakikishie kwa aina ya tabia zake yoyote atakayejitokeza kuandamana ajiandae kukutana na kipigo kitakatifu kwani jamaa anajali ushindi hata kama ni wa fedheha. Huwa hajiulizi madhara ya maamuzi yake bali hujuta baada, je watanzania walio wengi wako kama wakenya wanaojitambua kwenye kudai haki zao? Hilo ni suala la kusubiri na kuona.
Kwa analysis yako iliyokwenda shule pokea LIKES zangu kama 100 hivi.........
 
It is very very true.

Kwa kila anayetafakari mambo kwa kina sana atakubaliana na analysis yako kwa 100%

So far Muhimili pekee ambao ambao nauona bado angalau Mheshimiwa wetu hajafanikiwa kuuteka kwa kiasi kikubwa ni Muhimili wa Judiciary........

Kwa kuwa tayari mhimili wa Bunge, kupitia yule mdada mteule wake aliyekalia kigoda wakati wote kipindi 'bulai' yuko kwenye matibabu India alishageuza vikao vya Bunge sawasawa na vikao vya NEC ya CCM.......

Watanzania tuendelee kumwomba Mungu huyo jamaa asifanikiwe 'kuuteka' mhimili wa Judiciary kama alivyofanikiwa 'kuuteka' mhimili wa Bunge, kwa kuwa ikifikia hatua hiyo maana yake Tanzania itakuwa inaelekea kuzimu........
Kila raisi Ana mapungufu yake,hakuna raisi anayependwa na asilimia Mia moja ya wananchi wake na anaedai anapendwa na wote huyo ndio dikteta,na humu ndani kuna wachangiaji wengi wasipenda na wanaompenda magufuli kwa mimi binafsi sioni udikteta wa magufuli bali ni siasa tu katala nchi ambayo bado ni changa kidemokrasia.
 
Utakuwa hujanielewa nilichoongea.

Sijaongelea kuhusu JPM kama ni Rais anayependwa na wananchi wake au laa.

Nilichojaribu kueleza ni kuwa siyo hiari ya Rais aliyeko madarakani kutawala kwa kuitii Katiba, bali ni wajibu wake kwa asilimia 100, kwa kuwa Kabla hajaingia madarakani aliapishwa pale uwanja wa Taifa tarehe 5/11 /2015 na akakiri mwenyewe kwa kinywa chake kuwa ataitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu.

Vitendo vyake vya kuisigina Katiba ya nchi waziwazi, vinatufanya waTz hivi sasa tuikumbuke sana hotuba ya hekima ya hali ya juu aliyoitoa Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere, mwaka 1995, wakati aliposema kuwa Rais tunayemchagua ni lazima aitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu aliyoapa kuilinda, Mwalimu aliendelea kusema kwenye hotuba hiyo kwa msisitizo mkubwa kuwa Rais asiyetaka kuitii Katiba ya nchi yetu Rais wa aina hiyo HATUFAI.........
 
Mleta uzi wewe ni koyoyo... I hate guys who are kissing others guys ass... duniani hakuna Mtukufu isipokuwa Mungu pekee.Sasa wewe kumuita binadamu mwenzako mtukufu ni sawa na kumkufuru Mungu..hizi njaa ZENU na kujipendekeza kwenu kutawapeleka pabaya

Swissyou
Ndivyo anavyotaka kuitwa aka Rais wa Malaika.Huyo aaiyetaka kukosolewa ni nani zaidi ya Mungu.Kama Mungu tu anakosolewa basi ujue tuliye naye ni Mtukufu sana Matakatifu asiyena dhambi Rais wa Malaika ambaye ni zaidi ya Mungu
 
Utakuwa hujanielewa nilichoongea.

Sijaongelea kuhusu JPM kama ni Rais anayependwa na wananchi wake au laa.

Nilichojaribu kueleza ni kuwa siyo hiari ya Rais aliyeko madarakani kutawala kwa kuitii Katiba, bali ni wajibu wake kwa asilimia 100, kwa kuwa Kabla hajaingia madarakani aliapishwa pale uwanja wa Taifa tarehe 5/11 /2015 na akakiri mwenyewe kwa kinywa chake kuwa ataitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu.

Vitendo vyake vya kuisigina Katiba ya nchi waziwazi, vinatufanya waTz hivi sasa tuikumbuke sana hotuba ya hekima ya hali ya juu aliyoitoa Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere, mwaka 1995, wakati aliposema kuwa Rais tunayemchagua ni lazima aitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu aliyoapa kuilinda, Mwalimu aliendelea kusema kwenye hotuba hiyo kwa msisitizo mkubwa kuwa Rais asiyetaka kuitii Katiba ya nchi yetu Rais wa aina hiyo HATUFAI.........
Mheshimi
 
Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.

Je wakifanikiwa kufanya hayo maandamano lkn muafaka wa matakwa yao usipatikane kama tulivyoona bungeni walipozila kuhudhulia vikao, tafsiri yake itakuwa ni nini?
 
Wasipoandamana magu atatamba sana kwamba yeye hajaribiwi na upinzani utanyanyaswa mara nne zaidi ya sasa.
Kuzuiwa mikutano maana yake upinzani utakufa hakuna siasa za mtu mmoja mmoja.
Na bungeni watakuwa wasindikizaji tu.
Ni kweli hajaribiwi, nipo hapa Moshi kumetulia kama barafu ya mlima wake, wananchi wameishachoka vibaya na fujo fujo, hawataki kusikia hizo habari za kupanga matofari kwa simenti.
 
Miaka 2 ijayo usishangae tukiambiwa tumuabudu huyu jamaa. Tanzania huru kwaheri karibu Somali
 
Mkuu hata maandamano yasipokuwepo ila kwa rais tayari ameshafungwa speed gavana ya tabia zake. Ni kweli kwa sasa atakuwa mshindi lakini kwa namna moja ama nyingine tabia yake iko hadharani tayari. Watoto wa mjini wanasema message sent. Hivyo inatoa nafasi ya huko mbeleni akiendelea na tabia zake kupingwa kwa nguvu zaidi. Nikuhakikishie hata yeye amegundua kabisa kwamba cheo alichovaa sio cha kufanya ayatakayo kwani ameshajua dhahiri haongozi familia yake. Ni nadra kwa mkubwa kukiri hadharani ila kwa siku mbili hizi amepata mrejesho baada ya hao polisi kuuliwa amejua maamuzi yake yamepandikiza chuki kiasi gani na sio hofu kama alivyotarajia. Kwa bahati mbaya wanaomzunguka wanaoogopa kumwambia kwamba anavyoipeleka nchi sio. Nadhani unaona polisi wanavyojikakamua kutoa vitisho kwa umma, ila hata wao wanajua kwamba rais kawaweka kwenye wakati mgumu bila sababu ya msingi ila tu wakale wapi. Tutarajie viongozi wa dini watakaokutana naye pamoja na viongozi wengine watamwambia awe muangalifu kwani haiba yake kwenye jamii imeingia doa. Nataka nikuhakikishie kwa aina ya tabia zake yoyote atakayejitokeza kuandamana ajiandae kukutana na kipigo kitakatifu kwani jamaa anajali ushindi hata kama ni wa fedheha. Huwa hajiulizi madhara ya maamuzi yake bali hujuta baada, je watanzania walio wengi wako kama wakenya wanaojitambua kwenye kudai haki zao? Hilo ni suala la kusubiri na kuona.

Mkuu tindo

Unataka tuamini na unatuhakikishia kuwa yale mauwaji ya polisi yamesababiswa na maandalizi ya UKUTA na si tukio la ujambazi kama ilivyoripotiwa na vyombo vya usalama?
 
Plan B.maandamano yafanyike usiku na polisi itoe kibali
 
Mleta uzi wewe ni koyoyo... I hate guys who are kissing others guys ass... duniani hakuna Mtukufu isipokuwa Mungu pekee.Sasa wewe kumuita binadamu mwenzako mtukufu ni sawa na kumkufuru Mungu..hizi njaa ZENU na kujipendekeza kwenu kutawapeleka pabaya

Swissyou

Unajua maana ya "sarcasm" ?
 
Back
Top Bottom