Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.
Maandamano yasipokuwepo siku hiyo itabidi uache kubeba box uje huku bongo na kuimba USA baby barabarani.
 
Maandamano hakuna.Haiwezekani kukaidi amri za polisi.
 
Mkuu umenikumbusha, nina supavaiza wangu ana degree ya Plumbing basi usipomwita bila ya prefix ya Engineer lazima akupige paper. Anataka aitwe Engineer Eliuforo Nkya Mushi...

😀😀😀😀
 
Wasiwasi wangu itakapofika 2020, itatumika dola kuzuia uchaguzi. Hapo ndipo mtakapojua kama udikteta starehe au ni janga.
 
Mkuu hata maandamano yasipokuwepo ila kwa rais tayari ameshafungwa speed gavana ya tabia zake. Ni kweli kwa sasa atakuwa mshindi lakini kwa namna moja ama nyingine tabia yake iko hadharani tayari. Watoto wa mjini wanasema message sent. Hivyo inatoa nafasi ya huko mbeleni akiendelea na tabia zake kupingwa kwa nguvu zaidi. Nikuhakikishie hata yeye amegundua kabisa kwamba cheo alichovaa sio cha kufanya ayatakayo kwani ameshajua dhahiri haongozi familia yake. Ni nadra kwa mkubwa kukiri hadharani ila kwa siku mbili hizi amepata mrejesho baada ya hao polisi kuuliwa amejua maamuzi yake yamepandikiza chuki kiasi gani na sio hofu kama alivyotarajia. Kwa bahati mbaya wanaomzunguka wanaoogopa kumwambia kwamba anavyoipeleka nchi sio. Nadhani unaona polisi wanavyojikakamua kutoa vitisho kwa umma, ila hata wao wanajua kwamba rais kawaweka kwenye wakati mgumu bila sababu ya msingi ila tu wakale wapi. Tutarajie viongozi wa dini watakaokutana naye pamoja na viongozi wengine watamwambia awe muangalifu kwani haiba yake kwenye jamii imeingia doa. Nataka nikuhakikishie kwa aina ya tabia zake yoyote atakayejitokeza kuandamana ajiandae kukutana na kipigo kitakatifu kwani jamaa anajali ushindi hata kama ni wa fedheha. Huwa hajiulizi madhara ya maamuzi yake bali hujuta baada, je watanzania walio wengi wako kama wakenya wanaojitambua kwenye kudai haki zao? Hilo ni suala la kusubiri na kuona.
Magu hakutani na viongozi wa dini..
Pia chunga kauli zako za kusema kuwa meseji senti kwa kule kuuliwa kwa polisi..
Anagakia wasije wakakuweka katika kundi la wanaofurahia kuuliwa kwa polisi.. Na hapo ndipo unapoweza ukawapa uwakika wa mawzo yao kuwa siasa ya upand efulani wanahusika na hili.. Yaani kuhusianisha ukuta na mauaji haya....
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Yasipofanyika chadema itapoteza mvuto, watu hawatilia maanani kauli zao tena. Watakuwa sawa na mbwa wasio na meno.

Watu watakata tamaa kufuatilia mambo ya kisiasa, 2020 ccm watajipa ushindi tena.

Magu atatoka kwenye uchwara na kuwa halisi.

"This was their finest hour" - Winston Churchill.
 
Mleta uzi wewe ni koyoyo... I hate guys who are kissing others guys ass... duniani hakuna Mtukufu isipokuwa Mungu pekee.Sasa wewe kumuita binadamu mwenzako mtukufu ni sawa na kumkufuru Mungu..hizi njaa ZENU na kujipendekeza kwenu kutawapeleka pabaya

Swissyou
Wala hajipendekezi mkuu kapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Magu hakutani na viongozi wa dini..
Pia chunga kauli zako za kusema kuwa meseji senti kwa kule kuuliwa kwa polisi..
Anagakia wasije wakakuweka katika kundi la wanaofurahia kuuliwa kwa polisi.. Na hapo ndipo unapoweza ukawapa uwakika wa mawzo yao kuwa siasa ya upand efulani wanahusika na hili.. Yaani kuhusianisha ukuta na mauaji haya....

Mkuu mimi siongozwi na kutoa maoni yangu kwa hofu kama ambavyo wewe unafanya. Kinachosababisha watu watishie watu kutoa maoni ni maamuzi ya jazba ambayo hayawezi kuwa suluhisho la tatizo zaidi ya kufunika kombe mwanaharamu... Hao wanaotoa vitisho sidhani kama lengo lao ni kupata suluhisho la tatizo bali ni wale wanaoshinda hapa kwenye mitandao ya kijamii kusaka mchawi badala kupambana na tatizo.

Hii hali inanikumbusha wakati nasoma kuna jamaa mmoja alikuwa anajifanya mbabe sana, basi siku moja akakutana na mbabe wake, kwa kweli alipigwa vizuri, basi akawa anatutishia eti tusicheke kwa kuwa kapigwa. Ila ukweli ulibaki kwamba kapigwa. Hao wanaotoa vitisho hivyo ni wale wanaofanya kazi bila weledi maana huwezi kuzuia watu kusema kwani wengi wa wanaosema hapa mitandaoni ni wale wanaongozwa na mihemuko ya kisiasa, kwa kuona kwamba kundi lao linanyanyaswa na polisi hivyo wanaona ngoja na polisi nao wahisi maumivu kama wao wanavyoona kuonewa.

Ni kweli unachosema wanaweza kunikamata, lakini hilo halimaanishi kwamba mimi kwa kuongea ndiye niliyefanya tukio hilo, na iwapo wataona kwamba mimi ndio nahusika na ikaishia hapo ukweli utabaki kwamba hizo silaha bado ziko mikononi mwa wahalifu, je watakuwa wametatua tatizo? Na kama polisi wanafanya kazi hivyo ya kukamata tu aliyeongea nani atashindwa kazi hiyo? Maana kazi hiyo itakuwa unashinda hapa mitandaoni ukisikia tatizo basi yoyote anayechangia kinyume na jazba zako unamkamata.

Nikuambie kitu ndugu yangu tuwe wakweli, polisi wapitie huku kwenye mitandao ya kijamii wasikie ukweli mchungu maana huku ndio watajua ni wapi wanakosea na ni vipi wabadilike kwa faida ya kazi yao na taifa.
 
Kwa taarifa yako, hakuna cha maandamano wala binamu yake maandamano. Hawa watu hawajaanza leo habari kama hizo, mwaka jana walisema watalinda kura lakini baada ya kupigwa marufuku hakuna aliyethubutu, pia BAVICHA walisema watakwenda Dodoma hatimaye wakaufyata. Baada ya kuona msimamo wa rais Magufuli, wameanza kuwatuma ili kutaka mazungumzo ya usuluhishi. Kibaya zaidi watu hawajahamasika kufanya maandamano.
 
Mandamano hayafanyiki na wachora katuni wataendelea kuchora!

Hizi kelele sio mpya na haziwezi kumalizika mpaka pale wapiga kelele watakapo tembea katika maneno yao kwa sababu vyama vinavyopiga kelele kuhusu demokrasia havina hata misingi ya demokrasia ndani ya vyama vyao.

CHADEMA wamechukua jukumu kubwa ambalo kwa sasa liko juu ya uwezo wao kama chama.

“...Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country. I never went to a country, saw many parties and assumed that it is democratic. You cannot define democracy purely in terms of multi-partist parties...”-Mwl. Nyerere.

Tanzania is unique country!

CUF 2001 yalikua kama haya..na walifanya ....bora yaruhusiwe tu na polisi wetu walinde amani..wataenda watapiga kelele uwanjani , wakimaliza wanarudi nyumbani kula ugali..why so much tension ? ukiwaruhusu hawazidishi hawapunguzi ..
 
Screenshot_2016-08-22-07-42-17-1.png

Makamanda nimekutana na hii picha sehemu lakini tusiogope tarehe 1 lazima tuandamane.
 
Hata mimi nadhani hivyo. Naona kama mtu mwenye personality na falsafa ya kiuongozi kama ya Magufuli anahitaji force kubwa ya kumpinga kumuwezesha kuamka na kuona kuwa hayuko kwenye njia sahihi. Isipokuwepo force kama hiyo, mithili ya hii "ukuta" (kama itafanikiwa), tegemea kuona matukio mengi zaidi ya kidikteta huko mbeleni.
 
Mleta uzi wewe ni koyoyo... I hate guys who are kissing others guys ass... duniani hakuna Mtukufu isipokuwa Mungu pekee.Sasa wewe kumuita binadamu mwenzako mtukufu ni sawa na kumkufuru Mungu..hizi njaa ZENU na kujipendekeza kwenu kutawapeleka pabaya

Swissyou
Na wewe Sijui Ni mgeni humu ndaniii au umevamia jukwaa..Huyoo unayemsema yupo Na UKUTA Ila ametoa angalizo Na kuita ivyo mtukufu sidhani kama anamaanisha zaidi ya kuendeleza jejeli A lisuuuuu..Sasa MTU kama anasema yy hajaribiwi..tumwitejeeee. Ebu soma tena then umuombe msamaha
 
Back
Top Bottom