Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.
Hivi upo Tanzania au upo diaspora? Usituhamasishe wakati wewe upo ughaibuni.
 
Mleta uzi wewe ni koyoyo... I hate guys who are kissing others guys ass... duniani hakuna Mtukufu isipokuwa Mungu pekee.Sasa wewe kumuita binadamu mwenzako mtukufu ni sawa na kumkufuru Mungu..hizi njaa ZENU na kujipendekeza kwenu kutawapeleka pabaya

Swissyou
Nadhani somo la lugha kwako lilikua shida kidogo ulipokua shule
 
Hivi upo Tanzania au upo diaspora? Usituhamasishe wakati wewe upo ughaibuni.

Ona mhanga mwingine ajuaye kusoma lakini asiyeelewa akisomacho!

Mimi nimewahamasisha wapi na nimewahamasishaje?
 
Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.
Tukisema kuwa wewe ndie mastermind na mpangaji wa vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyopangwa na ukawa utakataa. Nadhani ujiandae kutoa maelezo kwenye vyombo vya dola. Watu bado tunataka kuishi tena kwa amani. Biashara yenu ya ukuta hatuitaki na tunaikemea. mnataka kuongopea vijana wetu muwatoe ngeu na mwisho nyinyi ndio mfaidike. Jahahaha
 
Wasipoandamana kwa kuogopa vitisho vya MTUKUFU, basi tatizo ni uvunjwaji wa katiba na sheria.
Wakiandamana baada ya kupewa onyo na vyombo vya dola ina maana vyombo vya dola viko weak na yoyote anaweza kuamua kufanya maandamano kwa sababu za kipuuzi tu yaani kila kukicha itakuwa ni maandamano.
 
Kwa hili...cdm nahisi wamejitega wenyewe...sina uhakika na uwepo wa maandamano kwa hiyo tarehe.
Na kwa jinsi ukuTA ulivyotangazwa na pande zote.....mshindi atakaetokea hapo, atadumu sana kuwa juu. Atasikilizwa kwa kiwango kikubwa.
 
Wakiandamana baada ya kupewa onyo na vyombo vya dola ina maana vyombo vya dola viko weak na yoyote anaweza kuamua kufanya maandamano kwa sababu za kipuuzi tu yaani kila kukicha itakuwa ni maandamano.

Mtu kuandamana kwa sababu za kipuuzi kuna ubaya gani?
 
Hakuna maandamano watu washaanza kuomba po kijanja oh tupo tayari kwa mazungumzo Magu kimya kakaza mpaka mwisho anawasubiri mtie timu tarehe 1
 
Wasipoandamana magu atatamba sana kwamba yeye hajaribiwi na upinzani utanyanyaswa mara nne zaidi ya sasa.
Kuzuiwa mikutano maana yake upinzani utakufa hakuna siasa za mtu mmoja mmoja.
Na bungeni watakuwa wasindikizaji tu.
 
This will be their acid test.

Mkuu hata maandamano yasipokuwepo ila kwa rais tayari ameshafungwa speed gavana ya tabia zake. Ni kweli kwa sasa atakuwa mshindi lakini kwa namna moja ama nyingine tabia yake iko hadharani tayari. Watoto wa mjini wanasema message sent. Hivyo inatoa nafasi ya huko mbeleni akiendelea na tabia zake kupingwa kwa nguvu zaidi. Nikuhakikishie hata yeye amegundua kabisa kwamba cheo alichovaa sio cha kufanya ayatakayo kwani ameshajua dhahiri haongozi familia yake. Ni nadra kwa mkubwa kukiri hadharani ila kwa siku mbili hizi amepata mrejesho baada ya hao polisi kuuliwa amejua maamuzi yake yamepandikiza chuki kiasi gani na sio hofu kama alivyotarajia.

Kwa bahati mbaya wanaomzunguka wanaoogopa kumwambia kwamba anavyoipeleka nchi sio. Nadhani unaona polisi wanavyojikakamua kutoa vitisho kwa umma, ila hata wao wanajua kwamba rais kawaweka kwenye wakati mgumu bila sababu ya msingi ila tu wakale wapi.

Tutarajie viongozi wa dini watakaokutana naye pamoja na viongozi wengine watamwambia awe muangalifu kwani haiba yake kwenye jamii imeingia doa. Nataka nikuhakikishie kwa aina ya tabia zake yoyote atakayejitokeza kuandamana ajiandae kukutana na kipigo kitakatifu kwani jamaa anajali ushindi hata kama ni wa fedheha.

Huwa hajiulizi madhara ya maamuzi yake bali hujuta baada, je watanzania walio wengi wako kama wakenya wanaojitambua kwenye kudai haki zao? Hilo ni suala la kusubiri na kuona.
 
CHADEMA wakirudi nyuma tu, basi harakati zao zote huko mbeleni zitaonekana kama kelele za chura.
Madhara yake hayatakuwa kwa chadema tu, labda hapa mwanzoni. lakini baadaye, maamuzi yatakayotokana na ushindi huo wa mwenye enzi yatakuwa machungu kwa kila mtu. Ni suala la muda tu. japo watu wanacheka leo, ipo siku tutashirikiana kulalama na kulia.
 
wacha uchochezi wewe. hayo maandamano
kwani yana ulazima kama sio cdm kujitutumua tu na kujaribu kumyumbisha rais.
Wanamyumbisha vipi Rais? kwani kama akiruhusu wapinzani wafanye siasa zao nani ataleta maneno? Halafu, kwani kuandamana ni mapinduzi?
 
..hata yasipofanyika tayari cdm wameshashinda.

..magufuli amekuwa exposed na kupoteza ule mvuto aliokuwa nao mwanzo.

..pia uwezekano wa kutoa kauli za hovyo-hovyo siku nyingine ni mkubwa sana. Upo uwezekano akazua jambo lingine litakaloturudisha hapa tulipo.

..mimi ningekuwa mshauri wa Magufuli ningemwambia ufute kauli yake na kuruhusu mikutano na maandamano.

The Boss, Nyani Ngabu
 
Back
Top Bottom