Maandamano ya kumtaka Benjamin Netanyahu aachie madaraka na uchaguzi uitishwe yameiingia hatua ya juu

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,186
10,922
Maandamano ya kumtaka Benjamin Netanyahu aachie madaraka na uchaguzi uitishwe yameiingia hatua ya juu leo pale waandamanaji kwenye mitaa tofauti ya Tel Aviv kuziba njia kuu za usafiri.

Hata hivyo Netanyahu pekee ndiye amekuwa na tamaa ya fisi ya kuishinda Hamas ambapo ametoa amri ya jeshi lake kuingia Rafah japo kumekuwa na makelele kutoka kila upande kumtaka asishambulie eneo hilo kwa hofu ya kusababisha vifo vingi na wengine wakiona anaweza akatibua hali ya vita kuwa vibaya zaidi.

Generali mstaafu wa jeshi la anga la Jordan kwa upande wake amelitahadharisha jeshi la Israel juu ya uwezekano wa kupata hasara kubwa kwa jeshi lake na kwa wananchi bila kupata mafanikio ya kuwafuta Hamas.Katika tamko lake generali huyo amesema mahandaki yamejaa Gaza yote lakini yale ya Rafah yametengenezwa kwa utaalamu zaidi na si rahisi kuyapenya.

Habari nyengine ni taarifa iliyotolewa na kikosi cha Islamic Jihadi ambacho kimerusha kwenye chaneli yao ya telegramu wakidai siku ya leo wamepiga kikundi cha askari wa IDF maeneo ya kambi ya wakimbizi ya Al maghazi iliyopo katikati ya Ghaza
kutokea kwa shambulio hilo kubwa eneo ambalo Israel imeshapita na kutangaza ushindi pamoja na tahadhari ya generali mstaafu wa Jordan na ukimya wa Misri kuelekea utekelezwaji wa amri ya kushambulia Rafah kunatoa picha kuwa kuna kipigo kikubwa kitatokea kwa jeshi la Israel na ambalo ndilo litakalomaliza vita na kumuondoa Netanyahu madarakani.
 
Acha ushabiki wakijinga wakati Wapalestina wanaumia na kuzidi kufa huko huku wewe unatuletea story zako za kiitikadi.

Misri chini Al Sisi ni mshirika mkubwa sana wa Israel na US, chochote akifanyacho ni maelekezo kutoka kwa hao wawili. The same to to King Abdullah of Jordan. Muwe mnafatilia mambo muelewe siasa za Mashariki ya kati zinaendaje badala ya kukurupuka tu.

Hapo Mashariki ya kati kama sio mshirika wa Israel na US haukai madarakani utatolewa tu namna yeyote
 
Maandamano ya kumtaka Benjamin Netanyahu aachie madaraka na uchaguzi uitishwe yameiingia hatua ya juu leo pale waandamanaji kwenye mitaa tofauti ya Tel Aviv kuziba njia kuu za usafiri...
Aende tu hana faida kama kima!
 
Yalikuwepo maandamano makubwa kabla ya hayo, hajaondoka. Hayo ya sasa no cha mtoto tu. Netanyahu ndio Baba wa Siasa za Israel.

Ukumbuke sera ya Israel dhidi ya wapalestina haibadiliki, hata akija kiongozi gani. Usijifariji na hilo la maandamano kana kwamba litawapa afueni wapalestina.
 
Utekelezwaji wa amri ya kushambulia Rafah kunatoa picha kuwa kuna kipigo kikubwa kitatokea kwa jeshi la Israel na ambalo ndilo litakalomaliza vita na kumuondoa Netanyahu madarakani.
Kuna muda unaandika upumbavu ambao ata wewe mwenyewe ukisoma unashangaa

Hapo Rafah pakishambuliwa maiti za watoto na kina Mama zitakua si chini ya 50 elfu lakn kwa kutumia mahaba ya dini et "kunakipigo kikubwa kitatokea kwa jeshi la Israel"

Hivi hizi akili waga mnatoa wapi?

Jumuia yote ya kinataifa inakataza Israel kuvamia Rafah kuepusha casualties and fatalities Kwa raia wasio na hatia Lakini unakuja apa jukwaani na mahaba yako ya kijinga et kunakipigo kikubwa hahaha

Hamas kama hawawapendi hao raia wao warushe rocket kutoka apo Rafah utaona Israel walivyo vichaa hawasikilizi sijui UN wala human Right
 
Kuna muda unaandika upumbavu ambao ata wewe mwenyewe ukisoma unashangaa

Hapo Rafah pakishambuliwa maiti za watoto na kina Mama zitakua si chini ya 50 elfu lakn kwa kutumia mahaba ya dini et "kunakipigo kikubwa kitatokea kwa jeshi la Israel"

Hivi hizi akili waga mnatoa wapi?

Jumuia yote ya kinataifa inakataza Israel kuvamia Rafah kuepusha casualties and fatalities Kwa raia wasio na hatia Lakini unakuja apa jukwaani na mahaba yako ya kijinga et kunakipigo kikubwa hahaha

Hamas kama hawawapendi hao raia wao warushe rocket kutoka apo Rafah utaona Israel walivyo vichaa hawasikilizi sijui UN wala human Right
hakuna cha ushabiki hapo,kwenye vita kufa hakukwepeki...israel vichaa ila wanapigika vizuri tu ngoja vianze kupigwa tuone,kwani tumejionea maelfu ya vifo na vilema wa IDF kule GAZA

hasara waliyoipata GAZA na hakuna walichopata haisemeki kilichobaki ni kujitutumua tu coz washajisifia sana wao kiboko watafanyaje zaidi ya kujitutumua
 
Back
Top Bottom