Maandamano ya Kumsapoti JK Washington DC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya Kumsapoti JK Washington DC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki, Aug 12, 2011.

 1. H

  Haki JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna jitihada kubwa zinafanyika kuhakikisha Rais JK anapokewa kwa heshima atakapokuja Washington. Watanzania mnaombwa kushiriki kwa wingi ktk Ubalozi wa TZ uliopo Washington DC kumpa Support na changamoto Rais JK ambaya alishinda uchaguzi 2010. WTZ mliopo Marekania mnaombwa mjitokeze kwa wingi kumpa Support Rais JK.

  Mpenda Haki, na Ukweli.
  NY, USA
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 28,854
  Likes Received: 29,066
  Trophy Points: 280
  Huko hakuna mabasi wala malori ya kukusanya watu kama kawaida yenu. Hizi ni imagination zako umeamua kutushirikisha.
   
 3. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Waraka huu ni kwako wewe hasidi wa upendo, utulivu, na amani ya taifa letu la Tanzania unayejiita Eliakim Mallya na wapuuzi wenzako. Sina uhakika kama kweli jina hilo ulilotoa ni lako, maana kina cha woga na ujinga ulionao, havikuwezeshi wewe kuwa na ushujaa wa kutoa jina lako la kweli. Ninasikitika kwamba imebidi watu wenye heshima zetu tukae chini kutoa kauli kuhusiana na upumbavu uliowekwa kwenye mtandao na mtu asiyekuwa na heshima wala adabu kama wewe, na wapuuzi wenzako wengine mlioko katika kapu moja.
  Kwanza, tendo la kumvunjia heshima kiongozi wa taifa letu kwa kutoa kashifa iliyotolewa, pia ni tendo la kulivunjia heshima taifa letu na watu wake, jambo ambalo linakufanya wewe Eliakim Mallya na wote mnaohusika na kashifa hii kuwa mahayawani, maana hayawani hana aibu.

  Pili, ukosefu wa utimamu wa akili yenu nyie mhusikao na kashifa hii, pia unajidhihirisha kwa jinsi mlivyojaribu kukosea heshima Watanzania tunaoishi Marekani kwa kujifanya kutuwakilisha wakati nyie ni vivuli. Ni mtu gani awezaye kusikiliza maneno yatokayo kwenye vinywa vya wapumbavu? Ninawajutia kuwa mmesoma kwa kiasi fulani lakini hamkuelimika hata kidogo.

  Tatu, ninyi ni viumbe msiokuwa na tone la shukurani kwani pamoja na kwamba Tanzania iliwasomesha na kuwafikisha hapo mlipo (hamwezi kulikataa hilo), mnaanza kuisaliti na kuibeza. Hali kadhalika ninyi ni wasaliti wa utamaduni, mila na desturi za taifa letu na watu wake. Hadhi ya Watanzania iko katika kauli zao njema nyumbani na hata ughaibuni-mahali popote walipo. Taifa letu limepata sifa kubwa sana kutokana na ubora na mwenendo wa tabia za watu wake dunia nzima. Leo hii, watu wachache mliochanganyikiwa mnataka kuupaka matope ubora wetu; hatutaruhusu wala kukubali vitendo na mienendo ya kihuni.

  Nne, wahenga walisema debe shinda haliachi kutika, na debe tupu haliachi kuvuma; ninyi mlionena na kuchapisha uvundo wenu huu, ni mifafano dhahiri ya methali hizo. Kwa vile Eliakim Mallya na wenzako mmetota, endeleeni kutota katika tope la ujinga na utovu wa adabu kama walivyo wahaini wa aina yenu.

  Mwesigwa. Blandesi
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nyie mafisadi mmefulia. tutakutana kwenye maandamano
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 28,854
  Likes Received: 29,066
  Trophy Points: 280
  Unathubutu kujiita mtu mwenye heshima kwa upupu huu ulioandika? Kumbe maandamano ya kumpinga JK washngton yanawaumiza kichwa??? Ni lazima mataifa yajue upuuzi wake pindi atakapokanyaga Washington DC.
   
 6. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,004
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  ninachotaka kukwambia ni kwamba, j.k. hakushinda mwaka jana.
   
 7. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 1,308
  Trophy Points: 280
  Yaani mnaficha maovu yake? Kumpongeza kwa lipi? Labda kwa kuwa mtanzania anayesafiri kuliko wote! :(
   
 8. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,796
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  natamani ningekuwa na mie huko NY kuandamana.....JK mpaka akione cha moto lol
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 3,574
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  .....@ New York City
   
 10. wende

  wende JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 707
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Eliakim mallya tupo pa1!
   
 11. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mtaweweseka sana mwaka huu , magamba yamegoma kuvuka, mnatwangwa kotekote, ndani na nje ya nchi, masaburi yenu
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 1,989
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Jamani tuanaomba tufanye mkutano wetu wa diaspora bila siasa kama kuna siasa pelekeni ubalozi wakati raisi atakapokuja au nendeni UN NY lakini msije kwenye Hotel ambayo sisi tumelipia na tukaalika wageni mbalimbali halafu ibadilike kuwa sehemu ya maandamano!. Mwaka jana tulifanya mkutano MN bila mambo kama haya na raisi hakuwepo na kama maandamano yatakuwepo tutamuomba raisi Kikwete asije kwenye Hotel ya mkutano wa diaspora kwani si lazima tuwe na raisi pale raisi hajawahi kuja kwenye mkutano hata mmoja!. labda hilo litawafurahisha lakini kama ni maandamano ningeomba mpeleke UN kwani huu mkutano wetu wa diaspora tunaweza kumuomba raisi asije na nyie mkawa mmepoteza pesa zenu bure!!. Kama mnataka uhakika nendeni UN siku atakapoongea mtampaka kwa uhakika kwani sisi hatutaruhusu raisi aje kama kuna maandamano ya kisiasa!!
   
 13. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,773
  Likes Received: 491
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mwesigwa Blandesi a.k.a Bernald Membe acha matusi hata kama una hasira kuna jinsi ya kujibu hoja.

  Tunakataa kwa kauli nzito jaribio la kutaka kutumia vitisho kukandamiza haki ya kidemokrasia ya kila binadamu kutoa maoni yake bila kujali cheo cha mtu, dini ,umri wala rangi. Maneno uliyotoa hapa ni mazito na ni matusi kwa wapenda amani na uhuru wa kujieleza. Ina maana hujaona akina Obama, Hujin Tao, Sarkozy n.k wakipingwa kwa mabango maeneo mbali mbali duniani wanakokwenda? Inaonyesha exposure yako ni finyu sana na una kiwango kikubwa cha upofu wa fikra na udikteta ndani yako kwani unataka watu wajibane hadi wafe wakati kuna majukwaa huru ya kupumulia kama anavyotaka kufanya Eliakim Mallya. Ninyi mnaoshindwa kuyatatua matatizo ya waTZ na kwenda nje kutafuta sifa mnatapatapa mnapoona aibu ya chumbani inatoka nje kwa majirani . Kilichowafanya msubiri waTZ wafikie hatua hiyo ni nini kama mlitaka muendelee kusifiwa na hawa wanaowapa ulaji. Mkuu vumilia upate hiyo sindano huko Marekani mtajifunza acha kutapa tapa humu na elewa siku hizi watu wanajua haki zao hata ukitumia maneno ya vitisho hayatasaidia na unachotakiwa kujua ni kwmba watu wamechoka na kama una ubavu kazuie hayo maandamano ya marekani. Kumbuka mficha uchi hazai na hivyo kama unaona watu kutoa maoni yao ni kulivunjia Taifa heshima basi wewe ndi mchawi tuliyekuwa tunakutafuta.
   
 14. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapa hakuna cha "taarifa za kiintelijensia" wala mabomu au maji ya kuwasha! JK, this time unalo, dunia nzima itatambua "who you real are!"
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 36,577
  Likes Received: 15,001
  Trophy Points: 280
  Kwani kaja mara ngapi huko ?
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,773
  Likes Received: 491
  Trophy Points: 180
  Kamundu hujui utendalo yawezekana na wewe umeahidiwa kacheo feki. sisi huku tunateseka na mafuta, mgao wa umeme na maisha magumu kwa sababu huyo rais unayemtetea ameshindwa kusimama katika nafasi yake na kukemea wale wanaokula na kudidimiza uchumi wa TZ. Unakuwa na proud gani kuwa na mtu kama huyo kwenye diaspora kama si kwamba una lako? Usitumie tena hii forum kueleza upuuzi kwani Tanzania na mwananchi wa kawaida ambaye hawezi kununua tena mafuta ya taa au sukari anafaidika na comments zako?. Ilitakiwa platform hiyo mjipange kumweleza hayo yote ila inaonyesha mmemkaribisha mje kumfungulia Champagne wakati huku watu wanateseka halafu unathubutu kusema asipokelewe kwa maandamano yenye ujumbe? You're crazy au uliondoka TZ miaka ya Nyerere na huwezi jua jinsi JK ameipeleka nchi ndivyo sivyo na hadi sasa anajishauri mwenyewe kwa sababu mzee haambiliki hawezi kuwa na washauri.
   
 17. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ama kweli majinga, wasaliti, waoga na maopportunists yako kila mahali.
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  JK akibadili venue afuatwe huko huko, ila angalieni asijedai kabadili venue kumbe amewalamba chenga ya mwili!
   
 19. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wewe gamba naomba uniambie kikwete kwanini atembelei mikoa kazikasin na kanda ya ziwa mpaka leo kama kweli alichaguliwa kialali haruta countinue mpaka angoke m kwerre...........k
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Kamende, fafanua, who ru talking about?
   
Loading...