Ndugu zangu wanachadema, ni ukweli usiyofichika kwa sasa, serikali iliyoko madarakani(C**) imepagawa, haijui nini ifanye na wapi ikimbilie, hakika imeshikwa pabaya, hali ni tete. Kwa kuwa hala hala mti na , na pia kifo cha nyani yawezekana akakurukia hata usoni
Nina angalizo kwa haya yafuatayo kwa siku chache zijazo
(i) Kama Tendwa (msajili wa vyama) atalazimishwa na bosi wake kukifuta chama cha CHADEMA kwa maslahi ya Taifa, je sisi wafuasi tufanyeje kwa hili
(ii) Kama viongozi wa CHADEMA watashitakiwa kwa kesi za uhaini, mimi na wewe tunafanyeje?
(iii) Mwisho kama vyombo vya habari vitaendelea kuchonganisha CHADEMA NA serikali hapa wewe unafanya nini?
Ndugu zangu msisahau kuwa tumewakamata nyeti zao ni vilio hivyo yakitokea haya tunafanya lipi? Toa ushauri kadiri utavyoweza.
Watu wenyewe hata mabomu mnaogopa, likipigwa moja watu wanakimbia wala hakuna hata mmoja anayesimama. Karibu sasa atasema basi na hapo ndipo mtakapo ona cha moto.
.
WANASIASA na taasisi mbalimbali nchini wamepinga maandamano yanayoendeshwa na Chadema kuhamasisha wananchi kuipinga Serikali na kuiondoa madarakani kuwa ni uhaini na inapaswa kushitakiwa.
Aidha, wamemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa, kuangalia uwezekano wa kukisimamisha au kukifuta chama hicho kwa usalama wa Taifa na kudai kuwa maandamano hayo ni chanzo cha vurugu na kuvunjika kwa amani, ambazo ni dalili zinazopaswa kuchukuliwa hatua za kiusalama haraka ili Taifa lisiingie katika machafuko ya kisiasa.