Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

Isaya, hoja zako si za kupuuza. Lakini mimi naamini CDM nao wamejipanga vizuri. Wana wasomi, wachambuzi na wanasheria mahiri sana. wanaona mbali. Hivyo, wamejipanga vizuri kukabiliana na kila changamoto iliyoko mbele yao. Lakini kubwa zaidi serikali inaona jinsi chama hiki kimefunika. Nao hawawezi kukurupuka. Hatua zozote dhidi ya CDM mara zote zimekuwa zikikinufaisha chama hiki. Kisiasa, hata wakifunguliwa kesi kwao utakuwa mtaji. Watacatch media na attention ya watu. Nafikiri unaona hata serikali hivi sasa, pamoja na vyama vingine, tena hivi sasa hata asasi nyingine, zimeshindwa kufikiri zimekamatwa na hoja za chadema. Hivyo, chama hiki kimefanikiwa sana kuongoza nchi. Huu ndio mtaji wa wanasiasa. Inavyoonekana ni kama nchi hii inaongozwa na CDM. Nakiri kweli gov. yetu imeshikwa pabaya. Ndiyo maana kila kiongoza anajitahidi kudandia hoja ya CDM tena walio wengi wanajitahidi kuipotosha.

CDM ni vema wawe makini. Mmekubalika sana. Lakini muwe makini zaidi. Of course binafsi navutiwa sana na viongozi wake walivyo serious.
 
Mwita,
CCM na serikali yake sasa hivi wamebanwa kila kona. Hao wanaowaita wahisani wao mpaka sasa hivi wamegoma kutoa pesa. Hatua yoyote ya kuikandamiza CDM itazidi kuiumiza serikali hivyo ondoa shaka. Hata hii mikutano na maandamano usifikiri CCM walipenda ifanyike, ni kwamba hawana namna ya kuizuia.
 
Nimeipenda ila kisheria watapaswa kuprove makosa ya cdm ndo wafuate hatua nyingine kitu ambacho hakipo!
 
mkuu .... nchi nzima imechanganyikiwa na hata huyo Tendwa kachanganyikiwa ... tunahitaji mabadiliko
 
Ni angalizo zuri kwa CDM, lakini ninawasiwasi na umakini wa viongozi wa CDM nasema hivi kwa sababu mikakati yao inaonekana maranyingi inafeli, kwa mfano Arusha maandamano yao hayakufanikwa kumuondoa meya madarakani. Walishauriwa wafungue kesi wakadai ni njia ndefu na maandamano ndio njia sahihi na kila mmoja wetu anajua matokeo yake. Kama tunadai chadema ina wasomi na wanasheria makini kwanini wasiwasaidie wanaharakati katika kesi ya dowans mahamani kama kweli wanataka deni lisilipwe au wanajua kisheria haiwezekani ila wanawahadaa wananchi ambao wengi hawana uelewa wa kisheria?
Tetesi nilizonazo ni kwamba baada ya mkutano wa CCM kuchagua watendaji wao wanajipanga kuboresha chama chao kuanzia mashina(balozi za nyumba kumi) na matawi nchi nzima kuwapa misaada ya hali na mali kuimarisha chama kwa uchaguzi wa 2015, je CDM wanafanya hayo au wanaandamana nchi nzima na kuwaacha wanachama na wapenzi wao waje kunasa katika mtego wa CCM? Ni ukweli usiopingika kwamba CCM bado wanamtandao mkubwa nchini ndio sababu walisimamisha wagombea kata zote na majimbo yote uchaguzi 2010 na si wajinga na wamelala kama wengi wetu tunavyoamini, msipojipanga vizuri 2015 mtabaki na maandamano na kulalamika kura zimeibiwa. TAFAKARI NA MCHUKUE HATUA.
 
Hivi hamjajua kama CHADEMA ipo upande wa wananchi na ccm ipo upande wa mafisadi?iweje mafisadi watishie wananchi?
 
aliyeshiba hamjui mwenye njaa,na daima ndivyo yalivyotekea duniani pote wakati wa mapinduzi viongozi walioshiba hutoa kauli za kejeli na vitisho lakini hatimaye umma hushinda...kama ilivyokuwa vigumu kuukamata upepo kwa viganja ndivyo ilivyokuwa vigumu kwa serikali dhalimu ya ccm kuushinda umma wa tanzania
 
Nimeshangaa ccm na wapiga debe wake wanavyokwepa kujibu hoja na badala yake wanazusha uongo usio na mashiko. Wakumbuke kuwa sasa hivi kila Mtanganyika 'anaona na kuelewa' hali halisi.
 
Waziri aitisha Chadema Send to a friend Thursday, 03 March 2011 20:54

13wasiraleo.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira

Na Waandishi WetuWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kisije kikailaumu serikali itakapokosa uvumilivu na kutumia nguvu ya dola dhidi yake.
Wassira alisema chama hicho kinapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali na kuandaa mpango wa kuiondoa kwa nguvu serikali iliyoko madarakani.
Wakati Wassira akisema hayo, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango naye amekishukia chama hicho akisema maandamano yake hayana nia ya kushinikiza Dowans isilipwe, bali kuhamasisha vurugu nchini.

Kauli hizo za viongozi hao wa CCM, zimekuja siku tatu tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaonya viongozi wa Chadema kwa kuandaa maandamano na kupandikiza mbegu mbaya za chuki dhidi ya serikali.

Rais Kikwete alisema hayo alipokuwa akilihutubia taifa katika hotuba ya mwisho wa mwezi Februari kupitia vyombo vya habari. Chadema kimekuwa kikifanya maandamano na mikutano ya hadhara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kupinga serikali kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans pamoja na kuzungumzia ugumu wa maisha.

Waziri Wassira, akizungumza katika kipindi maalumu kilichorushwa juzi usiku na Televisheni ya Taifa (TBC), alisema Chadema hakina haki ya kufikiria kuiondoa serikali madarakani.

"Hawawezi na hawana haki ya kufikiria kuiondoa serikali, hawana hiyo haki. Kikatiba hawawezi na kama itatokea itakuwa ni ukiukwaji wa katiba," alisema Wassira na kuongeza:

"Suala la kuiondoa serikali madarakani halipo na wakitaka mazungumzo, hilo halizungumziki... hatuna chuki na Chadema, lakini tunapingana nao wanapowashawishi watu wawaunge mkono katika yao. Hilo haliwezekani."

Akizungumzia kile Chadema inachosema inachokiita hali ngumu ya maisha, Wassira alisema: "Hali ngumu ya maisha inatokana na mtandao mrefu. Hivi sasa mafuta yako juu, pipa moja linafikia dola 150, sasa wanataka Rais Kikwete aende Uarabuni kusimamia kupanda bei za mafuta?"

"Mafuta ni kila kitu, sasa yakipanda si Tanzaia tu hata mataifa mengine ni hivyo. Hata ukienda China hivi sasa kuna mfumuko wa bei, ni wazi pia hata wanaotumia bidhaa za China, bei itakuwa juu kwa sababu dola imepanda."

Wassira alikishambulia Chadema akirejea kauli ya Rais Kikwete kuwa kinatumia vibaya nafasi na haki yao ya kuandamana kwa kueneza chuki kwa wananchi juu ya serikali yao.

"Dola ina mipaka yake ya kuvumilia. Uvumilivu ukizidi itatumika lakini kama wataendelea kupandikiza chuki, watawahadaa wananchi na kuwatia hofu, wananchi wanataka kuishi bila hofu...wakitaka tukae tuzungumze, bei zinapanda tufanye nini, huku tukidumisha amani."

"Hatuwezi kukaa kimya kuona eti kwa kuwa ni wapinzani wafanye wanavyotaka. Kuna mipaka yake, wakiendelea watakutana na mkono wa dola na wasije wakatulaumu."

Akinukuu vifungu vya Katiba, alisema: "Ibara ya 20 ya kifungu cha Katiba, inampa nafasi na haki kila mtu kukutana na yeyote na kutoa mawazo lakini, si kutumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa. "Huku (kutumia nguvu) ni kuvunja katiba na hatutakuwa wavumilivu katika hili."

Wassira amekishauri Chadema kutulia akieleza kuwa watu hawakihitaji sasa kwa kuwa si muda mrefu wananchi wamepiga kura na kila mmoja ameona matokeo.

"Tuliingia wote katika mapambano ya ubunge na urais, zilipigwa kura na wananchi hao hao ndiyo walioamua. Sasa hawa wameshindwa kwa njia ya demokrasia, wanataka kutumia nguvu, hiyo haikubaliki...haikubaliki."

"Sawa, leo wanasema wanaizungumzia Dowans, kwanza iko mahakamani, halafu watakuwa na kipi kipya? Kama huyo Slaa (Dk Willibrod, Katibu Mkuu wa Chadema) siku zote, kampeni zote ameimba Dowans, ufisadi kasema sana lakini watu wakampa kura Kikwete..."

"Tunachotaka ni amani na umoja. Hii ya kusema nguvu ya umma inatoka wapi? Kama nguvu ya umma basi iko CCM kwa sababu wamepiga kura watu milioni tano, CCM wakapata milioni tatu wao (Chadema) milioni mbili, sasa nguvu ya umma ni nani hapa?"

Kwa mujibu wa Waziri Wassira, Serikali haitazuia haki ya mtu au kikundi kuandamana lakini, haitavumilia wanaotumia vibaya fursa hiyo... "Ni wazi Chadema wanatuonyesha wao ni washari, wanawatia hofu wananchi, tunawaambia waache kufanya hivyo.

"Katiba iko wazi, kuna vikao halali vya kuwasilisha yao na zaidi ni Bunge, tena uzuri bungeni unasema unavyotaka ilimradi usivunje sheria, sasa kuwakusanya wananchi na kuwaeleza unayotaka ni kuvunja sheria. "Kuna Sheria ya Usalama wa Taifa, kutangaza kutaka kuiondoa serikali madarakani ni kuvunja Sheria ya Usalama wa Taifa, hapo dola haitavumilia," alisema Wassira.

Alisema wananchi wanataka kuishi kwa amani kwani hawajui vita... "Vita wanayoijua ni ile ya Kagera mwaka 1978 na ilipiganwa katika mkoa mmoja wa Kagera, labda haya mabomu ambayo yamelipuka katika kambi za jeshi kwa bahati mbaya. "Upinzani si vitisho, ni hoja, kama wana hoja wasubiri kikao cha Bunge la Bajeti Juni, waje na mawazo yao, waje na hoja za upinzani lakini si vitisho."

Kauli ya Kilango
Akizungumza na gazeti hili jana, Kilango alitaka chama hicho kisiendelee kupandikiza chuki kwa jamii akieleza hasara yake kuwa ni kuleta maafa na kuua taifa. Alisema inasikitisha kuona viongozi wa Chadema wanatoa kauli za kuhamasisha vurugu badala ya kushinikiza Dowans isilipwe kama ilivyodai awali.

Alisema kama kweli Chadema kinataka Dowans isilipwe, kingeongeza nguvu za wanasheria ili kuhakikisha kesi iliyofungunguliwa mahakamani na wanaharakati inafanikiwa na si kuzunguka nchi nzima kumtaka Rais ajiuzulu.

"Najua ndugu zangu wa Chadema hawataki kusemeshwa lakini, mimi kama kiongozi nimeona ni vyema niwaambie ukweli. Kauli kama kumtaka Rais ajiuzulu hazifanani na lengo la kushinikiza serikali isiilipe Dawans,"alisema.

Aliongeza "Nilikataa, ninakataa na nitakataa serikali ya CCM kuilipa Dowans na si wabunge wa CCM tu, ambao wanakataa hilo, bali hata wanaharakati wa haki za binadamu, lakini kwa nini tutake Rais ajiuzulu badala ya kukazania dai la msingi?"

Alisema Chadema wasifikiri kuwa wao tu ndiyo ambao hawataki Dowans isilipwe, bali huo pia ni msimamo wa wabunge wa CCM katika azimio lao walilolipitisha wakati walipofanya kikao Februari mwaka huu na mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete.

Kilango alisema kuwa ni muhimu Watanzania wakajiuliza kama kweli Chadema kuzunguka kwao ni kwa ajili ya kushinikiza serikali isiwalipe Dowans au la.

Kwa mujibu wa Kilango, kauli zinazotolewa na viongozi wa Chadema katika maandamano yao kama Kikwete ajiuzulu au iwe kama Misri na Tunisia, inaonyesha kuwa nia yao si Dowans isilipwe, bali malengo yao ni kutaka Rais ajiuzulu.

"Katika ulimwengu wa hekima na busara, binadamu yeyote yule angetazamia wote wanaopinga Dowans kulipwa wangeunganisha nguvu pamoja kuwasaidia wale ambao wamelichukua jambo hili kisheria na hasa tukijua wazi kwamba takriban Watanzania wote hawataki kodi zao zitumike kulipa Dowans," alisema Kilango.

Kilango aliitahadharisha serikali kutopenda kufanya vitu kwa dharura na badala yake iwe inachukua tahadhari katika kutatua matatizo ya kitaifa likiwamo suala hilo la umeme.

Ameishauri kutengeneza mabwawa makubwa yatakayosaidia kuhifadhi maji na kuondoa adha ya kupungua kwa maji katika mabwawa yanayotumika kuzalisha umeme nchini.

"Lazima serikali nayo iangalie hili kwani mfumo wa kuhifadhi maji ya akiba kama uliopo nchini Marekani kule Tenessee, ungeweza kusaidia kipindi kama hiki cha ukame," alisema.

Alisema gharama inayotumika kukodi mitambo ya dharura kila wakati tatizo linapotokea, zingeweza kutengeneza "Stigller's gauge" kuzalishia umeme na gharama yake ni dola za Marekani 400 milioni tu.

"Wasiwasi wangu ni kwamba fedha nyingi zinazotumika kwa dharura ambazo zingeweza kutengeneza "Stigller's gauge" ambayo iko sehemu za Chita katika Bonde la Kilombero,"alisema Kilango.

Mrema naye akerwa

Naye Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema ameonya kuwa kuiondoa serikali iliyoko madarakani bila kufuata njia za kikatiba kunaweza kuzalisha matatizo makubwa na kuliangamiza taifa.

Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) alikuwa akizungumzia hali ya kisiasa nchini hususan maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chadema.

Alisema licha ya kwamba hapingi maandamano hayo kwa kuwa yako kwa mujibu wa sheria, yakizidi yanaweza kuing'oa serikali iliyoko madarakani kama ilivyotokea Madagascar.

"Mimi siitetei CCM wala serikali ya Kikwete kwamba wasiondolewe madarakani kwa sababu wao hawana hatimiliki ya kutawala nchi hii, lakini njia za kikatiba zitumike kuwaondoa madarakani," alisema Mrema na kuongeza:

"Maandamano ya Chadema ni halali lakini, tukiwazoesha watu maandamano kila kukicha tutafikia mahali kama wenzetu wa Misri, Somalia, Libya na Madagascar."

Alisema ufisadi na matatizo mbalimbali yanayolikumba taifa sasa hayawezi kumalizwa kwa maandamano na kwamba njia za mkato zinaweza kuleta maafa makubwa nchini. Mrema alisema wapinzani wana kazi nyingi za kufanya ikiwamo matumizi ya fedha za umma katika halmashauri na Chadema wanatakiwa kubuni njia mbadala ya kufikisha ujumbe wao huo badala ya maandamano.

"Japokuwa mwaka 1995 niliandamana na kupigwa mabomu lakini, tunajifunza kwa sababu tunaona yanayotokea katika nchi nyingine," alisema.

Alisema serikali ikiondolewa kwa njia ya nguvu za umma ambayo ni maandamano, vurugu na mambo mengine, itasababisha katiba ya nchi kufa na kuifanya nchi isiwe na katiba.

Huku akionyesha vitabu vya takwimu za hesabu za serikali, Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa alisema, wapinzani wamepewa kazi nyingi badala ya kukimbilia kwenye maandamano na mikutano tu.

"Wapinzani tumepewa na Bunge kazi ya kupambana na ufisadi hivyo, tutumie fursa hizo tuwakamate, ufisadi hauwezi kuondolewa kwa maandamano," alisema.

Alisema kama serikali ikiondolewa madarakani kutakuwa na ombwe la uongozi na jeshi linaweza likachukua nchi wakiona inaingia kwenye migogoro.

Ataka Chadema wakamatwe
Katika hatua nyingine, Balozi wa amani wa taasisi ya Universal Peace Federation, Risasi Mwaulanga ametaka viongozi wa Chadema wakamatwe na kufunguliwa mashitaka ya uhaini kwa kile alichosema kuwa wanavuruga amani ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwaulanga alisema Chadema kinatumia fursa ya maandamano kumkashifu Rais Kikwete kitu ambacho ni uvunjifu wa amani.

"Hakika huu ni uhaini wa wazi ambao Chadema inaufanya, kwani umma unapokasirika na kupata hamasa mbaya, matokeo yake ni kuzigomea sera na kuwafanya wananchi kuacha kushiriki shughuli za maendeleo," alisema Mwaulanga na kuongeza:

"Mwenyekiti wa Chadema na Katibu wake Mkuu wanapaswa kukamatwa, kufunguliwa mashtaka ya uhaini. Bunge linapaswa pia kutoa onyo kali kwa wabunge. Hali kadhalika, Msajili wa Vyama vya Siasa aangalie vifungu vya Katiba yake kuona uwezekano wa kukisimamisha au kukifuta chama hicho kwa usalama wa Taifa."

"Vyama vya siasa vina haki ya kuandamana, ila ikitumiwa vibaya itavuruga amani. Kwa mfano, Chadema wanatumia maandamano kumpinga Rais Kikwete, huu ni uhaini kabisa."

Mwaulanga pia alitumia nafasi hiyo kumpiga vijembe bila kumtaja jina Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa akidai kuwa amekuwa akitumia vyombo vya habari na majukwaa ya kidini kuikosoa CCM huku akitolea mfano kauli yake ya hivi karibuni kutaka mishahara ya watumishi wa umma ipande.

"Sasa mtu unataka wafanyakazi waongezwe mishahara, Rais atazitoa wapi fedha hizo?" alisema Mwaulanga.

Kwa mujibu wa Mwaulanga, kutumia majukwaa ya dini kupinga mipango au upungufu wa Chama na serikali kwa viongozi wa siasa si sahihi hata kidogo.

"Wanapokaribishwa na viongozi wa dini wanachopaswa kufanya ni kupinga mipango mibaya ya shetani kwa binadamu kumuasi Mwenyezi Mungu na siyo kuiponda serikali" alisema.

Habari hii imeandikwa na Ibrahim Bakari, Boniface Meena,Nora Damian na Elias Msuya


 
Pinda aenda 'kufuta nyayo' za Dk Slaa Send to a friend Thursday, 03 March 2011 20:58

pindakilimokwanza.jpg
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Mwandishi Wetu
KATIKA kile kinachoonekana kama mpango wa Serikali kukabiliana na nguvu za maandamano na mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku nane katika Mkoa wa Kagera ambako atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kutembelea wilaya zote za mkoa huo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Waziri Mkuu ataanzia ziara yake katika Manispaa ya Bukoba kisha atakwenda Muleba, Chato, Biharamulo, Ngara, Karagwe, Missenyi na kumalizia Bukoba Vijijini.

Katika ziara yake ya Kanda ya Ziwa, Chadema kilitembelea na kufanya mikutano katika Wilaya za Biharamulo, Misenyi, Muleba na Chato ambako viongozi wake walifanya mikutano na maandamano huku wakitaka Kampuni ya kufua umeme ya Dowans isilipwe, bei ya umeme ishuke na kikitaka utawala wa CCM uwajibike.

Baadhi ya shughuli kubwa ambazo Waziri Mkuu amepangiwa kufanya wakati wa ziara hiyo ni pamoja na kuzindua Barabara ya Zamzam na mkutano wa hadhara kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba katika Uwanja wa Mayunga (Uhuru Platform).

Akiwa wilayani Muleba, Waziri Mkuu Pinda atakagua shamba la mkulima bora wa kahawa katika Kijiji cha Ilogero kabla ya kwenda Buganguzi ambako atakagua mashamba ya migomba yaliyoshambuliwa na magonjwa ambayo mpaka sasa hayajajulikana kisayansi.

Pia ataweka jiwe la msingi katika mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Buyaga na kuhutubia wananchi katika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Kasharunga.

Akiwa wilayani Chato, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kufungua Saccos ya Mshikamano kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Shule ya Msingi Chato.

Akiwa Biharamulo, Waziri Mkuu atakagua mnada wa ng'ombe wa Lusahunga, kukagua ujenzi wa wodi katika hospitali hiyo na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya St Clara huko Rukaragata na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Michezo wa CCM.

Akiwa Biharamulo, Jumanne ijayo Waziri Mkuu atakwenda Ngara kufungua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Ngara Farmers kabla ya kwenda kwenye Mgodi wa Nickel wa Kabanga. Pia atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara huko Muurusagamba.

Akiwa Karagwe, Jumatano ijayo atakagua bwawa la samaki huko Kishoju na kusalimiana na wananchi kisha atakwenda Kayanga kuzindua jengo la masjala ya ardhi. Mchana ataweka jiwe la msingi katika Chuo cha Ualimu Katera kabla ya kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Isingiro.

Akiwa Missenyi, Alhamisi ijayo, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo. Baadaye ataelekea Kiwanda cha Sukari cha Kagera kuona mitambo ya kisasa ya umwagiliaji mashamba ya miwa. Pia atakagua shughuli za kiwanda hicho na kisha kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa Mashujaa wa Bunazi.

Akiwa Bukoba Vijijini, Ijumaa, Waziri Mkuu atatembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku, maabara na baadhi ya vijishamba vya utafiti wa kilimo. Pia atakwenda Hospitali ya Izimbya kuzindua majengo ya OPD, watoto, maabara, chumba cha upasuaji na jengo la ushauri na upimaji VVU (CTC).

Jumamosi ijayo, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu Mkoa na kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo.
 
Pinda aanza ziara Kagera leo


Na Mwandishi Maalumu

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo anaanza ziara ya siku nane kwenye mkoa wa Kagera ambako atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kutembelea
wilaya zote za mkoa huo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Waziri Mkuu ataanzia Manispaa ya Bukoba, ataenda Muleba, Chato, Biharamulo, Ngara, Karagwe, Missenyi na kumalizia Bukoba Vijijini.

Baadhi ya shughuli ambazo Waziri Mkuu amepangiwa kufanya wakati wa ziara hiyo ni pamoja na kuzindua barabara ya Zamzam na mkutano wa hadhara kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba katika uwanja wa Mayunga (Uhuru Platform).

Akiwa wilayani Muleba, Waziri Mkuu Pinda atakagua shamba la mkulima bora wa kahawa katika Kijiji cha Ilogero kabla ya kwenda Buganguzi ambako atakagua mashamba ya migomba ambayo yameshambuliwa na magonjwa ambayo mpaka sasa hayajajulikana kisayansi. Pia ataweka jiwe la msingi katika mradi wa umwagiliaji wa Kijiji cha Buyaga na kuhutubia wananchi katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Kasharunga.

Akiwa wilayani Chato Jumapili, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kufungua SACCOS ya Mshikamano kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Shule ya Msingi ya Chato.

Jumatatu Bw. Pinda atakagua mnada wa ng’ombe wa Lusahunga, wilayani Biharamulo, kukagua ujenzi wa wodi katika hospitali hiyo na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Clara huko Rukaragata na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa CCM.

Wilayani Ngara Jumanne ijayo, Bw. Pinda atafungua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Ngara Farmers kabla ya kwenda kwenye mgodi wa Nickel wa Kabanga. Pia atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara huko Muurusagamba.

Waziri Mkuu pia atatembelea Karagwe Jumatano ambako atakagua bwawa la samaki huko Kishoju na kusalimiana na wananchi kisha kwenda Kayanga kuzindua jengo la masjala ya ardhi. Mchana ataweka jiwe la msingi katika Chuo cha Ualimu cha Katera kabla ya kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Isingiro.

Akiwa Missenyi, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo. Baadaye ataelekea Kiwanda cha Sukari cha Kagera kuona mitambo ya kisasa ya umwagiliaji mashamba ya miwa. Pia atakagua shughuli za kiwanda hicho na kisha kuzungumza na wananchi katika uwanja wa Mashujaa wa Bunazi.

Akiwa Bukoba Vijijini, Waziri Mkuu ataenda Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kutembelea maabara na baadhi ya vijishamba vya utafiti wa kilimo. Pia atakwenda Izimbya kuzindua majengo ya OPD, ya watoto, maabara, chumba cha upasuaji na jengo la ushauri nasaha na upimaji VVU (CTC).

Jumamosi ijayo, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu Mkoa kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo.




1 Maoni:

blank.gif

JOJAS BRAND said... Mh.Pinda nimefurahi sana kusikia unakwenda mkoani kagera.Ninaomba utakapofika Wilayani Ngara ninaomba uunde tume au ufanye uchunguzi kuhusu mwenyekiti wa kijiji na serikali wanakula Rushwa wanataifisha mashamba ya wananchi wanawapa watu wenye fedha(Matajiri)Suala Mh.Dc analijua analifumbia macho.
March 3, 2011 10:50 PM
 
Migodi kuguswa balaa la umeme


*Kamati ya Bunge yataka ipunguziwe matumizi
*Yadai wanatumia umeme kibao, hawana mgawo


Na Mwandishi Wetu

WAKATI suluhisho la mgawo wa umeme nchini halijapatikana huku suala la ama kuwasha au kutowasha mitambo ya Dowans likisumbua
vichwa vya Watanzania, imefahamika kuwa Kamati ya Bunge ya Bunge ya Nishati na Madini imependekeza yafanyika mazungumzo na migodi ya madini ili kuona kama inaweza kupunguza matumizi ya nishati hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Januari Makamba alisema jana kuwa migodi hiyo imekuwa ikitumia umeme mkubwa unaofikia megawati 125 kila mmoja, lakini haikuwahi kukumbwa na mgawo wa umeme, jambo ambalo wamesema likikubaliwa sehemu ya nishati hiyo inaweza kusambazwa kupunguza makali katika maeneo mengine.

"Migodi inatumia umeme mwingi sana na haikatiwi hata siku moja, kila mgodi unatumia megawati 125 kwa siku kwa migodi minne ni umeme mwingi sana, tumeshauri kuwepo kwa mazungumzo ya kupunguza matumizi ya umeme kwenye migodi kwa kipindi hiki," alisema Bw. Makamba.

Hilo ni moja ya mapendekezo makubwa manne ya upatikanaji wa umeme haraka ili kupunguza makali yaliyotolewa na kamati hiyo, likiwamo la kuwasha mitambo ya Dowans, ambalo hata hivyo linaweza kuathiriwa na kesi iliyopo mahakamani.

Akizungumzia suala hilo, Bw. Makamba alisema hakuna mahakama iliyozuia utekelezaji wa mapendekezo yao kuhusu hatua za dharura kunusuru nchi na janga la ukosefu wa umeme kama ilivyodaiwa bali kilichozungumzwa ni kwamba serikali itatakiwa kutoa taarifa yoyote iwapo kuna hatua za mazungumzo juu ya matumizi ya mitambo ya Dowans au suala lolote nje ya chombo hicho.

"Tuliwauliza mawakili wa TANESCO kilichosemwa na jaji ni kuwa kama kuna mazungumzo nje ya mahakama basi taarifa itolewe ili mahakama isimamishe kwanza shauri, haijazuia mapendekezo yetu jamani," alisema Bw. Makamba.

"Lakini pia hata kama tungeachana na hilo la mitambo ya Dowans bado kuna mapendekezo mengine matatu ambayo ni muhimu sana kufanyiwa kazi na serikali," alisema Bw. Makamba.

Pendekezo jingine ni pamoja na serikali kuwashwa mitambo ya IPTL yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 kwa siku ambayo kwa sasa inazalisha megawati 10 tu.

Pia waliishauri TANESCO ifanye marekebisho kwenye transfoma zake, umeme unaopotea kwa siku ni sawa na asilimia 75 ya umeme wote unaozalishwa na Songas kwa mwaka mzima ili kuokoa kiasi hicho.
 
Ukweli hali ilipofikia sasa ni taharuki. Sijajua mwisho wake ni nini? Lakini ngoja tuone!
 
Nimeshangaa ccm na wapiga debe wake wanavyokwepa kujibu hoja na badala yake wanazusha uongo usio na mashiko. Wakumbuke kuwa sasa hivi kila Mtanganyika 'anaona na kuelewa' hali halisi.

Badala ya kutumia muda kutafuta majibu ya changamoto zetu wanapoteza fursa kwa kuanza kupambana na Chadema huku umasikini ukiendelea kututafuna. Wakimshikilia Slaa wataibuka akina Mtikila ambao wako aggressive zaidi kuliko hata Slaa ambaye anatumia demokrasia zaidi
 
Hawa Wazee nadhani hawajui nguvu ya umma ilivyo sasa naona wanatuchokoza, waache tuu kama wanataka kustaafia nje ya nchi hii waache walete ujinga wao
 
Mwita,
CCM na serikali yake sasa hivi wamebanwa kila kona. Hao wanaowaita wahisani wao mpaka sasa hivi wamegoma kutoa pesa. Hatua yoyote ya kuikandamiza CDM itazidi kuiumiza serikali hivyo ondoa shaka. Hata hii mikutano na maandamano usifikiri CCM walipenda ifanyike, ni kwamba hawana namna ya kuizuia.

Gagnija unajua hakuna kitu kibaya kana kubanwa na haja kubwa (tumbo la kuhara) lolote laweza kukupata, maamuzi unayoweza kuyachukuwa kwa kipindi kile cha haja kubwa na choo haionekani mbaya zaidi iwe safarini.

Gagnija Tazama kipindi hiki ni kipindi kigumu sana kuliko kipindi chochote kile hawa C** wanachopitia, wasiwasi wangu isije ikawa kwamba maamuzi wanayoweza kuyachukua ili kupambana na hali hii ikawa ni pamoja na kumlazimisha Tendwa kukifuta chama cha Chadema.

Gagnija niliuliza swali hebu ikitokea hivyo sisi watz wa kawaida tunafanya nini kwa hili?

Gagnija naomba usisahau kuwa Uongozi wote wa C** wote ni JWT Kuanzia huyo Rais Katibu wake(Makamba) wakuu wa Mikoa.... na hata wakuu wa wilaya.

Kwa hili tunafanya nini ndugu zangu?
 
usijali mkuu, nguvu ya umma ni zaidi ya TENDWA na JWTZ pia kumbuka hata wajeshi wa kawaida hawapendi hizi richmonduli a.k.a DOWANS
 
71586_134425709941239_100001214312304_190645_7230553_n.jpg
36148_138841592832984_100001214312304_214761_3838170_n.jpg
Samuel Kanyon Doe (May 6, 1951 – September 9, 1990) was the 21st President of Liberia, serving from 1986 until his assassination in 1990. He had previously served as Chairman of the People's Redemption Council from 1980 to 1986. He was the ...first indigenous head of state in Liberian history.

Doe was an ethnic Krahn, part of a rural tribe in inland Liberia. The Krahn are a minority ethnic group but part of the large majority of the Liberian population that are of indigenous descent. These groups faced economic and political domination by the Americo-Liberian elites, who were descended from free-born and formerly enslaved blacks from America who founded Liberia in 1847.

Under Doe, Liberian ports were opened to Canadian, Chinese and European ships, which brought in considerable foreign investment from foreign shipping firms and earned Liberia a reputation as a tax haven.

Doe attempted to legitimize his regime with a new constitution in 1984 and elections in 1985. However, opposition to his rule only increased, especially after the 1985 elections which were declared to be fraudulent by the U.S. and other foreign observers. In the late 1980s, as fiscal austerity took hold in the United States and the threat of Communism declined with the waning of the Cold War, the U.S. became disenchanted with entrenched corruption in Doe's government and began cutting off critical foreign aid to Doe. This, combined with the popular anger generated by Doe's favoritism toward his native Krahn tribe, placed him in a very precarious position.

A civil war began in December 1989, when rebels intent on toppling Doe entered Liberia. Doe's forces were defeated, and in September 1990 he was captured, tortured, and killed.
Cont
1980 coup, new government

On April 12, 1980, Doe led a military coup, killing President William R. Tolbert, Jr. in the Executive Mansion. Many claim that Doe and some of his men disemboweled President Tolbert in his bed while he slept. Twenty-six of Tolbert's supporters were also killed in the fighting. Thirteen members of the Cabinet were publicly executed ten days later. Hundreds of government workers fled the country, while others were imprisoned.

The early days of the regime were marked by mass executions of members of Tolbert's deposed government. One of Doe's first acts after seizing power was to order the release of about 50 leaders of the opposition Progressive People's Party who had been jailed by Tolbert during the rice riots of the previous month. Shortly after that, Doe ordered the arrest of 91 officials of the Tolbert regime. Within days, eleven former members of Tolbert's cabinet, including Tolbert's brother Frank, were brought to trial to answer charges of "high treason, rampant corruption and gross violation of human rights."[1] Suspension of the Constitution allowed these trials to be conducted by a Commission appointed by the state's new military leadership, with defendants being refused both legal representation and trial by jury.

The spectacle was videotaped and seen on news reports around the world. The video shows Johnson sipping a Budweiser as Doe's ear is cut.
47895_122130397837437_100001214312304_133234_6440564_n.jpg
hayupo wakuzuia mabadiliko nchini tanzania kwasasa na chaguo la wanyonge ni Dr .W.P. slaa CHADEMA OYEEEEEEEEE...Usually
when people are sad they don't do anything they just CRY over their
condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X).

 
huyu nae na sura yake kama ya mamba asitishe watu, tumevizoea vitisho vyao, limewashika.
 
yap,uko sawa kabisa .waswahili wanasema ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni,na penye nia pana njia.cmd sio vilaza kama CCM.



Isaya, hoja zako si za kupuuza. Lakini mimi naamini CDM nao wamejipanga vizuri. Wana wasomi, wachambuzi na wanasheria mahiri sana. wanaona mbali. Hivyo, wamejipanga vizuri kukabiliana na kila changamoto iliyoko mbele yao. Lakini kubwa zaidi serikali inaona jinsi chama hiki kimefunika. Nao hawawezi kukurupuka. Hatua zozote dhidi ya CDM mara zote zimekuwa zikikinufaisha chama hiki. Kisiasa, hata wakifunguliwa kesi kwao utakuwa mtaji. Watacatch media na attention ya watu. Nafikiri unaona hata serikali hivi sasa, pamoja na vyama vingine, tena hivi sasa hata asasi nyingine, zimeshindwa kufikiri zimekamatwa na hoja za chadema. Hivyo, chama hiki kimefanikiwa sana kuongoza nchi. Huu ndio mtaji wa wanasiasa. Inavyoonekana ni kama nchi hii inaongozwa na CDM. Nakiri kweli gov. yetu imeshikwa pabaya. Ndiyo maana kila kiongoza anajitahidi kudandia hoja ya CDM tena walio wengi wanajitahidi kuipotosha.

CDM ni vema wawe makini. Mmekubalika sana. Lakini muwe makini zaidi. Of course binafsi navutiwa sana na viongozi wake walivyo serious.
 
Back
Top Bottom