Kwa hiyo maandamano ndio yataleta hospitali?
Vyama vinavyojifanya kujali kwa nini visihamasishe foundations zitakazofanya miradi ya maendeleo kwa mfano?
Maandamano feki ni unafiki tu!
Walisema lazima dowans ilipwe wathubutu waone
mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.
Huyu ze marcopolo katumwa ye haoni hata umeme umeshashushwa kisa serikali kusikia mandamano ya chadema
Zemarcopolo mjinga
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.
Cha msingi sio kujua theme bali ni kujiuliza jamii itanufaika vipi na maandamano hayo na je, jitihada zinazotumika kuandaa maandamano zisingeweza kutumika kuleta manufaa zaidi? Hawa wote wanafiki tu!
You have raised important points but the truth remains and that is change require force - in science or sociology.Maandamano kama yanafanyika kwa dhamira njema kwa nia ya kuelezea hisia fulani halali na kwa kuzingatia sheria hayana matatizo. Tatizo litakuja kama baadhi ya wanasiasa wasomi watavuta hisia za watu kutumia kauli mbiyu fulani kutekeleza fikra iliyojiificha. Kwa hili wananchi tunatakiwa kuwa makini. Tusiandamane kwa sababu ya kufanikisha matakwa binafsi ya kisiasa ya watu au kundi la watu fulani na wala tusizuiwe kuandamana kwaajili ya kulinda maslahi ya watu au kundi la watu fulani.
Kabla hatujakubari wala kukataa kushiriki maandamano tunatakiwa kutafakari juu ya uhalali wa dhamira ya maandamano hayo na umhimu wake. Vipindi ambavyo kuna matatizo fulani ya kiuchumi huwa ni hatari sana katika usalama wa nchi. Wakati mwingine wacheza siasa hutumia matatizo hayo kujipatia umaarufu wa haraka na hatimaye kutwaa mamlaka ya kisiasa kwa haraka. Hali kama hii ya kutwaa nguvu za kisiasa kutokana na panic ya wananchi ya kimaisha mara nyingine huweza kuzaa dola ya kidikiteta na hatimaye ikawa ngumu kuin'goa. Utakumbuka kwamba madikiteta kama Mussolin na Hitla walapata umaarufu na hatimaye kutwaa madaraka ya ghafula katika vipindi vya matatizo ya kiuchumi ambapo watu walikuwa na panic ya kimaisha. Watu waliona kila anachokisema Hitla ni muarubaini wa matatizo ya kiuchumi. Matokeo yake alijizolea upendo kwa watu na kutwaa nchi kwa vigelegele. Baadaye wananchi walijikuta wakijuta.
Sina wasiwasi sana na wanasiasa mbalimbali tulio nao. Lakini binaadamu hubadilika kutokana na mazingira. Ni bora wananchi tukawa macho kuangalia kila upande na kuchukua tahadhari zote. Kila kinachosemwa tukiangalie katika pande zake mbili. Mtu kwa macho yako unaweza kuona matatizo mawili lakini kutokana na umahili wa kalamu au mdomo wa mwanasiasa unaweza matatizo mawili ukayaona milioni. Mtu unaweza kujisikia unaumwa kichwa kidogo lakini kutokana na umahili wa uzungumzaji wa mwanasiasa ukajihisi huwezi hata kupumua bila msaada wa mashine.
Dada Regia, mimi mwanachama wa chadema. Lakini naanza kupata mashaka na agenda mliyonayo viongozi wetu hii ya kuandamana. Siogopi maandamano ila sidhani kama ni muda muafaka. Tumieni njia mbadala kuimarisha chama na sio hii inaleta mtazamo hasi na kukitenga chama na kundi flani kubwa la watu ambao kwa kiasi kikubwa kwa kutokuamini upinzani unaweza kufanya kile unachoahidi, waliipa kura ccm mwaka jana na kuirudisha madarakani japo wameshaichoka sana. Lazima tukubali ukweli, ccm bado inakubalika sana. Unaweza kuona Bungeni walivyofunika, ok hata ukisema walituibia viti 20 vya ubunge bado upinzani hauna nguvu. Maandamano na migomo haiwezi kuwang'oa kwa sababu ni wachache ndio wataunga mkono. Tena leo CCM wakiamka wakafunga mjadala wa Dowans, wakawafikisha mafisadi kadhaa kizimbani(kama ilivyofanya kwa kina Mramba), upinzani wote utanyong'onye. Hebu tutafute sera za kudumu tuachane na vivuli vya matukio ya mpito. Kwa hiyo staili yenu, mnapunguza kasi ya ukombozi wa Taifa hili. Muda wa maandamano sio sasa, msirubuniwe na wachache wanaowazunguka ambao ni waelewa, wasomi na walio karibu na vyombo vya habari. Watanzania wengi hawako pamoja na nyie hata kidogo. Na siku CCM ikiamua kutusambaratisha litakua ni pigo takatifu na hatutasimama tena. Mwambie Dk Slaa, ths will never work out!!