Maandamano ya CCM nchi Nzima yaja

alikusudia CCM. hawana moral authority si kwa hili tu hata mambo yote katika nchi hii...labda kula ufisadi. wakifanya, wafanye kama CDM, no kubeba watu kwa mafuso kutoka wilaya jirani au kushurutisha watu kufunga biashara zao au kushurutisha walimu na wanafunzi waandamane wale kulazimisha magari ya serikali kutumika.
 
mwenyekiti yupi wa kuanza kuzunguka kufany amikutano??huyu si ana ugonjwa wa kuanguka anguka jukwaani huyu....miguu inakosa stamina sasa ataweza mikiki ya mikutano this time around ?
 
watazunguka kujibu nini wakati hawana majibu yeyote??
watapatia wapi nguvu ya kuzunguka wakati walishachoka??
hivi ni nini watakachokiongea na watu kuwasikliza??
 
Sitashangaa nikisikia wamefanya hivyo! Sababu hawana jipya, hawana ubunifu, kazi yao kuwaiga tu wengine.
 
Kwa kuwa CDM wanatumia haki yao ya kikatiba kuzunguka nchi nzima kutangaza sera zao na msingi wao juu ya hali mbaya ya umeme, ugumu wa maisha na kadhalika haina budi kwa CCCM na wao kuzunguka nchi nzima kutumia majukwaa na maandamano kujibu hoja na tuhuma za CDM na kuwaeleza wananchi wanampango gani katika kutatua kero zao, na kwa kuanzia waende kanda ya ziwa kufuta nyayo za CDM na wafanye hivyo hivyo kwa mikoa mingine ambayo CDM watafanya maandamano na mikutano ya hadhara.

Lakini angalizo langu ni jee, nani katika CCCM mwenye mvuto na anayekubalika na watanzania ambaye atazunguka Tanzania nzima kujibu tuhuma na hoja za CDM, je CCCM watapata mahudhurio makubwa kama wanayopata CDM na je mwitikio wa maandamano na mikutano ya hadhara ukiwa mbaya hii itatufundisha nini?

Je mwenyekiti na katibu wa CCCM wako tayari kuchukua jukumu hili na kuzunguka Tanzania nzima kujibu hoja za CDM kwa wananchi.

Nawakilisha.
hiki chama kiitwacho CCCM kimesajiliwa na Tendwa au ni saccoss hii
 
Nivigumu kwa CCCM kuandamana. Na hata kama wakitaka kufanya hivyo hawawezi kupata umati wa watu wengi kama CDM. Shida yangu ni mikakati yao ya kibabe. Hata kama CDM ni wengi wataendelea kutapeliwa mpaka mikakati madhubuti iwepo ya kukabili ujanja wa CC(C)M. Can you imagine matokeo ya uchaguzi yanatangazwa kinyume na kwa ubabe wakijua sheria haziwezi kuwabana na zaidi wakijua gharama kubwa za uendeshaji wa kesi za uchaguzi.

Can u imagine, vyombo vya habari havitoi taharifa stahili ya maandamano/mikutano ya CDM! Na bado only fun events kwenye mikutano hiyo ndo unasikia wakitangaza.
 
''Ndugu Zangu;

Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang'atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo. Hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa. Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.''


  • Nyerere miaka 23 chini ya TANU/CCM hakumaliza matatizo ya Watanzania.
  • Mwinyi miaka 10 chini ya CCM hakumaliza matatizo ya Watanzania.
  • Mkapa miaka 10 chini ya CCM hakumaliza matatizo ya Watanzania,
  • Kiwete miaka 5+ chini ya CCM hajayamaliza na hatayamaliza matatizo ya Watanzania kwa kukiri mwenyewe.
Maneno haya yanaonyesha kuwa chama cha CCM tangu kikiwa TANU kimekiri kuwa KIMESHINDWA KUMALIZA MATATIZO YA WATANZANIA. Maneno haya yamezungumzwa toka moyoni na Mwenyekiti wa chama CCM wa Taifa na Rais wa serikali ya CCM iliyoko madarakani Bwana JK. Hapa siyo siri KIKWETE NA CCM YAKE WAMEJIMALIZA!!!!

Hiki ni kithibitisho tosha kabisa kuwa CCM wameshindwa KABISA KUMALIZA MATATIZO YA WATANZANIA. MWENYEKITI WAO NA RAIS WAO AMEKIRI KWA KINYWA CHAKE KUWA NCHI IMEWASHINDA!!!!

Sasa basi kama nchi imewashinda wanang'ang'ania nini kukaa IKULU??Kwanini wanalalamikia CHADEMA ambacho kimekuja na sera mbadala za kuwakomboa Watanzania?

Kwa lugha rahisi ni kwamba CHADEMA wapo tayari KUYAMALIZA MATATIZO YA WATANZANIA. Siyo kwa siku 9 alizopewa Kiwete. Kiwete ni mzito wa kuelewa mambo. Hizi siku amepewa ili atoe maamuzi, mwelekeo na mstakabali wa Serikali yake katika kutatua matatizo ya Watanzania yanayowakabili kwa sasa.

Mifano iko mingi ya JK kutoa matamko/maamuzi katika siku 9 ili kutoa mwelekeo kwa Seikali yake namna ya kukabiliana na adha zinazowakabili Watanzania kwa sasa. Kwa mfano kuna tatizo kama la umeme wa DOWANS,IPTL,SONGAS; kama Rais anatakiwa atoe maamuzi magumu ikiwezekana hata kuwafukuza kazi Mawaziri na Makatibu wakuu waliotuingiza kwenye janga hili la UMEME WA KIFISADI unaoitwa wa DHARURA miaka nenda rudi.Haiwezekani nchi iendeshwe kwa umeme wa dharura kila siku!!

Kuna mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto. Watu wamekufa kwa mabomu. Kikwete anasikia Watanzania wanalalamikia UTENDAJI MBOVU wa Waziri wa Ulinzi-Dk. Mwinyi na Mkuu wa Majeshi-Mwamnyange. Kwanini hajawafukuza???Je,hili nalo linahitaji miaka mingapi kulitatua??

Kuna hili la sasa kuwa hali ya Uchumi ni MBAYA kiasi kwamba wafanyakazi wa serikali HAWAJAPATA MISHAHARA yao ya Februari. Hazina kumekauka hakuna pesa.Mamlaka ya mapato-TRA wameshindwa kukusanya kodi kwasababu watu hawafanyi Biashara kwa kukosa UMEME! Lakini wakati huohuo WABUNGE wetu wamegawana milioni 90 kila mmoja za kujinunulia magari sawa na Shilingi 32.4 Bilioni kwa wabunge wote. Kwanini Kiwete asiagize hiyo pesa ya Wabunge wasipewe na badala yake serikali iagize magari ambayo si MASHANGINGI kwa bei poa toka China au India ili pesa ingine itumike kulipia MISHAHARA NA MAMBO MENGINE muhimu???

Hakika CCM wameshindwa kuongoza nchi. Ni aibu kwa Rais mzima kuhutubia Wananchi kwa kuzungumza UMBEYA wa vijiweni eti CHADEMA wanataka kupindua nchi kwa maandamano badala ya kuzungumzia MATATIZO YA WANANCHI NA NAMNA YA KUYATATUA. Hakika JK ni Rais bomu wa karne hii!!

Kweli kufa kwa nyani miti yote inateleza. CCM kwa sasa ni nyani anayekabiliwa na kifo tena cha ghafla. Hakuna hata mti mmoja utakaomwokoa CCM.
Kwisha kazi!!!


 
lol,nadhani tutarajie anguko takatifu la kiwete kwani am sure hatomaliza miaka mitano ,atacheza kiduku,mduara,taarabu ,mdumange lakini for sure ngoma ya cdm hatoiweza,r.i.p mr mkwere
 
Asipoanguka yeye Mkwere basi CCM itaanguka soon. Naskia jamaa kwa sasa hawana hata ubavu wa kufanya mikutano au maandamano kwa kuhofia hasira za wananchi huenda wakapigwa mawe, huoni hapo chama kimeanguka hicho.
 
CCCM bila shaka chama kipya hiki ila sijawahi kisikia, wanaanza lini waandamano? Na viongozi wake ni akina nani?

viongoz wake ni waimba taarab maaruf hapa nchni. Wa kwanza ni yusuph makamba, wa pil ni tambwe hiza. n.k.. Umenisoma mkuu?
 
Unajua, dalili za mgonjwa kukaribia kukata roho ni kutapatapa sana, na huwa hakubali dawa. Dalili hizi na zingine ziko wazi kwa ccm kwa sasa.
 
amaejihami kukiri wazi kabisa kuwa hatafanya mabadiriko yeyote hata hapo baaadaye,kwa hiyo tutegemee tu BIG NOTHING .
Hata ahadi zake zote hazitekelezeki
 
Mkwere alikuwa anajaribu kujitetea na kuueleza umma kuwa zile ahadi alizitoa hazitekelezeki... Ilikuwa ni danganya toto tu ya uchaguzi!!!
 
hiyo statement hata mi niliisikia.....hivi waandishi wa hizi speech anawachagua mwenyewe au? mbona UD kuna maprofesa....wanahusishwaga kweli kwenye kutoa mawazo kwa mheshimiwa? au labda kaandika mwenyewe?

yaani ninajiuliza maswali mengi sana.
 
Kuna tetesi kuwa chama cha mapinduzi kitaitisha maandamano makubwa nchi nzima mara baada ya kikao cha halmashauri kuu baadaye mwezi huu. Maandamano hayo yataanzia Singida Mjini, halafu Dodoma, Morogoro, Tabora, Lindi, Mtwara na kuishia Temeke Dar. Lengo ni kupima kama athari za vuguvugu la CDM limefika hadi katika mikoa hii ambayo ni ngome yake ya miaka mingi. Hakutakuwa na kuwabeba watu kwenye malori isipokuwa watu watahamasishwa tu kuhudhuria. Hata wanamuziki wa bongo fleva hawataalikwa.

Source: Ofisi ya katibu mkuu CCM makao makuu.
 
CCM ni wapuuzi sana... Yaani wao tabu na shida hawazioni, wanakerwa na CDM!!!!
 
Kuna tetesi kuwa chama cha mapinduzi kitaitisha maandamano makubwa nchi nzima mara baada ya kikao cha halmashauri kuu baadaye mwezi huu. Maandamano hayo yataanzia Singida Mjini, halafu Dodoma, Morogoro, Tabora, Lindi, Mtwara na kuishia Temeke Dar. Lengo ni kupima kama athari za vuguvugu la CDM limefika hadi katika mikoa hii ambayo ni ngome yake ya miaka mingi. Hakutakuwa na kuwabeba watu kwenye malori isipokuwa watu watahamasishwa tu kuhudhuria. Hata wanamuziki wa bongo fleva hawataalikwa.

Source: Ofisi ya katibu mkuu CCM makao makuu.


Ninavyo ijua CCM haiwezi fanya mambo ya kijinga kama hayo ya kuandamana! Ni upuuzi mtupu!
 
Back
Top Bottom