Maandamano ya CCM nchi Nzima yaja

Maandamano ya CCM nchi Nzima yaja

Labda wenye chama waujibu uzi huu kwani umekaa kiuchochezi. CCM ambacho wangeweza kufanya ni kukodi wataalamu kuandaa taarifa za kuzipiku hoja za CHADEMA. Hasa kuthibitisha kwamba maisha magumu hayasababishwi na serikali ya CCM bali na sababu zilizo nje ya uwezo wao. Ndio maana kuna serikali zinakodi watu wa PR ili kujipodoa huko nje ya nchi. Kwa upande mwingine, ndio hasara ya kudidimiza elimu kwa wananchi. Hata uwaelezeje hawawezi kuchambua na kujua mchango wa sababu za ndani na zile za nje katika kutoweka kwa ajira, bei kupanda, huduma kupauka, n.k. wao wanajua serikali ikiamua ina uwezo wa kuweka mambo sawa. Hivyo maandamano ya CCM hapa hayana tija wala hayawezekani bila pilau, usafiri, kanga, t-shirt na kapelo.
 
Mods unganisa hii thread na ile thread nyingine, please.
 
watazomewaje wakipita kwenye ngome ya chadema kama mikoa ya kanda ya ziwa, mbeya, arusha etc 😛lane:
 
Huko kwenye mikutano watakuwa wanaelezea kitu gani? Watawaomba wananchi wa waunge mkono maisha magumu yawe magumu zaidi, bei za bidhaa juu ziwe juu zaidi, malipo ya dowans yanacheleweshwa na mahakama mahakama ilitolee uamuzi haraka suala la dowans ili walipwe na kukodishwa haraka, wanafunzi wa shule za kata wamefeli wa feli zaidi nk, nk,.....
 
Aliomba u-Rais akitarajia atakuwa bwana harusi wa kuzungukwa na wapambe kwa miaka 10 bila kufanya kazi ngumu, sasa maji yamemfika shingoni. Toka ari, kasi na nguvu mpya na kisha ari, kasi na nguvu zaidi hadi kukiri kushindwa hadharani!!! Aibu....
 
Hizo hotuba za Jk kati ya waliokuwa wanamsaidaia ni J Makamba
Sijawahi kusoma hotuba yenye akili,kwa maana ya kujitosheleza kwa hoja na mantiki
Ni hotuba rahaisi rahaisi na nyepesi isiyobeba mambo ambayo yanategemewa kwa wakati husika
Hawezi kupeleka kwa wanazuoni kwa sababu ingechukua sura tofauti,kutokana na uoza wa kimfumo sio rahisi mtu mwenye sifa stahiki kupata hiyo kazi ya kumsaidia raisi katika maeneo kama kuandika hotuba
Hata akipata hataweza kutumia taaluma yake vizuri
 
Ninavyo ijua CCM haiwezi fanya mambo ya kijinga kama hayo ya kuandamana! Ni upuuzi mtupu!
Mkuu, heshima sana! ccm gani unayoongelea? Ni tofauti na ile iliyoandaa na kufanya maandamano ya kuunga mkono uongo wa kikwete kuwa hakuna mtu Tanzania anayekula 'mapanki' au???
 
Badala ya kutatua kero za wananchi walizoziwasilisha kupitia maandamano wao wanadesa. Sasa hayo maandamano yatashusha gharama za maisha au yatatupatia umeme wa uhakika? Watu waliozoea mipasho kamwe hawafai kabisa kupewa uongozi. Wanathibitisha jinsi tulivyochemsha kuwaachia watuongoze. I pity the fool.

haha hiyo avtr yako imenifanya nichekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
ccm walichobaki nacho ni kuita press conference halaf wanaanza kutoa ahadi mwisho ukiwabana wanasema hii nchi maskini na matatizo ya nchi hayatatuliki tokea kipindi cha mzee Nyerere (badala ya Baba wa taifa), then Mwinyi & Mkapa hata mimi mkwere siwezi kuwatoa ktk hali ya umaskini! ...lol, rais ambaye ni mwenyekiti wa chama anatamka hayo! Akienda kwenye mikutano ataahidi nini tena wakati ahadi zake zaidi ya 70 hazitekelezeki! Au aongeze ahadi nyingine! Katibu wake naye ndo kabisa last time I checked alikuwa na mkutano na watoto wadogo (primary pupils)
 
Katu CCM hawawezi kuandamana nchi nzima, maana hiyo itakuwa kuwasha mafuta kwenye kiberiti cha petroli. Kwani chama kama Chadema kitakapoitisha maandamano itakuwa ndio madaraka yao yamekwisha. Na tena wasilogwe.
 
Maneno kwamba mbona fulani kashindwa mm nitwezaje? Hayasemwi wanaume hadharani hasa ulizingatia ni x mjeshi. Uraisi aliomba wa nini kama hawezi kitu cho chote? Maskini wa Mungu

Ndugu umenifurahisha mno. Wakati wanaume wa ukweli kama akina Obama always wanaamini katika ushindi (YES WE CAN) rais wetu anaamini katika kushindwa. Na kwa kuwa imani au maneno huumba hakika si tu kwamba atashindwa bali alishashindwa. Kweli speech yake imemharibia mno. Siamini na haiwezekani kwamba alisema hivyo bali VYOMBO VYA HABARI VILIMNUKUU VIBAYA.
 
hiyo statement hata mi niliisikia.....hivi waandishi wa hizi speech anawachagua mwenyewe au? mbona UD kuna maprofesa....wanahusishwaga kweli kwenye kutoa mawazo kwa mheshimiwa? au labda kaandika mwenyewe?
yaani ninajiuliza maswali mengi sana.

Speech anaandaliwa, shida yake anataka kuweka remix na kuflo friistail, ndo anapoteaga.....
 
Mwenyekiti yuko paris na katibu mkuu sidhani kama anakubalika. Labda mwingine

anakubalika Jamani, yule yupo pale kutibua mambo, hivi unajua kichaa ana faida zake?? kama ulisha wahi kusoma Conflict management basi huyu yupo kwa ajili ya keleta mazingira hayo, sasa kwanini asiwe na faida? inabidi atibue Rais aangalie upepo wenu wananchi, kama mtibifu katibua alafu wananchi mmeendelea kuzabaa basi alipotibua kuna halalishwa cku zinakwenda.
 
Kauli,lawama na hofu, vilivyoshehen katika hotuba ya februari 28,ya rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekit wa chama tawala CCM na kufuatiwa na kukamatwa kwa kiongozi wa mkuu wa CHADEMA pamoja na baadhi ya wanachama ni ishara ya kwamba vyombo vya dola tayari vimepokea amri ya kuanza kuwakandamiza wapinzani hasa CHADEMA.
Haiwezekani kabisa,rais akatumia mda mrefu kukilaumu chama kikuu cha upinzani halafu kesho yake wapinzani wakatwe na kuhojiwa kwasababu za kughushi eti"UCHOCHEZI"hata ile hotuba ya kuwalaumu CHADEMA kwa kisingizio cha usalama wa Taifa inaonesha wazi kuwa ni hila ya kutafuta uhalali wa kuyazima maandamano na mikutano ya chadema,vinavyoendelea kufanyika hivi sasa kanda ya ziwa na baadaye nchi nzima.
Kikwete na chama chake cha CCM,wametambua jambo moja.Utambuzi wao unatokana na uzoefu wa uchaguzi mkuu na matukio baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.CCM na Kikwete wametambua kwamba kuna kila dalili ya kupoteza uhalali wa kutawala Tanzania siku za usoni.
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu za mwaka jana,CHADEMAi ilitoa changamoto kubwa haijawahi tokea tangu kurejewa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hapa Tanzania.CC waliokolewa na Uchakachuaji wa kura za urais,ubunge na udiwani.CCM mpaka walishinda kwa kutegemea uchakachuaji,walijua nguvu ya CHADEMA,kwamba kushindwa kwao kihali haiwezekani.Hi ni dalili ya kuanza kupoteza uhalali wa kutawala tanzania.
Baada ya uchaguzi kumalizika,nguvu ya CHADEMA,iliendelea na mpaka sasa inaendelea kulitikisa bunge la kumi.CCM wakaendeleza hila zao,wakaichakachua CHADEMA kwa kushirikiana na vyama vidogo vya upinzani.Kanuni za bunge zilikabadilishwa kwasababu ya kuogopa nguvu ya CHADEMA.Kwa CCM kutegemea kuendelea kutawala nchi kwa kufanya ujanja ujanja wa mabadliko ya sheria na kupachika pachika vifungu vya sheria ni dalili ya kuanza kuaga na kuondoka kwenye enzi za utawala,ujanja ujanja una mwisho.
Hata kule kuwakamata wapinzani CCM inaona kama kuwatisha ni mbinu muafaka ya kuwafanya waache harakati zao. wakolon wa kiingereza walifanya hivyo kwa viongozi wakuu wa TANU wakaishia kufunga vilango na kwenda makwao.Makaburu wa Afrika ya Kusini waliwakandamiza wapinzani wao wa kiafrika,baadae wakaishia kuondoka madarakan.
UKIONA CHAMA TAWALA KINALILIA DHIDI YA UPINZANI,KINALAUMU UPINZANI BILA SABABU NA KUKANDAMIZA UPINZANI BILA SABABU KWA SABABU TUU UPINZANI UNAANZA KUINGWA MKONO NA SEHEM KUBWA YA UMMA,JUA NI MWANZO WAKE WA KUPOTEZA UHALI WA KUTAWALA.NDIVYO INAVYOTOKEA KWA CCM HIVI SASA.
 
Hayooooo yameshindwa uchaguzi nakubaki kuota oooh CCM ita anguka! Msahau kabisa na 2015 tutashinda na mtasema tumechakachua!
Lazima utakuwa sophia simba wewe.
Eti, hayooo.. yani mipasho mipasho tu'
 
Ushirikina umewakaa sana wale, viongozi wao wote wanavaa pete za majini ya sheikh yahaya nimeshangaa hata wasomi na vijana kama kina Ngereja William naye analo pete kuuuuuubwa.

Kaka mapete ya bahati yale. Si yako pale Mchikichini Safari Jewellers (SONARA KUUUUUUUUUUBWA). Kaka uko nchi gani wewe.
 
Back
Top Bottom