Maandamano makubwa Songea!

Kwa kuwa polisi ni ccm, mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa wa ccm na aliyetoa order amiri jeshi mkuu naye ni wa ccm, nina hakika hakuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya wauaji.
 
Mtindo huu wa kuuana kama kuku sidhani kama unawasaidia polisi,na sijui kama ndio kutimiza ilani ya CCM au nini.Nchi nyingine watu wanapouliwa namna hii watu wanaingia mtaani ili wauwawe wote.Risasi za polisi aziwezi kumaliza watanzania mil.40.Tukiendelea kuwachekea CCM na serikali yake kwa kweli tutegemee kuuliwa kama kuku.Kuna jamaa mmoja hapa JF kwenye signature yake kaweka maneno haya na namnukuu "CCM imechoka kuongoza sasa ni kama inatukomoa" mwisho wa kumnukuu...Haya ndio matunda na matokeo ya kuiweka CCM madarakani.
 
Walaaniwe polisi walimwaga damu isiyo na hatia siku hii ya jumatano ya majivu!! damu hii inamlilia bwana toka ardhini hadi juu mbinguni!!
 


Kwa akili za viongozi wetu zilivyo za kijuha utasikia kuna watu wanaochochea haya na sio wananchi wenyewe,na huwa hayaendi mbali mojamoja yanasema ni CHADEMA...Nyie subirini muone ndio mtajua kuwa tuna viongozi wenye akili tope kupita kawaida.
 
mmemsikia kamanda wa polisi songea anavyosema?

anasema kulikuwa na maandamano yasiyohalali-haramu yaliyo ongozwa na watu 56 waliotaka kuvamia kituo cha polisi,ktk kujihami polisi wame waua kwa bahati mbaya watu wawili tu.hahahahahaha,watu wawili tu wala sio wengi,yaaani wawili tu.

Polisi wamegeuka mungu wanasema watu wawili tu ndio wame waua ila 54 waliobaki wapo hai hahahahahaha,polisiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

haya bwana,sina imani na hiyo taarifa ya watu wawili tu kutokana na tabia ya polisi kuwa sio wa kweli ktk kutoa taarifa zao.
 
Pasco kwa kutufanya tuamini zaidi atasema hata yeye alikuwepo Songea wakati wa tukio hakuna mauaji ila ni polisi ndio walioshambuliwa tunawasingizia. Mmesahau ya Apollo.

hahahahaha
mimi nataka siku moja Pasco nae wamkamue moja itokee upande wa pili,sijui hapo atasemaje,mwenzake Mh Hamisi kigwangala alikoma maana walimbambikia kesi na vibao wakampa baada ya hapo ndio akaelewa kuwa polisi bwana wapo kwa ajili ya wenye pesa na ni pangu pakavu,sasa nasikia huyo wa songea yeye ndie mfanya biashara mkuu wa meno ya tembo,so uki ingia ktk anga zake tu yeye ni mungu ametoa na pia anatwaa fasta utadhani hatakuja kufa.

halafu wakifikia mda wa kuzeeka wana okoka na kumrudia bwana.kaaaaaaaaaaaaazi kwelikweli
 
التمزق لجميع الذين فقدوا حياتهم القتال من أجل حقوقهم الأساسية!
 
Mheshimiwa DCI Manumba hizo ndio taarifa za kufanyia kazi, usingoje kusimuliwa tuma vijana wapate ukweli!!! Vinginevyo squad ya Zombe mpya itatokea au pengine tayari ipo inauwa watu kimya kimya!!!! Fuatilia bwana wacha kujichimbia ofisini ukisubiri eti uletewe!!!!Ushauri wa bure!!!!

 
dunia imefikia mwisho lakini mungu hawaondolee roho mbaya binadamu. hii taarifa ni ya kweli kabisa

Hilo ndilo tatizo la kuingiza siasa mpaka za kusimamia sheria kama police 7bu siku hizi wanajulikana kama policcm
 
Uletaji wa taarifa wa namna hii na unataka watu wajadili sidhani kama unakubalika kwenye jukwaa makini kama hili.Wewe ndio mleta taarifa sasa unataka nani mwingine atoe taarifa? Sisi hatujui wewe ndio unajua sana unauliza kwetu ili iweje?

Kwani kuleta taarifa hapa ndo inamaanisha unajua kila kitu? na kwani hakuna mwingine anaweza kuwa na hiyo habari humu jamvini na kutoa ufafanuzi zaidi? Yafaa kufikiria kwa makini kabla ya kufanya post yako hapa
 
Kaka mbona wewe unaonekana mzoefu hapa JF ..........wewe kama hunandugu Songea tulia..........acha wenye jamaa songea wapige kisha tutajua kinachoendelea.

Pia waloko songea wanaweza kutujuza
 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma anadai mauwaji ni ya kishirikina
 
Nilisema usishangae viongozi wetu majuha watasema vurugu hizi zimesababishwa na siasa...kwa masikio yangu na macho yangu nimemsikia kiongozi mkubwa wa mkoa wa RUVUMA bahati mbaya sikushika jina lake na cheo chake akiongea kupitia TBC 1 Habari akisema,vurugu zile zimesababishwa na hisia za uchawi na siasa...huu ndio ujuha wa viongozi wetu.Wameshindwa kutimiza wajibu wao kulinda usalama wa raia wanakuja na hoja kuwa ni siasa...stupid!!
 
Kweli kabisa watu 56 ndio wameshindwa kudhibitiwa na polisi bila kuwafyatulia risasi? kweli wengine tumesema hili jeshi linahitaji kuvunjwa na kuundwa upya bado lina mawazo ya kikoloni sana!

Inashangaza sana ndugu, our police are trigger happy people, hivi hakuna mbinu nyingine za kudeal na public disorder other than shooting. This is about life, families losing their loved ones.

It's appalling seeing someone dying when demonstrating about their rights. INAUMA SANA,
 
inawezekana kabisa hata hao nane wameuawa na polisi wadoria,ije vita tu nadhani watuwana hamu ya kutumia risasi za moto
 
Polisi wa Tanzania akili zao zipo masaburini, kama walivyo wakuu wao wa Serikali na Bunge.
 
Mimi mwenyewe nilikuwa barabara ya songea-mbinga hali ilikuwa ni mbaya sana namshukuru mama aliyetupatia maji ya kuzimua mabomu
kuna askari mmoja alikuwa kihelehele alikaribia kufika nilipojificha akanikosa
vifo ni watu watatu na majeruhi ni wengi taarifa zaidi kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…