Maandamano kupinga ujio wa Prince Charles | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano kupinga ujio wa Prince Charles

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Nov 6, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wakuu jioni ya leo wale wote wanaopinga sera za uingereza za kushinikiza Tamaduni za kishetani kama vile upewaji wa misaada kwa ushoga basi naomba mshiriki maandamano makubwa ya kupinga ujio wa prince charles katika nchi yetu ili tuonyesha hatutaki mashinikizo yao na tupo tayari kwa kujitoa jumuia ya madola.

  kwa kila unachoweza ata ikiwa kuziba njia kuzomea au kwa kila ishara basi fika uwanja wa ndege leo kushiriki maandamano haya
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Na mabango ya kupinga ushoga
   
 3. Fang

  Fang Content Manager Staff Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 489
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  That is what is called "kumpigia mbuzi guitar"
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwanini tusherehekee miaka 50 kwa kumwita mkoloni wetu tena wakati huu ambao viongozi wa taifa hilo wametoa kauli ya kishenzi dhidi ya mataifa yaliyo kwenye jumuia ya madola.


  Hatumtaki kukanyaga nchini kwetu mwakilishi kutoka taifa la kishetani la uingereza
   
 5. S

  Sheba JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Godwine Ndugu yangu unamuandamania nani? Unachoshawishi hapa kifanyike ni sawa na kuwaambia wananchi waandamane kwenda polis kushinikiza kuachiliwa kwa mtuhumiwa au mfungwa ambaye yuko rumande baada ya uamuzi wa mahakama.

  Prince Charles ni mwakilishi wa Royal Family, hana mamlaka ya kisera. Hatoi msaada wala hawezi kuzuia msaada kutolewa na Serikali yake. nguvu yake kiushawishi ni ndogo kuliko hata ya Ridhiwan Kikwete.

  Mkiandamana wenyewe watawashangaa kweli na kujua upeo wenu wa akili na kuwadharau. Maandamano hayatamtikisa maana atajua tu mmekosea njia au hamkutaarifiwa vyema kuwa anayekuja ni Prince Charles na si Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye ndio angestahili mabango hayo. Isitoshe, kwa dola na demokrasia komavu kama Uingereza, wamekwishaona sana maandamano duniani ya kila aina. Wala maandamano hayawatikisi maana ndio sifa ya ubabe lazima upingwe. Wao muhimu kwao ni Kama maandamano hayo hayatawadhuru tu. Mindhali hampigi mawe, tengenezeni tu mabango hata mkitaka ya digital muandamane hadi mridhike.
   
 6. u

  ureni JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mkuu huyu jamaa anayetaka kuandamanisha watu kama nilivyomuelewa anataka ujumbe ujumbe ufike,usisahau huyu prince anaheshimika sana nchini kwao na atakuja na vyombo/waandishi mbalimbali wa habari duniani,sasa huyu jamaa akiandamana na bango lake moja kwa moja mpaka CNN itakua imekamata hivyo ujumbe wake atakua ameshaufikisha duniani kiraisi bila kutumia nguvu nyingi.La maana analotakiwa kufanya akachukue kibali cha kuandamana ili kuepukana na bugudha kama wanayopata wakina Lema.
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nadhani kuna kitu ambacho bado haujakifahamu , katika uingereza nguvu za taifa hili liko kwenye familia ya kifalme lakini mwongozo wao unaitaka familia ya kifalme kutoingilia uendeshaji wa serikali mpaka watapoona mwenendo wa serikali unaweza kusababisha maafa au athari kwa taifa la uingereza kwa mfano pale wanapoona taifa la uingereza linaweza ingia vitani au kutengwa na jumuia ya kimataifa.

  Pia tambua sheria za uingereza zimeipa nguvu familia ya kifalme kupitia kwa mfalme au malkia uwezo wa kuvunja serikali iliyo madarakani na kuitisha chaguzi mpya pale wanapoona maslahi ya uingereza yanapotea
   
 8. C

  Chief JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Badala ya kuandamana kumtoa msanii magogoni anayeangamiza nchi?
   
 9. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,463
  Likes Received: 10,672
  Trophy Points: 280
  nategemea membe awe wa kwanza kuandamana na sio kwenye msafara wa kumpokea huyo prince au princess
   
 10. S

  Sheba JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Godwine, utatusaidia sana ukifika mifano ambayo Malkia ameonyesha mamlaka yake hiyo. Malkia ni symbolic figure head tu kwa sababu za kihistoria. Tafadhali rejea Commercial Revolution in UK katika karne ya 16-17.

  Hata opinion polls nchini Uingereza zinaonyesha jinsi popularity yake inavyoteremka siku hadi siku kutokana na mabadiliko ya kizazi. Hadi sasa, hoja pekee inayomtetea ni hoja ya kiutamaduni na historia.
   
 11. J

  JALUO Senior Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu lema tayari ni shujaa tatizo lenu nini msipomtaja shujaaa? Huyo mme wenu prince atawashughulikia tu coz inaonesha mnamind kinoma.

  Jamaa inaonekana anawakera kwa kutaka kuandamana na kuwapeperushia rijali wenu tena handsome,,,jamani si jana tu nyie ndoo mlikua no 1 kutoa tamko..ooooh hatutaki misaada yenye shinikizo, oooh hatutaki wanaume kuolew,,,eti leo tena mnawashwa...mmmh kweli a green snake in a green grass...

  Sie wanaharakati huu ndo mda wetu wa kuonesha hisia zetu juu ya aina yoyote ile ya dhuluma...nyie huu sio utamaduni wenu.siunaona ata kujivua gamba tu kulivyo wamaliza je hili kubwa mtaliwezaa???mwiteni kamanda 1 tu kutoka cdm awape maelekezo on what to do on your magamba....ushoga nooooooooooooooooooooo
   
 12. rasmanyara

  rasmanyara Senior Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Taarifa za kiintelejensia zinasema kunauwezeka wa Al shaababu kuwepo nchini so halitawezeka kua na maandamano.
   
 13. S

  Sheba JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe. Kama ni kupata photo opportunity pendekezo lake ni sawa kabisa na nadhani angeendelea tu, na ushauri wako kuwa afuate Sheria na taratibu ni mzuri tu. Maandamano yoyote hutengeneza news na haya mabango hayatakuwa exceptional. Kama nilivyoeleza awali, nchi zao zimezoea wala hayatakuwa unique. Muda huo pengine ungetumika hapa kujadili Katiba na mustakhabali wa taifa letu.

  Alikuja hapa George Bush ambaye alishawahi hata kutupiwa kiatu. Watu wakaomba kuandamana, wakapewa kibali wakandamana picha zikapigwa na hata hazikuwa na impact hata kwenye magazeti yetu tu.

  Kwa kifupi, maandamano haya hayatakuwa na impact. Angalau umefafanua kuwa lengo ni kupata attention ya international media. Kama hivyo wanaweza kupata. Lakini mwenye thread hii hakusema lengo ni nini. Pengine atufafanulie.

  Lakini cha kushangaza zaidi, wale waratibu wetu hodari wa maandamano (people's power) mbona wamekuwa kimya kabisa? Sio ndio tungewapa jukumu la kuratibu maandamano hayo? Au wanaunga mkono Sera ya Conservative Party kwa kuwa nao ni wanachama wa Conservative Parties walikuwa Vice Chairman wa umoja huo?
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nijuavyo mimi maandamano lazima yawe na kibali, ni bora mhamasishaji angeweka wazi kama kibali kimepatikana au kimefikia wapi ili watu wajiandae kwa ajili ya maandamano ya amani. Huo ni upande mmoja, upande wa pili ni vigumu kwa serikali yetu kuruhusu maandano hayo kwa kutoa kibali kwa sababu za kiintelejensia.
   
 15. u

  ureni JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mkuu kweli wewe umepotea mwelekeo kabisa kwani CHADEMA wanapata wapi fedha za kurusha helikopta Tanzania, ni huko huko UK ndio wafadhili wakuu wa CDM. Kwani umeona comment yoyote ya CDM kuhusu hili suala la USHOGA kimyaa.
   
 16. G

  Godwine JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mfano mzuri ni chaguzi uliopita uingereza baada ya kutopatikana mshindi mwenye viti vya kutosha kuongoza serikali malkia alitoa muda wa vyama vya siasa kuweza kufanya coalition(kuungana) na kama katika kipindi hiki kusingewezekana kufanyika ushirikiano wa conservative na mwenzio wanaongozana nae pamoja, malkia angetoa muda kwa chama kinachofuata kama na chenyewe kinaweza kushawishi muungano wa kuunda serikali na chenyenye kikngeshindwa basi malkia angeteua serikali


  Pia uingereza haiwezi kuingia vitani bila ya sahihi ya mfalme au malkia , kumbuka sakata la king George  soma majukumu mengine kwenye mwongozo wao http://projectbritain.com/royal/role.htm
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,183
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  Al shabaabu ipo!, jeshi la polis lipo mbioni kupiga marufuku mikusanyiko yote zikiwemo ibada!
   
 18. S

  Sheba JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Godwine asante. Mamlaka haya si mamlaka ya kisera. Mamlaka ya kisera yana hulka ya kuathiri bajeti na programs. Haya ni mamlaka ya symbolic head. Queen ni unifying factor. Kwa Uingereza, queen ni custodian wa historia na anabeba taswira ya Ufahari wa taifa lao. Ndio maana inapendeza akitangaza vita yeye lakini kazi yote inakuwa imefanywa na executive.

  Ni sawa na sisi Amiri Jeshi Mkuu ni Rais ambaye inawezekana hata hajawahi kupiga risasi lakini inapendeza akitangaza vita. Kila nchi in Mfumo wa symbolism na rhetorics za namna hiyo. Ni njia ya kujitambulisha duniani kuwa nawe upo. Sie Rais akifika mahala waxed wa ukoo wanampa silaha na kumtangaza Chifu au Mtemi wa Kabila fulani.

  Nachelea kusema, mamlaka yake ni ya formality kutokana na utamaduni wao na si mamlaka ya kidola.
   
 19. V

  Victim Member

  #19
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [
  QUOTE=Chief;2766655]Badala ya kuandamana kumtoa msanii magogoni anayeangamiza nchi?[/QUOTE]

  How true - Uwoga imetuzidi
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hoja ni nyingi sana lakini wajumbe wa maandamano haya ya kupinga ujio wa kiongozi wa taifa la kishenzi la uingereza yanaendelea na tumeshawatumia polisi fax watambue kuwa leo ni maandamano makubwa kupinga ujio wa mwakilishi wa familia ya kifalme pamoja na balozi wao nadhani pindi fax hiyo itapojibiwa na ok ya maandamano nitaiweke ubaoni na kama wakikataa pia nitaiweka ubaoni
   
Loading...