Maana na asili ya neno “BABATI” jina la wilaya mojawapo ya mkoa Manyara.

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Mji wa Babati ni mji wenye historia ya kipekee nchini Tanzania.Kihistoria asili ya jina ‘BABATI’limeanzia tangu miaka ya 1918 wakati wa ujenzi wa barabara iliyokuwa ikipitia katika maeneo ya mji wa Babati wa leo hii wakati wa ukoloni.

kuhusu jina ‘BABATI’ Msimamizi mzungu mjerumani wa ujenzi wa barabara aliyekuwa akisimamia waafrika wafanyakazi waliokuwa wakitengeneza barabara katika maeneo ya makazi ya vijiji vya wananchi wenyeji katika mji wa leo hii wa Babati alimuona kijana mmoja wa kiume wa kabila la kigorowa nje ya kibanda cha nyumba na pembeni yake walikuwepo wazee wawili wanaume wamesimama na waliokuwa katika maongezi.

Msimamizi huyu mzungu mjerumani wa ujenzi wa barabara akamsogelea kwa ukaribu kijana yule wa kabila la Kigorowa na kumuuliza amtajie jina la kijiji kile alichokuwa akisimamia ujenzi wa barabara.

Yule kijana wa kabila la kigorowa hakuelewa lugha ya kijerumani aliyozungumza yule mzungu mjerumani na hivyo basi katika hali ya kufikiria tu akazania ya kwamba anamuulizia kuhusiana na wale wazee wawili wanaume wagorowa ni yupi aliye Baba yake kati ya wale wawili.

Hivyo basi yule kijana wa kabila la Kigorowa akamtazama mzee mmoja kati ya wale wawili ambaye ni Baba yake mzazi na kumjibu yule mzungu mjerumani katika lugha yake ya mama- “BABATI” ikimaanisha ya kwamba huyu
ni Baba yangu (This is my father).

Mara moja yule mzungu mjerumani msimamizi wa ujenzi wa barabara akaandika katika kitabu cha kumbukumbu –‘BABATI’ na mpaka leo hii katika lugha ya kabila la Wagorowa neno Babati maana yake ni (Huyu ni Baba)
 
Back
Top Bottom