Maana mbaya ya Emojis kwenye Jamii imefanya nikosane na Bebi wangu

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Salamu nishawaachia waswahili!



images (1).jpeg



Hii Emoji sijajua kwenu ina maana gani lakini kwangu ninavyofahamu ni Tunda aina ya Fulisi(Mafulisi) au kwa kisorongai uitwa Peach(Peaches).

Mimi huwa ni mdau mkubwa sana wa haya matunda,juzi nimeyanunua ya kutosha pamoja na matunda mengine,hivyo sikupata muda wa kuyatumia kwa kuwa nilisafiri.

Kwakuwa Demu wangu huwa anakuja na kukaa siku kadhaa na kuondoka kuelekea kazini,pale nyumbani anabaki binti wa kazi pamoja na wadogo zangu 2(Mmoja Ke na Mwingine Me).Wakati nachati na Bebi nikamwambia akiondoka amwambie binti wa Kazi ahahakikishe ananitunzia 🍑 kwasababu nayapenda sana!.

Eeeeeh!,kumbe mwenzangu sijui kichwani alifikiria nini!,Aiseeee hajaanza kuniwakia!

Bebi akaanza kunituhumu na kuniambia eti kumbe yeye akitoka mimi huwa natembea na binti wa kazi,Yaaani aliwaka na akawa mkali kweli,nikajaribu kupiga simu na kumuelewesha lakini holaaaaa!.

Nimeambiwa akirudi asimkute binti wa kazi la sivyo mimi na yeye mahusiano yetu yatakuwa yamefikia mwisho.Kwakuwa nampenda na sikutaka kumuudhi Black Beuty wangu,jana nikampatia binti wa kazi nauli na pesa ya kutosha nikampeleka Mbezi Stand akapande gari arudi kwao.

Hadi sasa sijajua kosa langu mimi ni lipi!.

Haya mambo ya kutumia Emojis za matunda na kuyahusisha na mambo ya hovyo yatakuja kutuletea matatizo makubwa mnoo!
 
Ungemuandikia kwamba unapenda sana yamkini angeshangaa pia!!

NB: Next time angalia na trending, usije ukatafsirika tofauti!

Sio kila kitu kina maana ile inayoonekana, vingine vinamaana tofauti!!

Ongea naye taratibu, huku ukimuaminisha kwa dhati maana uliyokusudia!!
 
Ungemuandikia kwamba unapenda sana yamkini angeshangaa pia!!

NB: Next time angalia na trending, usije ukatafsirika tofauti!

Sio kila kitu kina maana ile inayoonekana, vingine vinamaana tofauti!!

Ongea naye taratibu, huku ukimuaminisha kwa dhati maana uliyokusudia!!

Mkuu hiki kizazi cha sasa kinashida sana!
 
Back
Top Bottom