Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Nilishasema toka awali kua huyu mama anakurupuka sana watu wakapinga vikali. Mpaka hapa sijaona mwelekeo wa mafanikio kwa uwepo wa huyu mama Wizara ya Elimu. Wizara ya ELIMU sio NECTA, sio taasisi ndogo! Hii wizara ndio moyo wa nchi.

Sijui mwaka huu vyuo vikuu vingapi vitakavyopokea wanafunzi wa fani za Sayansi. Utaratibu wa kizamani sana huu.
We mchawi
 
Naongezea: mara uhakiki, rara kuwanyang'anya digrii wale wahitimu hata walio kazini ambao kwa mtazamo wake hawastahili au hawakustahili kuwa kusoma hadi kufikia kiwango cha hizo digirii...
We nawe mchawi na mzandiki
 
We The boss siku hizi ni kama umechanganyikiwa unaendekeza chuki kisa mamvi si raisi.
Hivi ulikuwa wapi kuyashangaa maamuzi ya Mungai wakati akiyaondoa masomo ya biashara na kilimo na kubakiza ya sayansi.
Kuna ubaya gani wanafunzi kuyasoma hayo masomo ya sayansi ?
 
Umeeleza vizuri,ila hapo la akili ni maamuzi ya mhusika jinsi atakavyo itumia. Mfano,nikwanini tuwe na shule za serikali zinazochukua wenye ufaulu wa juu kwenda hizo zinazo itwa special,wengine waende shule za bweni na wengine wapelekwe shule za kata ambazo hata cutoff point hazieleweki,kila mwaka zinabadilika kutegemea idadi ya wanaomaliza.
Nilisha sema nyie mnatengeneza mazingira yakuhukumu walimu nasivinginevyo,binadamu tunatofautiana uelewa hata kujitambua pia.

Mungu si mjinga kutupa AKILI wanadamu wote, wala hajawa mbaguzi ktk kugawa AKILI.

Kwa hiyo Tumtendee haki kutumia AKILI Zetu.

Maendeleo ya China ambayo kila mtu anayafurahia leo ni msisitizo mkubwa wa science. China kwa sasa ni nchi inayoongoza kwenye kuzalisha maengineer na watu wa sayansi na ndio hao wanaokuja na kila products.

Haina maana kwamba kuna watu wataacha kusoma masomo mengine. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba sayansi positive effect yake ni kubwa kuliko kwingine.

Kwa kukusaidia tu soma kitabu kinaitwa HOW THE WASTE WAS LOST by Dambisa Moyo.
 
Kama tumekubaliana kuwa mtu anaitumia akili yake apendavyo ili kupata maarifa anayoona yanamfaa hapo tuko pamoja.
 
Kama tumekubaliana kuwa mtu anaitumia akili yake apendavyo ili kupata maarifa anayoona yanamfaa hapo tuko pamoja.
Hapana hapo hatujakubaliana.

Mimi nimekubaliana na Profesa Ndalichako kwa kutaka kila Mwanafunzi asome masomo.

Kumbuka saivi tunasema Nchi ya Viwanda. unadhani tufafikia lengo bila kuweka mkazo kwenye Sayansi Mkuu?

Tunapotaka ku pursue a greater goal za Nchi lazima tukubali mabadiliko
 
Mimi nashangaa kitu kimoja tu kwa nini mtoto afundishwe kwa lugha moja level flani afu aendelee kwa lugha nyingine level inayofuata?kama huyu shangazi anahitaji hawa vijana wasome sayansi basi aanze kurekebisha mfumo wa lugha ya kujifunza iwe moja kutoka primary hadi sekondary kama ni kiingereza au ni kiswahili...itakua rahisi zaidi kukabiliana na hayo masomo ya sayansi
 
Hapana hapo hatujakubaliana.

Mimi nimekubaliana na Profesa Ndalichako kwa kutaka kila Mwanafunzi asome masomo.

Kumbuka saivi tunasema Nchi ya Viwanda. unadhani tufafikia lengo bila kuweka mkazo kwenye Sayansi Mkuu?

Tunapotaka ku pursue a greater goal za Nchi lazima tukubali mabadiliko
Kwahiyo mtalazimisha ufaulu kwa mtoto ambae hataki kufaulu hilo somo?
 
Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?

The Boss

Maendeleo ya China ambayo kila mtu anayafurahia leo ni msisitizo mkubwa wa science. China kwa sasa ni nchi inayoongoza kwenye kuzalisha maengineer na watu wa sayansi na ndio hao wanaokuja na kila products.

Haina maana kwamba kuna watu wataacha kusoma masomo mengine. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba sayansi positive effect yake ni kubwa kuliko kwingine.

Kwa kukusaidia tu soma kitabu kinaitwa HOW THE WASTE WAS LOST by Dambisa Moyo.
 
Tusitafute visingizio Mkuu. tuweke mkazo saaana kwenye Sayansi
Mimi naongea kwa uzoefu,nilisoma technical school haikuwa na combination zaidi ya PCM tu,na kigezo kikuu kwenda huko ilikuwa ufaulu wa juu ktk hesabu za darasa la saba. Shule ilikuwa inapata div 1 mpaka 80 lakini sikwasababu ya walimu wala waziri kasema
 
Wengi mmeona habari ya leo kuwa sasa ni lazima wanafunzi wote wasome Sayansi kabla ya hiii zimekuwepo habari nyingi za kushangaza za wizara hii ya elimu. Siku Magufuli aliposema anashangaa fimbo kupigwa marufuku mashuleni, kesho yake tu Wizara hii ikatangaza 'fimbo kurudishwa mashuleni'
yaani halikuwa na mjadala wala kutolewa maelezo labda why fimbo zilizuiwa mwanzo au kuna watalaam gani walihusika kufikia maamuzi.

Halafu yakaja maamuzi ya kuongeza ufaulu ili kujiunga na vyuo, hili nalo limechukuliwa kama Tanzania ni kisiwa vile mpaka sasa wala hakuna maelezo iwapo mwanafunzi wa kitanzania akipata nafasi kusoma nje ya nchi kwa ufaulu ambao hapa nchini haumruhusu, vyeti vyake vitakuwa na 'status' gani hapa nchini mradi maamuzi ya wizara hii sasa ni kama vile Tanzania ndo 'The world'
na kila atakachoamua yeye ndo 'final'

Huyu mama na Mabosi zake wanasahau kuwa tuko katika 'global village' Maamuzi ya ajabu ajabu sanasana yatawaathiri watoto wa masikini tu
wengine wenye options za kusoma nchi jirani na nchi za mbali hayatawagusa na mwishowe watakao 'umizwa na maamuzi' haya ni watoto wa masikini.Sasa hili la lu kulazimisha Sayansi nalo unajiuliza nchi ngapi duniani linatumika?

Je mtoto wa kitanzania akisoma Kenya au Uganda au kwingineko
ambako hakuna 'maamuzi ya aina hii' huyu mama atafanyaje? Hivi why 'tuna invest kwenye kuongeza kero na vizingiti' vya kila aina kwa watanzania? Kwani Tanzania ni kisiwa? Si masuala ya elimu yanapaswa kuwa 'Universally acceptable'? Sasa huyu mama ndo mifano wa maprofessa wetu?
Hivi vitu vya kukurupuka vina kikomo chake, only time will tell. Wanajiita maprofesa halafu wanakuja na tafiti za kizumbukuku. Walianza kubugi kwa kupandisha madaraja ya kudahili wanafunzi huku wakiwa hawajua kuwa wanaosoma michepuo ya sayansi ni kama walisacrifice kutokana na mazingira mabovu ya kusomea sayansi kwa maana hiyo kupandisha point maana yake ni kuwakatisha tamaa, naona wamegundua hili sasa wakadhani kulazimisha kusoma sayansi ndo suluhisho kumbe wanazidi kuongeza tatizo juu ya tatizo maana kama ni kusoma sayansi watasoma lakini je matokeo yatakuwaje?
 
The Boss

Maendeleo ya China ambayo kila mtu anayafurahia leo ni msisitizo mkubwa wa science. China kwa sasa ni nchi inayoongoza kwenye kuzalisha maengineer na watu wa sayansi na ndio hao wanaokuja na kila products.

Haina maana kwamba kuna watu wataacha kusoma masomo mengine. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba sayansi positive effect yake ni kubwa kuliko kwingine.

Kwa kukusaidia tu soma kitabu kinaitwa HOW THE WASTE WAS LOST by Dambisa Moyo.
Tatizo sio kulazimisha kusoma sayansi ndugu, tatizo ni je hawa watoto wanaoambiwa wasome sayansi wameandaliwaje mazingira ya kusoma hiyo sayansi? Je kuna vifaa vya kutosha vya kujifunzia, vitabu, maabara za kufanyia majaribio, walimu wa sayansi wa kutosha nk. Mwanafunzi anafundishwa jinsi ya kutumia test tube na wala hajawahi kuiona hata siku moja, unamfundisha mwanafunzi preparation of oxygen kinadharia sasa kwa nini huyo mwanafunzi asione sayansi ni kama hadithi za alfu lela ulala, saa nyingine shule ina walimu wawili wa sayansi shule nzima unakuta mwanafunzi anapata kusoma vipindi viwili kwa mwezi kutokana na mwalimu kubalance angalau aweze kufundisha vidato vyote, sasa hapo unawezaje kuchukua mfano kutoka china? je ukifanya china kama case study unajua china iliwezaje kufaulu hiyo falsafa ya kusoma sayansi? je na wewe upo tayari kuiga kama wao bila kupinda sehemu yoyote? Au sisi tunatoa matamko tutegemee matamko yatatufikisha kama wale? Kwa hiyo unapotoa mfano inabidi uwe tayari kuuishi huo mfano
 
Mkuu nimekuelewa.

Ila ungefanya bidii kidogo kusoma nilichosema toka mwanzo wa huu mjadala usingesema hivyo.

Nilisema lazima tuwaandae Wanafunzi na Walimu wetu.

Lzima kuwe na mazingira bora kwa kila Upande.

Utaniuliza kwanini tamko si mazingira kwanza . na mimi ntakujibu mbona Shule za kata zilianza kabla kuwa na walim?

Leo Impact ya shule za kata mnaiona au hamuioni?
 
Back
Top Bottom