MH.NDALICHAKO HII SIYO NECTA
Kwa kipindi cha miaka tisa alifanyakazi ya katibu baraza la mitihani japo marachache nyuma alioneka akifanya masuala ya utafiti na shirika la elimu la aghakhan.Siukatai uwezo wake mkubwa kipindi hicho cha nyuma ingawa amepata bahati baada ya kutoka masomoni anakutana na fursa ya uwaziri......
Sikuzote unapoipata fursa ni lazima umuonyeshe alikupa kuwa hajapoteza...kwa kipindi kirefu umekuwa ukijishughulisha na matukio baadala ya matatizo yanayoikabili sekta ya elimu...Najaribu kutafuta nini umefanya ili baada ya miaka miwili mitatu tukukumbuke kwa kusema hichi ni chafulani au unataka tuseme baadae matatizo haya kayaleta ndalichako.......
UTATA WA MH.NDALICHAKO
Kuna vitu mh waziri amevifanya mpaka unajiuliza huyu ni waziri au nani kasema? Baadhi ni:-
1:masomo ya sayansi lazima
Hivi waziri ulishindwa kutengeneza miundo mbinu bora kuboresha maslahi ya walimu wa sayansi na kuandaa walimu wakutosha motisha n.k wala ilikuwahaina haja kulazimisha wenyewe wangeenda....
Mfano mzuri jiulize kwanini raisi magufuli ni mwalimu mzuri wa sayansi mzuri aliacha kazi ya ualimu akaenda kiwandani baadae kwenye siasa...sababu zilizomtoa yeye na wengine zinawatoa pia......
2:ubora wa baadhi ya vyuo vya elimu ya juu....
Kimsingi huwezi ukatibu tatizo hili kwa kusema wachuo fulani wakienda chuo fulani warudie mwaka mmoja nyuma kwa kuwa ubora tofauti ilihali hawa maprofesa ndiyo hao hao kilachuo......
Lakini nikukumbushe kitu ulikuwa huna haja kuwaambia warudie mwaka kwani kila chuo kikuu upo utaratibu wa KUSAP na KUDISCO sasa hivyo ndiyo vilikuwa vipimo kuwa wana ubora au la kuliko kusema asiyetaka arudi kwao(huu ni ubabe).....
Ulichotakiwa kufanya nikuuangalia upya mfumo mzima wa elimu ya juu ikiwezekanafumua wote......
3:utoaji adhabu kwa wanafunzi
Hili jambo naona mara ya tatu unalirudia kana kwamba waalimu awajitambui vile..kifupi kwa sheria ya adhabu mashuleni hakuna mwalimu mwenye muda mchafu wa kuweza kuitekeleza kila mwalimu anamambo yake ya kufanya......
MWISHO
Kama utaendelea kuwa waziri wa kuzindua na matamko ukifikiri bado upo necta na kusahau kuwafikiria walimu tutegemee kushuhudia waziri mbovu ndani ya wizara ya elimu baada ya magreth sitta na mungai kutokea