Maamuzi ya Mbowe yanaididimiza CHADEMA

Maamuzi ya Mbowe yanaididimiza CHADEMA

Chadema asili ndio kina nani hao?
wale ambao sio maslahi wapo wengi; ambao hawapendezwi na maamuzi ya Mbowe lakini hawana pa kusema. Nawasaidia kutoa nyongo zao.
 
wale ambao sio maslahi wapo wengi; ambao hawapendezwi na maamuzi ya mbowe lakini hawana pa kusema. nawasaidia kutoa nyongo zao.
Hawana pa kusemea kwa hiyo wamekuja kusemea kwako ndio ukajua nyongo zao ni zipi? Au wewe ni mganga wa kienyeji/mchawi/mfumu/kalumanzira, etc kiasi cha kujua hao ambao wameshindwa kusema walitaka kusema nini?
 
Mkuu Anzisha Chama chako! Uko huru Kabisa Yaani. Kwanini uhangaike Na CDM? Mbona Mbowe Ni mwanaume Kama wewe tu, Hamna tofauti yeyote baina yenu ya kimaumbile, kwanini yeye aweze wewe ushindwe? Kwanini usononeke Na maamuzi Yake Wakati Na wewe una nafasi ya kuanzisha Chama chako!
 
Halafu ungeanza Na mwenyekiti wa Chama chako, Mbona yeye alikuja Na Magufuli instead of chaguo Lenu? Kwanza Mwambie imetosha ampishe mwenzie.
 
sidhani hapo chadema kuna kidume hata mmoja ana uwezo wa kupingana na maamuzi ya mbowe; atachosema ni finals; that is not healthy.
Vipi nyie hapo lumumba?. Ajabu nyani anamcheka kundule
 
Kinachoonekana kwa CHADEMA kwa sasa ni maamuzi ambayo yanakiua chama taratibu.

Tujikumbushe uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais kwa chadema ambae baadae alikuja kuwa mwakilishi wa tiketi ya ukawa.

maamuzi yalifahamika kama kubadili gia angani. Kumtosa mfia chama na mpiganaji wa muda mrefu dr. Slaa ilikua dhihaka kwa wapambanaji wengi. Maamuzi haya hayakuwafurahisha wengi.

Hivi majuzi tena tukasikia kauli nyingine tena akiahidi kuwaletea wanaCHADEMA katibu mkuu makini.

Kilichotokea kinafahamika; uteuzi haukushawisi wana CHADEMA asili wanaona wamesalitiwa.

Mifano hiyo miwili ni katika kuonesha tu ni kwa namna gani maamuzi ya mwenyekiti yamekuwa yakikigharimu chama.

Inaweza isionekane kwa haraka ila kinachotokea ni mipasuko kila baada ya maamuzi flani toka ngazi za juu.

Wahusika watalipinga hili lakini ukweli lazima usemwe kuwa; maamuzi hayo na mengine kama hayo taratibu yana kipumzisha CHADEMA.

Kwa aili zako ukitaka amteue nani katibu mkuu,na kwa akili zako anadhani slaa angekipatoa chama kura milion sita?
 
Inawauma sana kuwa na katibu mkuu msomi duniani sio huyo mwenye elimu ya kubumba na vyeti kama hivi. Cheti cha kugawa kofia
chti cha kugawa kanga.
Cheti cha kugawa tishet
cheti cha kugawa bendera. Dah watu na vyeti vyao chezea acha kabisa.
 
Umemsaidia mleta thread kuthibitisha aliyoyasema maana, mmekuwa viziwi kwenye ukweli. Maamuzi hata kama ni mabaya, ili mradi yametoka kwa mtu fulani, basi waliobaki wanaimba chorus tu. Hili ndilo analosema mleta thread na msipoamka toka usingizini, hakika you are headed to oblivion.

Nyie hivi nani analeta jina la katibu mkuu? Na kama hatakiwi asingepata kura mabunyenye nyie
 
Kimsingi chadema walicheza kamali kumchukua lowasa.

ni sawa na mfanyabiashara anayekuwa anafanya kazi kwa kuvuja jasho jingi lakini anapata mafanikio ghafla ikatokea kamali ambayo unacheza kwa fedha nyingi na ukibahatisha unakuwa tajiri mkubwa. mfanya biashara huyu akachukua mtaji wote akaweka kwenye kamali ili akibahatisha awe bilionea lakini akikosa anakuwa masikini maana mtaji umepotea.

chadema wana kazi kubwa kujenga tena misingi ya chama maana waliibomoa kwa kuwakumbatia watu ambao kwa itikadi zao walikuwa ni watu waliionekana kukwamisha nchi na wao huko nyuma wakionekana ndio wanaoweza kuwa wakombozi wa kweli kwa wananchi.

mtihani wa kupata madaraka katika uchaguzi wa mwaka 2015 umewafunua ukweli kuwa hawa walikuwa watu wanaopiga kelele kupata madaraka tu na wakiyapata wanaweza kufanya yale yale.

walijisema kuwa wao wanasafisha wachafu na kuwa wasafi wakasahau kuwa maji yakisafisha chombo mwisho wake ni maji yaliyosafisha chombo yanabaki machafu na chombo kilichokuwa kichafu kinakuwa kisafi. kitafsiri chadema kwa kuwachukua wachafu kwa mujibu wa misimamo yao ya huko nyuma ilikuwa ni kukisafisha chama tawala na wao kubaki na uchafu.

hii ilikuwa technical mistake ya hali ya juu ambayo tuliwaonya mapema kuwa lowasa anapingana na itikadi za chama hivyo kumchukua kutaua chama.

leo hii wako kimya maana wanashindwa pa kuanzia kwa kuwa sera zilizowafikisha hapo walipo walizitibua na wanashindwa waanzie wapi. chama tawala sasa kinatumbua majipu ndio kabisa wanakosa pa kuanzia kwa maana wengi wanadhani upinzani ni kupinga serikali iliyoko madarakani.

ili kufufua chama kwanza inabidi kukisafisha chama na kila mtu abebe mzigo wake na sio chama kubeba mizigo ya watu.

pili siasa za sasa ni kutafuta kuwa upande wa wananchi na sio kupinga serikali au kusapoti.

Kinachoonekana kwa CHADEMA kwa sasa ni maamuzi ambayo yanakiua chama taratibu.

Tujikumbushe uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais kwa chadema ambae baadae alikuja kuwa mwakilishi wa tiketi ya ukawa.

maamuzi yalifahamika kama kubadili gia angani. Kumtosa mfia chama na mpiganaji wa muda mrefu dr. Slaa ilikua dhihaka kwa wapambanaji wengi. Maamuzi haya hayakuwafurahisha wengi.

Hivi majuzi tena tukasikia kauli nyingine tena akiahidi kuwaletea wanaCHADEMA katibu mkuu makini.

Kilichotokea kinafahamika; uteuzi haukushawisi wana CHADEMA asili wanaona wamesalitiwa.

Mifano hiyo miwili ni katika kuonesha tu ni kwa namna gani maamuzi ya mwenyekiti yamekuwa yakikigharimu chama.

Inaweza isionekane kwa haraka ila kinachotokea ni mipasuko kila baada ya maamuzi flani toka ngazi za juu.

Wahusika watalipinga hili lakini ukweli lazima usemwe kuwa; maamuzi hayo na mengine kama hayo taratibu yana kipumzisha CHADEMA.
 
Sasa mbona kinawauma sana Ninyi CCM kuliko Sisi wana CHADEMA

Poleni sana....Tunawafahamu vizuri...Na hamtuhangaishi
 
Kimsingi chadema walicheza kamali kumchukua lowasa.

ni sawa na mfanyabiashara anayekuwa anafanya kazi kwa kuvuja jasho jingi lakini anapata mafanikio ghafla ikatokea kamali ambayo unacheza kwa fedha nyingi na ukibahatisha unakuwa tajiri mkubwa. mfanya biashara huyu akachukua mtaji wote akaweka kwenye kamali ili akibahatisha awe bilionea lakini akikosa anakuwa masikini maana mtaji umepotea.

chadema wana kazi kubwa kujenga tena misingi ya chama maana waliibomoa kwa kuwakumbatia watu ambao kwa itikadi zao walikuwa ni watu waliionekana kukwamisha nchi na wao huko nyuma wakionekana ndio wanaoweza kuwa wakombozi wa kweli kwa wananchi.

mtihani wa kupata madaraka katika uchaguzi wa mwaka 2015 umewafunua ukweli kuwa hawa walikuwa watu wanaopiga kelele kupata madaraka tu na wakiyapata wanaweza kufanya yale yale.

walijisema kuwa wao wanasafisha wachafu na kuwa wasafi wakasahau kuwa maji yakisafisha chombo mwisho wake ni maji yaliyosafisha chombo yanabaki machafu na chombo kilichokuwa kichafu kinakuwa kisafi. kitafsiri chadema kwa kuwachukua wachafu kwa mujibu wa misimamo yao ya huko nyuma ilikuwa ni kukisafisha chama tawala na wao kubaki na uchafu.

hii ilikuwa technical mistake ya hali ya juu ambayo tuliwaonya mapema kuwa lowasa anapingana na itikadi za chama hivyo kumchukua kutaua chama.

leo hii wako kimya maana wanashindwa pa kuanzia kwa kuwa sera zilizowafikisha hapo walipo walizitibua na wanashindwa waanzie wapi. chama tawala sasa kinatumbua majipu ndio kabisa wanakosa pa kuanzia kwa maana wengi wanadhani upinzani ni kupinga serikali iliyoko madarakani.

ili kufufua chama kwanza inabidi kukisafisha chama na kila mtu abebe mzigo wake na sio chama kubeba mizigo ya watu.

pili siasa za sasa ni kutafuta kuwa upande wa wananchi na sio kupinga serikali au kusapoti.
Kwani CDM tulishindwa Ktk uchaguzi? Wenyewe walisema hawatokabidhi Nchi kwa vikaratasi.. Issue sio MTU, issue Ni kwamba CCM hamtaki Upinzani..! Kwahiyo acheni kupotosha humu, tutibu source sio impact.
 
Kwani shida yako ni Nini???? Si ufurahi sasa chama unachokipinga kila siku kikifa
 
Back
Top Bottom