mwekundu
JF-Expert Member
- Mar 4, 2013
- 22,476
- 21,046
Ametokea kwetu Kilimanjaro yuleMpe tu hata Ukatibu wa familia yako Mkuu!
Ametokea kwetu Kilimanjaro yuleMpe tu hata Ukatibu wa familia yako Mkuu!
wale ambao sio maslahi wapo wengi; ambao hawapendezwi na maamuzi ya Mbowe lakini hawana pa kusema. Nawasaidia kutoa nyongo zao.
Kwani CDM tulishindwa Ktk uchaguzi? Wenyewe walisema hawatokabidhi Nchi kwa vikaratasi.. Issue sio MTU, issue Ni kwamba CCM hamtaki Upinzani..! Kwahiyo acheni kupotosha humu, tutibu source sio impact.
Nenda kawahutubie wenzio lumumba furaha yenu hiyo. Pia Dr Slaa sasa mnae kabisa baada ya kumlipia madeni yake. Mpeni ukatibu Mkuu badala ya Ndovu lager master. Nadhani itamsaidia na kuwafanya muache kutafuta book saba kwa hoja zilezile mufilisi kilasiku.Wacha Mbowe aiyumbishe CHADEMA maana ndio tunachotaka sisi CCM. Hatutaki kabisa kuiona CHADEMA iliyo imara
Ungejuwa.........Nenda kawahutubie wenzio lumumba furaha yenu hiyo. Pia Dr Slaa sasa mnae kabisa baada ya kumlipia madeni yake. Mpeni ukatibu Mkuu badala ya Ndovu lager master. Nadhani itamsaidia na kuwafanya muache kutafuta book saba kwa hoja zilezile mufilisi kilasiku.
Ukabila tena???Ametokea kwetu Kilimanjaro yule
Tunataka siasa za facts na sio siasa za ushabiki. nasema hivyo kwa kuwa shabiki siku zote hatumii akili yake kuchambua mambo maana kile anachokishabikia kitakuwa kizuri haijalishi ni kibaya kiasi gani na kile asichokishabikia kitakuwa kibaya haijalishi ni kizuri kiasi gani.
jaribuni kutathmini kwa kina maana ukisema mlishinda kwa grounds zipi? kwa maana unahitaji kuangalia taifa na sio kufocus marafiki zako na ukaona wote wanaongea lugha moja na wewe alafu ukasema nitashinda au nilishinda.
pili kwa rekodi yenu ya kusema hiki ni kibaya na kesho mkasema ni kizuri inaondoa utamu katika hoja yoyote mtayoibua ya kusema tumeonewa kwa maana jamii inaweza kudhani hiyo ni hulka ya yoyote utakayempa madaraka. mfano mkitaka kuchagua viongozi wenu kama wenyeviti tunasikia habari zilezile mnazolalamikia ndizo mnafanyiana sasa kwako unasema hiyo ndio siasa kwa mwingine unasema hatakiwi kufanya vile?????
tafuteni hoja za kubeba chama na mnachokisahau ni kuwa huko nyuma chama kilivyokuwa kichanga walikuwa wanaingia watu wenye vipaji vya siasa na ndio hao walikuwa wanabeba chama na kinakua. lakini sasa chama kinaonekana kama kinaweza kuwa alternative ya kupatia madaraka yenye maslahi manono hivyo walafi wasiojua siasa nao wanakimbilia humo wakifanya siasa zinazowakasirisha wananchi.
bila kuwa makini chama kinaweza kudumaa.
LOWASA fisadi to Urais
Hivi Daudi si Alimkosea sana Mungu ? Mungu hakumsamehe? Unamjua Sauli? Unajua Kama huyu Ndio alikuja Kua Paulo mwandishi wa vitabu vingi kuliko wote? Ikiwa Mungu anapima Na Kukubali baadhi ya Sababu wewe wa Udongo unakipi cha kujivunia kumtupia mwenzio Jiwe? Mangapi unawakosea wanaokuzunguka Ila mpaka Leo wanacheka Na wewe tu! Ni wajinga? Au unafikiri siasa Ni Nje ya Maisha yetu ya kawaida?
UCHAGUZI
Kuhusu kushinda Uchaguzi Chukua tu mfano Mdogo, hapo ulipo tafuta watu 10, Uliza walimpigia Nani kura December halafu utajua maoni Yao yakoje! Ukiona hao hawatoshi Fanya zoezi Hilo wiki Nzima kwa sehemu tofauti tofauti Mwisho Kabisa wapigie simu Rafiki Zako wote unaowajua usikie walimpa Nani kura Yao then njoo hapa!
USHABIKI;
Wewe mwenyewe hapo unazungumza kishabiki, nikuulize tu, Bunge la kina Msekwa Ni Sawa Na la kina Sita Na Makinda? Huoni mchango wa Upinzani katika maendeleo ya Tanzania? Siku zote mtu hupigania kile kilichopimwa Na utashi wake! Wewe Kama unaona Upinzani Ushabiki wao Ni wa kindaki ndaki Na wewe Kua Mndaki ndaki huko utawalani.. Mwisho wa siku wote tutakufa tu !
Wewe huna Dini? Unafikiri kila anaezungumzia siasa humu JF anauchu wa madaraka Kama wako? Hizo rasimali kupitia CCM unanufaika nazo Vipi? Huyo Lowasa Mbona mpaka Leo hamjampeleka Mahakamani?Nilisema siasa leo hii zinaingiliwa na watu wasiofaa kuwa wanasiasa kwa kuangalia uchochoro wa kujitajirisha kupitia mali za wananchi.
hakika kwa mawazo yako sijui kama hata unafaa kuongoza hata mtaa tu lakini watu wenye mawazo kama ya kwako ndio wanaamini wataikomboa afrika kutoka katika umasikini.
hakika afrika ni bara tajiri kuliko mabara mengine yote kwa rasilimali za asili lakini ni masikini watu wake ni masikini kuliko wanadamu wote tukiangalia wastani wa umasikini kutokana na kukumbatia ujinga huu wa kusema daudi alimkosea mungu, sauli alifanya mangapi? na matokeo yake ni jamii hizi zinaendelea kukumbatia ujinga kuwapa watu wanaochukua rushwa kugawa rasilimali zao kuwa ndio wasimamizi wa rasilimali zao.
mtu anayejua maana ya uongozi ni nini na maendeleo ni kitu gani hawezi kutoa kauli kama zako za sauli na daudi. sijui tuwaiteje watu wanaoweza kuchanga fedha ili wafanye jambo la maana alafu wakachukua michango yao na kumpa mtu mwenye historia ya kutafuna michango ya watu huko nyuma na kuibuka na misemo ya mungu anasamehe eti wewe kutokusamehe ni nani?
umasikini wa kwanza ni ujinga maana mjinga pekee ndiye anayeweza kuwa na duka, muuza duka akamuibia na akabaini, wakajitokeza watu kuomba kumuuzia duka wenye historia za uaminifu na uchapa kazi alafu pamoja na yule aliyemuibia eti akasema sauli alifanya mangapi na mungu akamsamehe hivyo duka amkabidhi mwizi.
vyama vya siasa kufilisika ni pale vinapoanza kuhalalisha uovu kwenye jamii na kushawishi jamii kuona kuwaibia ni jambo la kawaida na waendelee kuwapa uongozi watu ambao wanawakwamisha kimaendeleo. vyama hivi vinakuwa vinaamini vyama vya siasa vinabebwa na watu hivyo kugangania majina fulani wakidhani ndio watabeba vyama vyao.
kazi ya vyama vya siasa ni kuwa taasisi za kuibua vipaji vya kupeleka taifa mbele. nadhani tunatakiwa kufike hatua chama cha siasa kinachopaza sauti kutetea maovu kwenye jamii kifutiwe usajili, chama cha siasa kikisiamama kupinga jambo lenye faida katika jamii kwa mantiki ya kutaka kukwamisha eti ili kesho aliyeshika madaraka aonekane hajafanya lolote kifutwe kwa chama chenye lengo la kuleta maendeleo katika jamii hakiwezi kutafuta mbinu chafu kukwamisha maendeleo katika jamii.
mimi nadhani nyinyi mliomsamehe lowasa mpeni rasilimali zenu asimamie.
Inachukua muda sana kwa chama kupata umaarufu na kukubalika kwa wananchi. Wengi tulidhani act ingepata wabunge wengi sana lakini mambo yakawa tofauti kabisa na kumuacha zito mwenyewe.Wanachomwogopa Mbowe, ni kwamba CHADEMA ni kama NGO yake kupitia kwa mkwe wake Matei kwa hiyo watu wanabaki kusononeka tu moyoni lakini hakuna namna. Pengine njia pekee wamwachie chama waende hata kwa zzk au waunde chama chao.
Kinachoonekana kwa CHADEMA kwa sasa ni maamuzi ambayo yanakiua chama taratibu.
Tujikumbushe uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais kwa chadema ambae baadae alikuja kuwa mwakilishi wa tiketi ya ukawa.
maamuzi yalifahamika kama kubadili gia angani. Kumtosa mfia chama na mpiganaji wa muda mrefu dr. Slaa ilikua dhihaka kwa wapambanaji wengi. Maamuzi haya hayakuwafurahisha wengi.
Hivi majuzi tena tukasikia kauli nyingine tena akiahidi kuwaletea wanaCHADEMA katibu mkuu makini.
Kilichotokea kinafahamika; uteuzi haukushawisi wana CHADEMA asili wanaona wamesalitiwa.
Mifano hiyo miwili ni katika kuonesha tu ni kwa namna gani maamuzi ya mwenyekiti yamekuwa yakikigharimu chama.
Inaweza isionekane kwa haraka ila kinachotokea ni mipasuko kila baada ya maamuzi flani toka ngazi za juu.
Wahusika watalipinga hili lakini ukweli lazima usemwe kuwa; maamuzi hayo na mengine kama hayo taratibu yana kipumzisha CHADEMA.
Wewe huna Dini? Unafikiri kila anaezungumzia siasa humu JF anauchu wa madaraka Kama wako? Hizo rasimali kupitia CCM unanufaika nazo Vipi? Huyo Lowasa Mbona mpaka Leo hamjampeleka Mahakamani?
Kura zipi unazungumzia Mkuu? Hivi nyinyi mnaheshimu Kura Kweli? Ongea mengine sio Kura! Kwanini iharibike Kura ya Rais tu? Ktk kituo hicho hicho ambacho kwa wengine Ni halali?hakuna mwananchi mwema mwenye machungu na nchi yake anaweza kuingia jamii forum kushawishi jamii iache kutumia nguvu ya kura kudhibiti mali na utu wao.
ni yule tu anayetegemea kunufaika na hizo mbegu haramu anazopanda kwenye vichwa vya watu anaweza kufanya hivyo.
mimi nakushangaa kwa sababu unashindwa kubaini kuwa siasa ziko dynamic na sio static.
kabla ya awamu ya tano kuingia madarakani, kiukweli viongozi walikuwa wanatetea hadharani maovu wanayotendewa wananchi. hii ilitishia uhai wa chama na ikawa inavipa vyama vya upinzani nguvu kwa sababu walipinga maovu hayo.
enzi hizo ukisema ccm kwa maana ya jina la mbaya hukuhitaji maelezo na wananchi walikuelewa.
sasa wapinzani wengi wao walidhani hoja na kupinga ccm tu. sasa leo ccm imebadilika kwa kuwa na safu mpya ya viongozi wa serikali wapinzani mnachukua side ya kutetea maovu??????
hivi kweli mko serious?
mimi kama mwananchi ninanufaika pale viongozi tunaowakabidhi mali zetu wanapozitumia kutuletea maendeleo.
tunataka kodi ikusanywe itumike kutuletea maendeleo na sio wakusanya kodi watajirike kupitia kukusanya kodi na fedha serikalini haingii, tunataka nchi yetu rasilimali kama madini yavunwe kwa mikataba ya haki na tanzania ikipata mgao wake na sio viongozi wachache tuliowapa dhamana kuchukua rushwa kwenye makampuni ya madini na kusaini mikataba ambayo nchi inagawa madini badala ya kuuza. tunataka kodi zinapokusanywa sio wenye dhamana kuchukua ten percent kutoka kwa wazabuni na kutupandishia gharama za manunuzi, majengo tunaishia kujenga kwa gharama mara mbili ya gharama halisi, hivyo hivyo miradi yote ya maendeleo. na huo mchezo wa kuchukua rushwa ndio ufisadi na ni mzizi mkubwa wa umasikini wa wananchi wa kawaida na ni chimbuko la watumishi wa umma matajiri.
sasa nyie msiojua siasa haya ndiyo mnafanya itikadi zenu kwa leo????? kusema wala rushwa wasamehewe na warudishwe kwenye uongozi????
serikali inajaribu kurudisha nidhamu na ninyi mnachukua anayewajibishwa na kutaka kuendelea kutetea maovu mfano kuna mtu mmoja alikuwa mkubwa kinondoni alipokumbwa na upepo huu mkaanza kujaribu kutaka kumtetea.
haya maswali ya fulani mbona hamjampeleka mahakamani kawaeleze watu wa vijijini watakuelewa lakini sio mtu anayefahamu michezo michafu inayochezwa na viongozi ambayo kisheria wengi hawaachi "loose ends" za kuwatia hatiani kisheria.
unaweza kuwa na biashara ambayo mtu umempa madaraka ya kununua na kuuza na yeye akawa ananunua na kuuza na faida akiweka mfukoni mwake na ukalijua hilo lakini ukashindwa kumpeleka mahakamani kwa kuwa hakuna ushahidi wa kuonyesha ulipata faida hiyo na yeye akaichukua. mtu kama huyu dawa yake ni kumtimua utafute watu waaminifu. kura kwa wananchi zinaweza kutumika kwa staili hii.
Kura zipi unazungumzia Mkuu? Hivi nyinyi mnaheshimu Kura Kweli? Ongea mengine sio Kura! Kwanini iharibike Kura ya Rais tu? Ktk kituo hicho hicho ambacho kwa wengine Ni halali?
Sasa uchaguzi gani ambao mnafanya wenyewe tu tena bila usimamizi wowote wa kimataifa Na kitaifa? Mmeforce kuweka majina ya wagombea mtaforce Na mawakala?
Kama Unataka MABADILIKO Kweli ya kiutawala kwanza tubadilj Katiba halafu tuiheshimu, tusiwe Na double standards Ktk utekelezaje wa katiba hiyo, tuache Mlio wa Kuku Na Bundi iwe Na tafsiri moja Ktk fikra zetu!
Hivi Ni Kweli sisi wa kuzidiwa hata Na Rwanda tu? Miaka yote ya uhuru hiyo tunajivunia barabara Na uwanja wa Mpira tu Kweli? Hebu tutoe fikra zetu Ktk fungate la uhuru tuiheshimu misingi ya utawala kwa mujibu wa katiba!
Huu uozo uliopo wote si Ndio umetengenezwa Na Chama hicho hicho? Kilichopo kwa Sasa Ni Pombe ile ile Ktk chupa mpya!
Mwisho Kabisa Kama Upinzani haufai basi tuufute Kabisa Ktk Nchi yetu, tukibalieni Kua Ni nchi ya Chama kimoja Hakuna atakaewasumbua tena! Tutaheshimu makubaliano yetu! Ila kujidai Kua Ni Nchi ya vyama vingi Wakati sio inakwaza sana,! Hivi unafikiri kina Hitler Na Benito Mussolini + Ndui Iddy walikua wanajiona wao Ni dictators?
Hujajibu hata swali moja kati ya niliyokuuliza Mkuu! Stick with the topic please!wewe una tatizo tena kubwa kwa maana unayoyaongea mtu akikuangalia chini mpaka juu anakushangaa.
hivi wewe unayesema mafisadi wasamehewe maana daudi alifanya mangapi, sauli alifanya mangapi ndio wa kusema uwanja wa mpira tu na barabara.
kuna watu kutafuta ajira alafu wanatunga ngonjera wasizozijua na kuimba huku hajui sababu ya sisi kuwa masikini ingawa tuna rasilimali nyingi na hana mpango wowote on paper wa kuleta mabadiliko bali yeye anadhani mabadilko ni kubadili majina ya vyama, kubadili rangi za bendera, kubadili vitu visivyo na impact katika maisha ya watu na kutegemea mabadiliko katika maisha ya watu!!!!!!!
una maana gani kusema kubadili chupa wakati mvinyo ule ule kwa maana kama mgejua maana ya msemo huu ukawa msingefanya mlichokifanya katika uteuzi wa mgombea wa uraisi.
vyama vya upinzani ni muhimu sana lakini yaonekana umuhimu wa upinzani kwa wananchi na mtizamo wako wa upinzani vinakinzana.
mwananchi anahitaji upinzani wa kuleta ushindani katika siasa na mwisho wake ni mwananchi kupata faida zaidi kupitia siasa bila kujali ni nani amechukua uongozi kwa wakati gani bali daima yule ambaye anakuja na best solutions za matatizo ya wananchi wakati wa kampeni ndiye wananchi watampa uongozi.
sasa kikwazo hapa ndugu yangu ni ujinga kwa wananchi ambao hauishii kwa wananchi tu bali kwa kuwa na wanasiasa wamo katika kundi hilo ujinga huu unatambaa mpaka ndani ya vyama vya siasa.
maana ya siasa za upinzani inapotoshwa na watu wanataka kutumia ujinga wa wananchi kuwapora wananchi ama madaraka au mali.
mimi kama mwananchi wa kawaida najaribu kuangalia vyama vyote vya siasa na kujaribu kuangalia mfano nafasi ya uenyekiti. katika vyama vyote ni chama gani nafasi ya mwenyekiti au nafasi nyeti za maamuzi ziko huru ndani ya chama kugombaniwa na watanzania wote. kugombaniwa na watanzania wote hakuna chama cha hivyo bali vyama vyote vimehodhiwa.
unakuta chama kimepata usajili kwa kusema ni cha watanzania lakini kimehodhiwa na mtu mmoja au familia moja alafu kinapiga kelele kuwa kundi fulani limehodhi serikali.???? hivi mtu kama huyu jamii inafaa kumsikiliza kwa maana anapigania umma au anajipigania mwenyewe na akipewa madaraka ni mbaya zaidi kwa maana uongozi wote wa nchi atauhodhi mwenyewe?
upinzani wenye itikadi za mafisadi kusafishwa kwenye majukwaa na kupewa madaraka ni bora kutokuwa na upinzani kabisa. Faida za upinzani hazipatikani kwa kuwa na upinzani tu hata kama unaleta itikadi za kubomoa taifa bali faida za upinzani zinapatikana kwa kuwa upinzani unaokuja na hoja mbadala za kujenga taifa.
Hujajibu hata swali moja kati ya niliyokuuliza Mkuu! Stick with the topic please!
Mimi hapa.CHADEMA asili ndio kina nani hao?
Yaani umeongea point sana kwa hoja Zako, Ila sikukuuliza hayo Mkuu!maswali yako yana wigo mdogo na maswali uliyouliza yanaonyesha unavyojaribu kudhani maswali magumu yana majibu mepesi.
nimekupa majibu ya advanced unayoyahitaji kuyajua na sio unayoyajua unayoyalenga katika maswali yako.