Maamuzi ya Kawaida alafu unayaita Magumu!

MOD..Please usiunganishe post yangu....

Nipo kimya nikitafakari ni nini hasa kinachoendelea ndani ya Chama changu au Chetu kwa wale walio na fikra kama zangu, Mara huyu kavuliwa uanachama kama sehemu kubwa ya jinamizi la Chama.

Baada ya kukaa kimya nikitafakari sana, Nimegundua kuwa Chama kina watu wenye njaa uroho na uchu wa kuitwa viongozi ambao hawajakiri kukitetea chama kwa Shida na kwa Raha mpaka pale kifo kitakapotenganisha.

Sioni sababu ya Mifano kwani yeyote mwenye kujua maana ya siasa anaona nini kinachofanyika ndani ya Chadema,
Wakati mwingine nagundua kuwa si rahisi kwa Chama kama CCM kuamua kuwatemesha watu walio na majina makubwa ndani ya chama na ambao tayari wanakifanya chama chao au lichama leo linuke kwa rushwa, ufisadi na mengine.

Maamuzi magumu huya yana uchungu lakini maadamu kwenye ngano nako kuna magugu huota mithili ya ngano, hekima inaacha kuota pamoja na mazao yanapoanza unajua kilicho chema ni kipi na kilicho kibaya unaking'a na kukipiga moto maana hakifai hata utawala wa Ardhini.

Hili naliweka mbele kabisa kukipa hongera chama cha Chadema na natembea kifua mbele maana ndiyo ukweli halisi na wala hakina ukabila wala udini, Vipimo vya ukabila na udini, wabunge kila kona ya nchi wameenea na nchi nzima wapo wafuasi wa chadema.

Nawaomba kama kweli chadema hakiwaumi nyinyi msiopenda post kama hizi acheni walio wafuasi hai wa Chama chetu wa comment.

Aluta kontinyua.
 
Maamuzi magumu huya yana uchungu lakini maadamu kwenye ngano nako kuna magugu huota mithili ya ngano, hekima inaacha kuota pamoja na mazao yanapoanza unajua kilicho chema ni kipi na kilicho kibaya unaking'a na kukipiga moto maana hakifai hata utawala wa Ardhini.

Hili naliweka mbele kabisa kukipa hongera chama cha Chadema na natembea kifua mbele maana ndiyo ukweli halisi na wala hakina ukabila wala udini, Vipimo vya ukabila na udini, wabunge kila kona ya nchi wameenea na nchi nzima wapo wafuasi wa chadema.

Aluta kontinyua.
Kwanza Concept ya kuacha magugu na Ngano kuota pamoja ni concept inayohamasisha tolerance. Kustahimiliana na kuvumiliana hata pale tunapokuwa na utofauti wa Hoja na mitazamo. Wanachama wa CHADEMA kama Chama wanaunganiswa na ITIKADI na IMANI na MISINGI ya chama chao. Lakini wanaweza kuwa na approach mbali mbali kuweza kufikia malengo waliyojiwekea. Kwamfano Mh. Lema akapenda kutumia njia ya confrotation na Maandamano while Mh. Zitto akataka njia ya non Violence na dialogue zaidi. Mh. Lema akataka watu wanaoonekana kama vile ni vikwazo kufikia malengo wakashughurikiwa mara moja aidha kwa kupewa adhabu kali au kutupwa nje ya Chama wakati Zitto akataka watu kama hao waelimishwe, wapewe support ili waweze kuelewa wapi tunataka kwenda na baadaye washawishiwe kwa hoja kubadili njia yao. Hii ndio Filosofi ya kuacha magugu na ngano kuota pamoja. Sasa Ndani ya CHADEMA hii filosofi imeheshimika???

Pili ni yapi tutayaita maamuzi magumu na yapi tutayaita maamuzi ya HOVYO???? Labda nipe mifano ya maamuzi magumu na ya busara ambayo tunaweza kusema CHADEMA imefanya na hayaangukii katika category ya maamuzi Ya Hovyo?
 
by Mkuu mimi naamini zzk vyovyote vile itakavyofanyika yeye atapenda kuwa opposite kwa malengo yake mwenyewe ... anapenda zaidi kushine yeye mwenyewe kuliko cham ... Self Glory Seeker!

Nikichukuliwa kuwa uko sahihi kwa hiki unachosema, Je, ikitokea hivyo kuwa tofauti na wenzie walio naye ndani ya chama wakashindwa kumvumilia kwasababu ya utofauti wa mawazo na approach watakuwa sahihi?
 
kwanza concept ya kuacha magugu na ngano kuota pamoja ni concept inayohamasisha tolerance. Kustahimiliana na kuvumiliana hata pale tunapokuwa na utofauti wa hoja na mitazamo. Wanachama wa chadema kama chama wanaunganiswa na itikadi na imani na misingi ya chama chao. Lakini wanaweza kuwa na approach mbali mbali kuweza kufikia malengo waliyojiwekea. Kwamfano mh. Lema akapenda kutumia njia ya confrotation na maandamano while mh. Zitto akataka njia ya non violence na dialogue zaidi. Mh. Lema akataka watu wanaoonekana kama vile ni vikwazo kufikia malengo wakashughurikiwa mara moja aidha kwa kupewa adhabu kali au kutupwa nje ya chama wakati zitto akataka watu kama hao waelimishwe, wapewe support ili waweze kuelewa wapi tunataka kwenda na baadaye washawishiwe kwa hoja kubadili njia yao. Hii ndio filosofi ya kuacha magugu na ngano kuota pamoja. Sasa ndani ya chadema hii filosofi imeheshimika???

Pili ni yapi tutayaita maamuzi magumu na yapi tutayaita maamuzi ya hovyo???? Labda nipe mifano ya maamuzi magumu na ya busara ambayo tunaweza kusema chadema imefanya na hayaangukii katika category ya maamuzi ya hovyo?

kama unataka kuvuna ngano huwezi kuichanganya na magugu , na huwezi kuleta mabadiliko ndani ya taasisi yoyote kwa kutumia njia haramu ( maana kuna ushahidi kwamba wametumwa na wamelipwa ili kuvuruga ) , hatuwezi kuwavumilia hata kama ni maarufu , na hayo ndiyo yanayoitwa maamuzi magumu na wala huwezi kuyaita ya hovyo .
 
Fanyeni hivyo na CCM, nafasi ya Mwenyekiti iwe huru kwa mtu yeyote tuone,

Nimekeleka sana juu ya maamuzi ya Kawaida yaliyofanywa na CDM alafu watu wenye Mahaba na chama hiko Wanaita Maamuzi MAGUMU,tena wengine wanaenda mbali na kusema CCM iige Chadema(hili ndo limenikera kama mwanachama wa CCM)naangalia kilichofanywa CDM sioni UGUMU wake kwa hizo nafasi,eti CCM tujifunze kwa Chadema!!!!

Tujifunze nini hapo au siasa za majungu na za eneo moja,ulishawai kuona mbunge wa CCM anamtuhumu kiongozi wake katika CHAMA kupitia Mitandao,nawaambia mlichofanya ni kitu kidogo sana,labda uchanga wenu katika siasa mnaona ni maamuzi magumu....

CCM ndani ya miaka nane tumebadili makatibu wakuu CCM mara tatu,Makamba,Mukama,Kinana,sina uhakika kama tutafika nae mwisho,na haikugombanisha chama,wala majungu,au kuvuana nguo katika mitandao.Tumebadili manaibu mara tatu:Jakamwambi,Chiligati,Mwiguru,na hakuna aliekashiwa mpaka sasa.Je siku mkimtoa Silaa mtaita maumuzi gani?

Chadema kama kweli wanapenda kufanya maamuzi magumu,basi kipengere cha ukomo kirudi katika katiba yenu,pili mfanye uchaguzi mkuu wa chama,nafasi ya uenyekiti iwe huru kwa yoyote kugombea,mtangaze adharani mapato na matumizi ya fedha zote na zile za account maalum ya uchaguzi

#Ex CHADEMA simper aliquid novi#
 
Kwenye ile Taarifa ya siri, jamaa (ZZK) kavuta kama $2,000,000/=, lazima roho iwaume CCM/TISS
 
Kwa mtazamo wangu mimi ni kuwa ikiwa hivyo ndivyo,bora aondoke tu maana hataweza kufanikisha anachotaka hata kama kiko sahihi,support ya wengine ni muhimu na team work is better than individual
 
Kwa mtazamo wangu mimi ni kuwa ikiwa hivyo ndivyo,bora aondoke tu maana hataweza kufanikisha anachotaka hata kama kiko sahihi,support ya wengine ni muhimu na team work is better than individual
 
kama unataka kuvuna ngano huwezi kuichanganya na magugu , na huwezi kuleta mabadiliko ndani ya taasisi yoyote kwa kutumia njia haramu ( maana kuna ushahidi kwamba wametumwa na wamelipwa ili kuvuruga ) , hatuwezi kuwavumilia hata kama ni maarufu , na hayo ndiyo yanayoitwa maamuzi magumu na wala huwezi kuyaita ya hovyo .
  1. Hukubaliani na Mleta Mada?
  2. Kwa mfano kama uchaguzi utakuwa mwezi february, na mimi nikakuambia wewe mshikaji wangu bwana nina mpango wa kugombea Uchaguzi mwezi February naomba uniunge mkono na unichague pindi nitakapokuwa nimegombea, Je hayo mabadiriko ninayotaka kuleta yatakuwa haramu ay halali?
  3. Kama kuna ushahidi kwanini tunaogopa kuupeleka kwenye vikao vya juu (Kubali rufaa ya mwanachama maana ni haki yake, na ushahidi ukatolewe kwenye vikao vya juu)
 
Nikichukuliwa kuwa uko sahihi kwa hiki unachosema, Je, ikitokea hivyo kuwa tofauti na wenzie walio naye ndani ya chama wakashindwa kumvumilia kwasababu ya utofauti wa mawazo na approach watakuwa sahihi?

kwanini alisubiri alipwe kwanza ? Kwanini asifanye hivyo kwa utashi wake ?
 
kwanini alisubiri alipwe kwanza ? Kwanini asifanye hivyo kwa utashi wake ?
Kiongozi unaonaje ungekuwa unajibu kwanza swali uliloulizwa kabla hujatoa swali lako. Hajawahi kulipwa na hakuna Ushahidi wa kuonyesha kuwa amewahi kulipwa pesa za mafisadi. Kwa hiyo Mambo yote anayofanya ni kwa Utashi wake.
 
  1. hukubaliani na mleta mada?
  2. kwa mfano kama uchaguzi utakuwa mwezi february, na mimi nikakuambia wewe mshikaji wangu bwana nina mpango wa kugombea uchaguzi mwezi february naomba uniunge mkono na unichague pindi nitakapokuwa nimegombea, je hayo mabadiriko ninayotaka kuleta yatakuwa haramu ay halali?
  3. kama kuna ushahidi kwanini tunaogopa kuupeleka kwenye vikao vya juu (kubali rufaa ya mwanachama maana ni haki yake, na ushahidi ukatolewe kwenye vikao vya juu)

nitajibu namba 3 tu , hakuna anayeogopa vikao vya juu , tumeanza na kamati kuu na maamuzi yake umeyaona , tutaenda kwenye baraza kuu ambalo nakuhakikishia litabariki maamuzi ya kamati kuu .
 
Kiongozi unaonaje ungekuwa unajibu kwanza swali uliloulizwa kabla hujatoa swali lako. Hajawahi kulipwa na hakuna Ushahidi wa kuonyesha kuwa amewahi kulipwa pesa za mafisadi. Kwa hiyo Mambo yote anayofanya ni kwa Utashi wake.

nimejiridhisha kwamba hakuna unachokijua .
 
nitajibu namba 3 tu , hakuna anayeogopa vikao vya juu , tumeanza na kamati kuu na maamuzi yake umeyaona , tutaenda kwenye baraza kuu ambalo nakuhakikishia litabariki maamuzi ya kamati kuu .

Je wakati mnaanza na kamati Kuu mlizingatia yafuatayo?
"Mwanachama YEYOTE hatachuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza;

a) kujulishwa kosa lake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili

b) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao husika.

c) mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa
 
nimejiridhisha kwamba hakuna unachokijua .
Mkuu mbona unakimbia hoja kirahisi namna hiyo? hata kujiridhisha kuwa mtu hana akijuacho lazima uwe na vigezo na umfahamishe huyo mtu kuwa kutokana na vigezo vifuatavyo nimejiridhisha kuwa huna Ujualo. Unaweza kunambia vigezo vya kunidisqualify? au ndio unatafuta namna ya kuingia mitini politely?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom