Maamuzi ya Kawaida alafu unayaita Magumu!

Sitakuwa najadili sana uhalali wa kuondolewa kwa Zito Kabwe au la. Nitakuwa najadili uthubutu uimara na wa chama. Wote tunakubali kuwa Zito Kabwe ni maarufu kwa watu wengi. Lakini kwamba CHADEMA wamethubutu kufanya maamuzi magumu ni jambo la kupongezwa. Suala la kaonewa au hapana hilo kila chama kina vikao vyake vya kupima uhalali au uonevu.

Chama kikubwa kama chama cha mapinduzi kimekuwa kila mara kinapiga kelele za kuchukua hatua lakini wanasuasua. Mapacha watatu walikuwa wachukuliwe hatua, mpaka leo ni kigugumizi.

Ikafika wakati wa kuvua gamba lakini gamba halitoki. Ikafika wakati wa kuwachukulia hatua walipata madaraka kwa rushwa. Hakuna kilichofanyika.

Tuhuma kila kukicha lakini hakuna hatua.

Ninasikitika kuona mtu wa CCM anathubutu kuongelea hatua ya kamati kuu.

Nawapongeza CHADEMA kwa ujasiri na uthubutu wa kutokuogopa kuchukua hatua mnayoamini ni kinyume na maadili yenu.

MNAFAA KUAMIMINIWA NA WANANCHI KUWA PAKIWEPO NA TUHUMA MTACHUKUA HATUA BILA WOGA.

CCM igeni mfano huo. Fanyeni maamuzi magumu kwa wanaoharibu sifa ya chama.

CCM hawawezi kuamua haya maana wameshikamana na wajuana katika maovu yao .It is a long chain ya wala Nchi wanaongea tu lakini they cannot act nani anaweza nmnyooshea kidole mwenzake ?
 
ccm wameshindwa kuwajibishana ndio maana wamebaki na wahimdi tu. huku arusha wamebaki nawahindi siunajua wakati wauchaguzi wanakimbilia nchi jirani .
 
nasema hivi,,,,,ndio ishakuwa mtapiga sana kelele na mkimwingiza papeti mwingine nae tunapiga chini
 
naona wamehak mtandao kila nikiwajibu hayatokei....ccm wapi nyie...afu wea is lukosi simuoni
 
HongerA chadema huu ni uamuzi tosha, Viongozi watimuliwa wAtajibeba.
 
sina imani kama ccm wanaweza kufanya maamuzi magumu kwa vigogo, labda kwa vidagaa tu kama kina mansur himid.
 
Makala katika gazeti la Raia Mwema. PAGE 23.

Badala ya kutatua tatizo la kilimo cha jembe la mkono, unalima pamoja na wananchi kwa kutumia jembe la mkono ili upige picha. Hapo bei ya sukari haijashuka na tatizo la soko la korosho halijatatuliwa.

bei ya umeme bado inapanda pamoja na kuwa na rasilimali. Miaka 52 ya Uhuru bado tunategemea Mzungu aje kuchimba kisima, kuzindua na kupiga nae picha.

Makada wa CCM wamejitoa ufahamu, hawazungumziii matatizo ya wananchi na jinsi ya kuyatatua, HAPANA. Wao wako bize kushabikia masuala ya CDM....

RAIA MWEMA PAGE 23
 
Mwananchi aliyehudhuria kituko hicho alifika kwa sababu mchele kama viroba 4 vilitangulizwa na nyama ng'ombe alichinjwa. Watu wale na kunywa fedha ya mhisani wa kisima.
Elimu ya uraia ni muhimu zaidi hata ya kujua hizo sera za vyama. Tuleteeni elimu ya uraia, haya Mafisadi tutayatoa kama kule juu ya africa walivyo fanya. Ukitamka hicho, mafisadi na Maccm tumbo linawakata.
 
Wananchi wanafaham mchawi wao,wanacheka nae ila wanamsubiri aingie king 2015 watamnyoa kwa vigae vya chupa,wait and see..
 
CCM ni chama kilicho gubikwa na madudu na uchafu mwingi huku kikishindwa angalau kujisafisha na kurejesha imani kwa wananchi, Pamoja na kwamba ni chama tawala chenye dola na kila aina ya nyenzo lakini ni chama dhaifu sana linapo kuja swala la kufanya maamuzi. Leo hii CCM haiwezi kusimama na CHADEMA kwenye mzani wa kufanya maamuzi magumu, kikithubutu kujifanya kinataka kufanya maamuzi huishia kutokujiamini na kuogopa kuchukua hatua, yaani CCM iko kama mtoto mdogo anaye ogopa kivuli chake wakati wa kwenda msalani anapo kuwa na haja.

Mtakumbuka kuwa katibu wa chama hiki amezongwa na tuhuma za meli yake kukamatwa kwa usafirisha meno ya tembo nje ya nchi kinyume na sheria, na yeye baadae akakiri, hii pekee ilipaswa kuwa fursa ya kumvua uwanachama na kumuwajibisha. Lakini kwa kuwa uwezo wa kufanya maamuzi ni mdogo mabingwa hawa wa Tanzania wa kufunika kombe wakaa kimya na kumkumbatia shujaa wao. Mnajua kuwa uwindaji haramu na kuuwawa kwa Tembo kumetia doa taifa letu, kwa nini wasinge anzia kwa Kinana?!

Ilisemwa na mpaka leo haijawahi kukanushwa kuwa CCM ilitumia pesa za EPA 2005 kumuingiza JK madarakani, pesa hizo zilikwapuliwa kwenye akaunti ya madeni ya nje na baadae ukwapuzi mkubwa ukatokea kupitia Kagoda. Pesa hizo zilikuwa za walipa kodi hazikuwa mali ya chama. Matokeo yake baadae wezi wakapigiwa magoti wakiombwa wazirejeshe. Nani mwenye msuli wa kusema hata aliyeingia madarakani kwa pesa hizo au wote walio chora ramani ya kukwapuliwa pesa hizo wawajibishwe kwa kuwaibia watanzania?

Majuzi kule Arusha kabla ya bomu kulipuliwa kwenye mkutano wa Chadema viongozi waandamizi wa ccm walitangulia kutoa kauli tata zilizo ashiria mauwaji na baadae kweli bomu na risasi zikarindimishwa na wafuasi wa Chadema kuuwawa mkutanoni. mpaka wa leo hakuna kiongozi hata mmoja wa ccm au serikali aliye laani kauli za viongozi wale au hata kuchukua uamuzi mgumu wa kuwawajibisha kwenye nafasi zao kwa kusababisha watanzania wenzao kuuwawa. Wamepiga kimya kana kwamba wanao uwawa kwenye mikutano ya vyama pinzani si watanzania. Nini kinazuia maamuzi magumu watu hawa wasiwajibishwe?

Kule Kagera CCM ilithibuti kufuata nyayo za Chadema kwa kuwafukuza madiwani wake walio enda kinyume na sera ya chama chao. madiwani walimpinga meya wao kwa ufisadi, meya akaweka msuli, ccm ikaona kuliko meya fisadi ang'oke ni bora kuwafukuza wanao mpinga. wakaja kugundua kuwa uchaguzi utaitishwa. Badala ya kumfukuza meya wakarudisha na wale madiwani walio kuwa wanampinga meya kwa ufisadi na wakapiga kimya ili upepo upite. upepo umepita hakuna maamuzi magumu. Uwezo wa kufanya maamuzi magumu uko wapi?

Mzee Kapuya kwenye SMS zake kwenda kwa kabinti alikokabaka moja ya SMS inasema ''.. Sisi ndio wenye nchi, mbona watoto wetu wanauza unga lakini hawakamatwi
..." kubaka na SMS kama ile vilipaswa kushughulikiwa mapema sana. lakini maskini ya Mungu binti akiambiwa na Katibu wa chama kuwa yale yalikuwa mambo binafsi ya Kapuya. Kwa tukio lile ilipaswa Ccm kama chama wamchukulie hatua kada wao na mwanachama wao lakini yuko wapi wa kutengeneza mkondo wa mazingira magumu ndani ya chama?

Leo hii CHADEMA inasafisha nyumba yake kwa kufanya maamuzi magumu ya kukomesha usaliti, cha kushangaza wa kwanza kulalamika ni CCM!!! Kulikoni mwenye nyumba anasafisha nyumba yake majirani walalamikie vumbi ilhali kwao kuna uchafu wenye vumbi la madawa ya kulevya, pembe za ndovu, ufisadi na kila aina ya uchafu? kwa nini wasiwaige chadema kusafisha nyumba yao? kinacho washinda kufanya maamuzi magumu ni nini?!
 
Vibaka wa buku 7 wanaokesha JF kama ZeMarcopolo Ritz na majihadist wenzake huwezi kuwaona kwenye thread kama hii.
 
Last edited by a moderator:
Mzee mtoi akili yake sijui ipoje maamuzi magumu hata kibaka anafanya hayo maamuzi ya kibaguzi na ubabe ndiuo unaita maamuzi chadema inaviongozi wa ajabu kweli kuanzia mama mpaka mtoto wake wanabaguliwa tu hicho chama chenu cha sisi kwa sisi si cha watanzania ni chenu mwisho mtakichemsha mnywee chai.
 
Vibaka wa buku 7 wanaokesha JF kama ZeMarcopolo Ritz na majihadist wenzake huwezi kuwaona kwenye thread kama hii.
Tatizo lako unaviroboto hii threat inanini mpaka watu washindwe kuichangia vijana siyo waonga kama mbowe na slaa wanavyomgwaya zitto mpka wanamfanyie vitimbi asigombee uenyekiti.
 
CCM ni chama kilicho gubikwa na madudu na uchafu mwingi huku kikishindwa angalau kujisafisha na kurejesha imani kwa wananchi, Pamoja na kwamba ni chama tawala chenye dola na kila aina ya nyenzo lakini ni chama dhaifu sana linapo kuja swala la kufanya maamuzi. Leo hii CCM haiwezi kusimama na CHADEMA kwenye mzani wa kufanya maamuzi magumu, kikithubutu kujifanya kinataka kufanya maamuzi huishia kutokujiamini na kuogopa kuchukua hatua, yaani CCM iko kama mtoto mdogo anaye ogopa kivuli chake wakati wa kwenda msalani anapo kuwa na haja.

Mtakumbuka kuwa katibu wa chama hiki amezongwa na tuhuma za meli yake kukamatwa kwa usafirisha meno ya tembo nje ya nchi kinyume na sheria, na yeye baadae akakiri, hii pekee ilipaswa kuwa fursa ya kumvua uwanachama na kumuwajibisha. Lakini kwa kuwa uwezo wa kufanya maamuzi ni mdogo mabingwa hawa wa Tanzania wa kufunika kombe wakaa kimya na kumkumbatia shujaa wao. Mnajua kuwa uwindaji haramu na kuuwawa kwa Tembo kumetia doa taifa letu, kwa nini wasinge anzia kwa Kinana?!

Ilisemwa na mpaka leo haijawahi kukanushwa kuwa CCM ilitumia pesa za EPA 2005 kumuingiza JK madarakani, pesa hizo zilikwapuliwa kwenye akaunti ya madeni ya nje na baadae ukwapuzi mkubwa ukatokea kupitia Kagoda. Pesa hizo zilikuwa za walipa kodi hazikuwa mali ya chama. Matokeo yake baadae wezi wakapigiwa magoti wakiombwa wazirejeshe. Nani mwenye msuli wa kusema hata aliyeingia madarakani kwa pesa hizo au wote walio chora ramani ya kukwapuliwa pesa hizo wawajibishwe kwa kuwaibia watanzania?

Majuzi kule Arusha kabla ya bomu kulipuliwa kwenye mkutano wa Chadema viongozi waandamizi wa ccm walitangulia kutoa kauli tata zilizo ashiria mauwaji na baadae kweli bomu na risasi zikarindimishwa na wafuasi wa Chadema kuuwawa mkutanoni. mpaka wa leo hakuna kiongozi hata mmoja wa ccm au serikali aliye laani kauli za viongozi wale au hata kuchukua uamuzi mgumu wa kuwawajibisha kwenye nafasi zao kwa kusababisha watanzania wenzao kuuwawa. Wamepiga kimya kana kwamba wanao uwawa kwenye mikutano ya vyama pinzani si watanzania. Nini kinazuia maamuzi magumu watu hawa wasiwajibishwe?

Kule Kagera CCM ilithibuti kufuata nyayo za Chadema kwa kuwafukuza madiwani wake walio enda kinyume na sera ya chama chao. madiwani walimpinga meya wao kwa ufisadi, meya akaweka msuli, ccm ikaona kuliko meya fisadi ang'oke ni bora kuwafukuza wanao mpinga. wakaja kugundua kuwa uchaguzi utaitishwa. Badala ya kumfukuza meya wakarudisha na wale madiwani walio kuwa wanampinga meya kwa ufisadi na wakapiga kimya ili upepo upite. upepo umepita hakuna maamuzi magumu. Uwezo wa kufanya maamuzi magumu uko wapi?

Mzee Kapuya kwenye SMS zake kwenda kwa kabinti alikokabaka moja ya SMS inasema ''.. Sisi ndio wenye nchi, mbona watoto wetu wanauza unga lakini hawakamatwi
..." kubaka na SMS kama ile vilipaswa kushughulikiwa mapema sana. lakini maskini ya Mungu binti akiambiwa na Katibu wa chama kuwa yale yalikuwa mambo binafsi ya Kapuya. Kwa tukio lile ilipaswa Ccm kama chama wamchukulie hatua kada wao na mwanachama wao lakini yuko wapi wa kutengeneza mkondo wa mazingira magumu ndani ya chama?

Leo hii CHADEMA inasafisha nyumba yake kwa kufanya maamuzi magumu ya kukomesha usaliti, cha kushangaza wa kwanza kulalamika ni CCM!!! Kulikoni mwenye nyumba anasafisha nyumba yake majirani walalamikie vumbi ilhali kwao kuna uchafu wenye vumbi la madawa ya kulevya, pembe za ndovu, ufisadi na kila aina ya uchafu? kwa nini wasiwaige chadema kusafisha nyumba yao? kinacho washinda kufanya maamuzi magumu ni nini?!
Naomba nipingane na wewe mchana kweupe unasema katibu wa ccm anakabiliwa na tuhuma siyo kweli katibu wa chadema ndiye anaongoza kwa tuhu na kashifa kwanza anaongoza kwa kipora wake za watu hilo liko wazi mpaka mahakamani,pili ndye anayeongoza kwa kufanya mambo ya hovyo akiwa kwenye nyumba za ibada mpaka akafukuzwa upadri.

Leo hii anachukua hela za chama ambayo ji ruzuku hela za watanzania anaenda na rafiki yake josephine ulaya na marekani kutembea hatua gani zimechukuliwa dhidi yake.

Slaa pia aliiba pesa kanisani za watoto yatima zile za msaada mpaka leo chama hakijamwazibu si hayo tu kutwa kucha anawatuma akina yericko na ben kumwinda zito kwa malengo anayojua yeye.

Ametanganza taifa liingie kwenye mgogoro wa kutotawalika lakini chama hakijafanya kitu au ulitaka dola itumie chuma cha shaba kumnyamazisha.

kabla hujasema jitazame kwanza ubaguzi utawaua kaburi lenu li tayari mtazikwa tu.
 
sina imani kama ccm wanaweza kufanya maamuzi magumu kwa vigogo, labda kwa vidagaa tu kama kina mansur himid.
Kwani himidi alikuwa kidagaa hujui kuwa alikuwa mbunge na alishawahinkuwa kuwa waziri twambie chadema wamefanya maamuzi gani zaidi ya maamuzi kibaguzi ya kumuonea zitto na wapigania demokrasia wengine narudia kusema hakuna kiongozi wa chadema au kikao chochote cha chadema kinachoweza kumfukuza zitto kumvua uongozi ilikuwa ni kutishia nyau.
 
HongerA chadema huu ni uamuzi tosha, Viongozi watimuliwa wAtajibeba.
Hakika mkuu mtapata aibu ya mwaka kwa sasa zitto hafukuziki ndani ya chadema kinachofuata sasa wanambembeleza kama mtot ili asilipuke mengi yaliyopo aibu yenu aibu yake hafukuziki.
 
Tatizo lako unaviroboto
hii threat inanini mpaka watu washindwe kuichangia vijana siyo waonga
kama mbowe na slaa wanavyomgwaya zitto mpka wanamfanyie vitimbi
asigombee uenyekiti.

Mkuu, hawa watu naona wamechanganyikiwa sasa. wanaanzisha thread kwa lengo tu la kutaka watu wajibu na si kujenga hoja
 
Mzee mtoi akili yake sijui ipoje maamuzi magumu hata kibaka anafanya hayo maamuzi ya kibaguzi na ubabe ndiuo unaita maamuzi chadema inaviongozi wa ajabu kweli kuanzia mama mpaka mtoto wake wanabaguliwa tu hicho chama chenu cha sisi kwa sisi si cha watanzania ni chenu mwisho mtakichemsha mnywee chai.

Ubaguzi unaongelea ni upi mkuu?

Zitto ni mjumbe wa kamati kuu, mama yake ni mjumbe wa kamati kuu, Zitto ndio mbunge pekee wa kutoka Kigoma ana wabunge wa viti maalumu 3, mkoa wa Kilimanjaro una wabunge 3 wa kuchahiliwa una wabunge wa viti maalum 3 upendeleo uko wapi?
 
Back
Top Bottom