Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Haki ya wabunge kuhudhuria vikao na kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao ni ya kikatiba na kanuni feki za Bunge zinazolipa Bunge mamlaka ya kuwasimamisha wabunge kutekeleza majukumu yao ya kikatiba ni kuikiuka katiba walioapa kuilinda na kuitetea!
Bunge halipo juu ya katiba na ndiyo maana huapa kabla ya kuanza shughuli za Bunge ya kuwa wataitii katiba ambayo hakuna mahali ndani ya katiba hiyo wamepewa mamlaka ya kuwasimamisha wabunge na kuwapora wananchi wanaowawakilisha haki yao ya kikatiba ya uwakilishi.
Tusipokuwa waangalifu itafikia wakati Bunge linamsimamisha Mbunge kwa miaka mitano na kuwapora wananchi wa jimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa.
Kama Mbunge kavunja kanuni Bunge linaweza kumpa faini ili aathirike Mbunge mwenyewe bila kuathiri haki ya kuwakilishwa ya wananchi wa jimbo lake.
Spika Job Ndugai kuwaadhibu askari walioheshimu haki za binadamu pia linatia aibu si kwake tu bali kwa Bunge zima na taifa kwa ujumla.
View attachment 520010View attachment 520011View attachment 520012
Ni lazima wahanga wa suala hili wawaburuze mahakama kuu Spika na AG wakajibu kwanini wanawapora wapigakura kwenye majimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa.Kwa bunge la spika huyu Mpiga bakora na naibu mrushusu matusi kutoka ccm tutegemee mambo mengi ya hovyo
Una hoja but you have a missed a point kwa kutoa conclusion.Haki ya wabunge kuhudhuria vikao na kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao ni ya kikatiba na kanuni feki za Bunge zinazolipa Bunge mamlaka ya kuwasimamisha wabunge kutekeleza majukumu yao ya kikatiba zinakiuka katiba wabunge hawa waliapa kuilinda na kuitetea Katiba husika!
Bunge halipo juu ya katiba na ndiyo maana huapa kabla ya kuanza shughuli za Bunge ya kuwa wataitii katiba ambayo hakuna mahali ndani ya katiba hiyo wamepewa mamlaka ya kuwasimamisha wabunge na kuwapora wananchi wanaowawakilisha haki yao ya kikatiba ya uwakilishi.
Tusipokuwa waangalifu itafikia wakati Bunge linamsimamisha Mbunge kwa miaka mitano na kuwapora wananchi wa jimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa.
Kama Mbunge kavunja kanuni Bunge linaweza kumpa faini ili aathirike Mbunge mwenyewe bila kuathiri haki ya kuwakilishwa ya wananchi wa jimbo lake.
Spika Job Ndugai kuwaadhibu askari walioheshimu haki za binadamu pia linatia aibu si kwake tu bali kwa Bunge zima na taifa kwa ujumla.
View attachment 520010View attachment 520011View attachment 520012
Anayekemea mapungufu ya sheria na mikataba ni mzalendo siyo mtetezi wa wezi kama wabunge wa CCM wanavyodai.Nikiangalia kwa umakini kabisa vurugu yote ya ijumaa ilipangwa kwenye vikao vya CCM ili ile bajeti ipite.!Tatizo wapinzani walidhani CCM wako pamoja nao kwenye issue za raslimali za Taifa kumbe hakuna kitu.
Inatia shaka na hasira pale wabunge 300 wa CCM wanaposhabikia mchanga aka Makinikia na kuacha minara ya dhahabu inayoporwa na hao akina Kalemani.
Ninawashangaa wanachama wa CCM wanaoona lakini wanajifanya hawaoni.Ninawashangaa wasomi wanaoambiwa ati wanaPhD kuacha huu uovu wa Ndugai ukawa kigezo cha kuzika issue nzima ya madini na mikataba mibovu halafu tunaambiwa ti Rais ana nia njema na madini,sijui lakini siyo kwa style hii
Bila kuhitimisha nitakuwa sijajitendea haki na wala wewe sijakutendea haki.Una hoja but you have a missed a point kwa kutoa conclusion.
Hoja yako umeinyima haki ya kudadavuliwa na wajuvi wa sheria na katiba kwa hoja yoyote inayokinzana na conclusion yako inaweza kuzua malumbano yasiyokuwa na tija.
BTW una nafasi ya kuirekebisha kwa kufanya editing ambayo itaifanya iwe hoja chokonozi badala ya hoja inayohukumu.
Bunge halina mamlaka ya kuwapora wananchi wa majimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa.kwa hiyo katiba imesema wavuta bangi waingie bungeni na kutukana watakavyo kisha wakenuliwe meno?
kanye urudi kitandani ulale mambo ya sheria na katiba yaache hujui kitu.Bunge halina mamlaka ya kuwapora wananchi wa majimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa.
Mvuta bangi aadhibiwe yeye binafsi bila kuathiri haki za wapigakura za kuwakilishwa
Anayekemea mapungufu ya sheria na mikataba ni mzalendo siyo mtetezi wa wezi kama wabunge wa CCM wanavyodai.
Pili, kumtafuta mchawi kwa kuunda kamati feki kama ile ya Prof. Mruma ni kukiuka mikataba ambayo imeweka kifungu cha msuluhishi kwa minajili ya kutatua migogoro.
Anayetetea ukiukwaji tajwa yeye ndiye mtetezi wa wezi wa mali za umma.
Tuwekee kipengele mahsusi cha katiba kilichovunjwa
kwa hiyo katiba imesema wavuta bangi waingie bungeni na kutukana watakavyo kisha wakenuliwe meno?
Haki ya wabunge kuhudhuria vikao na kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao ni ya kikatiba na kanuni feki za Bunge zinazolipa Bunge mamlaka ya kuwasimamisha wabunge kutekeleza majukumu yao ya kikatiba zinakiuka katiba ambayo wabunge hawa waliapa kuilinda na kuitetea Katiba husika!
Bunge halipo juu ya katiba na ndiyo maana wabunge wote huapa kabla ya kuanza shughuli za Bunge ya kuwa wataitii katiba ambayo hakuna mahali ndani ya katiba hiyo wamepewa mamlaka ya kuwasimamisha wabunge na kuwapora wananchi wanaowawakilisha haki yao ya kikatiba ya uwakilishi.
Tusipokuwa waangalifu itafikia wakati Bunge linamsimamisha Mbunge kwa miaka mitano na kuwapora wananchi wa jimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa kwa kipindi chote cha uwakilishi.
Adhabu za kikanuni za Bunge hazina mamlaka ya kupora wananchi haki zao za kikatiba kama kuwakilishwa.