Maamuzi ya baraza la mawaziri sasa ni kinga ya Mafisadi?

Ruta,
Uzi wako huu hitimisho lake ni kwamba ktk nchi yetu hakuna mtu wa kumkamata mwingine miongoni mwa vigogo. Mkapa hawezi kumtosa mtu ye yote ktk baraza lake kwa kuwa walikula wote wakati wao. Leo tukimshinikiza JK ampeleke Lowasa & co mahakamani hawezi kwa kuwa naye alikula nao sometimes some where. Vivyo hivyo, Jk hana moral authority ya kubadili Sheria na kumwajibisha Mkapa kwa sababu mkapa kwa network yake na intelligence anajua miradi yote yaliyoko mafichoni ya JK.
Suluhisho la kuondoa ufisadi Tz ni kuiondoa ccm madarakani. Full stop.
Hilo ndilo lilikuwa pia pendekezo langu jana ITV-malumbano wakati tunajadili Tz kufanya vibaya ktk olympik.
[MENTION]
Mikael P Aweda[/MENTION] ni rahisi kudhani wakiingia cdm madarakani basi ufisadi utakwisha lakini ukweli ni kuwa utazidi maradufu kama mfumo wa uzalishaji wa viongozi utaendelea huu uliopo........
 
Jueni siku zote kua mtu akitumwa akaibe na boss wake basi mwenye kosa zaidi si yule aliyeiv
ba bali ni yule aliyemtuma maana asingetumwa asingeiba.. Ndio maana mataifa ya ulaya utakuta kama umefanya kosa na ulitumwa basi FBI au MI6 wako tayari kukupunguzia adhabu ili mradi umtaje aliyekutuma so kwa hapa bongo hawa watu wanaopelekwa mahakamani ni small fish tungekua na fbi hapa wasingehangaika na hao wao wangetaka big fish wenyewe bongo hatuwezi hiyo

mtotowamjini hiyo ndiyo hoja kwa nini Mkapa na JK wake hawashitakiwa kama siyo ubabaishaji wa mfumo uliopo?
 
Last edited by a moderator:
Rutashubanyuma Ufisadi utaisha endapo mfumo mzima ilopo madarakani utaondolewa kabisa pamoja na katiba yao kiraka kwan katiba inawalinda wa haohao ndio wako madarakani hakuna kunguru ampigae kunguru mwenzio na ukiona wanapigana ujue wanacheza hao, sasa basi ni wakati wa kila mmoja mwenye kuhitaji Tanzania tukufu na si nyumba ya mafisadi anapaswa kubalika kwa kila kitu kwanza akatae katika nafsi yake kuwa anaichukia na kujiapiza ndani yake kuwa siko tayari kuona Tanzania na watanzania wake wasio na hatia wakitaabika na wachache wakifaidi neema zilizopo ndani yake, Kwa staili hii nina huakika ufisadi utakoma Tanzania tunahitaji viongozi au kiongozi mmoja mkuu ambaye atasimamia maslai ya taifa na si maslai binafsi. Watanzania muda wa kufanya mabadiriko ni sasa jamani tubadirike kwa kutumia chaguzi tuchague kiongozi na viongozi thabiti katika kusimamia maslai ya taifa letu na sio maslai yake binasfii

p_prezdaa ni kweli changamoto ni namna ipi tufanye tupate mfumo ambao utawajibika kwa raia badala ya viongozi............
 
Last edited by a moderator:
Wanajitundika kwenye maamuzi ya ikulu na Baraza la Mawaziri kwa sababu wanaelewa jambo likithibitika lilifanyiwa maamuzi kwenye ngazi hizo lazima kesi ife kwa sababu, tulipitisha sheria ya kinga kwa Rais hata baada ya kutoka madarakani, na kwamba maamuzi ya baraza la mawaziri ni matakatifu. Sina uhakika kama mtu anaweza kulipeleka baraza lote la mawaziri mahakamani.



Bunge letu pia hupitisha sheria kandamizi kwa wananchi lakini lenyewe linajiwekea kinga. Huwezi kulishitaki bunge. Wabunge pia hupitisha sheria za kodi kandamizi lakini wao hujisamehe kodi

Kwa hiyo tuanze kwenye sheria zetu, zitoe haki sawa kwa kila raia. Vinginevya huu mchezo utaendelea hadi nchi hii itaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu wananchi watakua hawana njia nyingine ya kudhibiti wizi bali kupambana. Tukifikia hapo hata hao mafisadi watakimbia nchi watatuacha tukichinjana

Gurudumu tafsiri yako ya sheria ina walakini.....................Raisi analindwa na sheria kama maamuzi yake aliyafanya kwa nia nzuri..........................sasa kuchora michoro ya wizi na ubadhirifu nia nzuri iko wapi?
 
[MENTION]
Mikael P Aweda[/MENTION] ni rahisi kudhani wakiingia cdm madarakani basi ufisadi utakwisha lakini ukweli ni kuwa utazidi maradufu kama mfumo wa uzalishaji wa viongozi utaendelea huu uliopo........

hoja yako ina mantiki,,,,je tuwe na mfumo GANI,,,,ili hata wakija CCK kusiwe na ufisadi???
 
mkuu Rutashubanyuma,

Mimi kila ninapokumbuka mchoro wa wizi katika EPA na ukweli kuwa uliratibiwa na CCM na kupewa baraka zote na mkuu mwenyewe huwa nachoka kabisa na kwa kweli ingawa mimi sipendi kuwa cynic lakini naamini kwa dhati kabisa EPA imekuwa ni pandora's box ambayo imehalalisha wizi and all kind of nasty stuff by the system.

To me EPA imekuwa ni sinema ya kweli...kilichotokea ni kitu ambacho kingepaswa kutokea kwenye movie...but the reality ni kuwa kimetokea katika maisha halisi....astonishing!

Nilisoma kuhusu the so called chess masters and the like mfano katika novel fulani ikiitwa The Almighty ikimhusu jamaa akiitwa Edward Armstead(kama sijakosea, nliisoma long time nikiwa form two back in 1992)....the link is below:

Great Books that I liked: The Almighty (published in 1982) by Irving Wallace - A power drunk man

Mkuu, wanachokifanya sasa ni kutumia hiyo kinga ya raisi ya kutoshtakiwa...so, ukishasema nlipata approval ya rais..umemaliza...hakuna kesi hapo!

Like that Zakia Meghji alisingizia usalama wa taifa katika issue ya KAGODA pale delloitte auditors walipotaka some informations na Pinda akatumia the same excuse kukataa kujibu hoja ya Zitto Kabwe bungeni last year or the year before kuhusu MEREMETA.

Honestly, sasa naamini, nothing happens in this world that is not planned!!!

Am speechless!!!
[MENTION]
Al Zagawi[/MENTION] upole wetu sasa imekuwa sumu kali kwetu..................na wa-tz tu wavivu sana.............
 
Ni kweli Ruta! Lakini katika usemi huo wa Basi Inatosha kutoka kwa WaTZ hata yeye itamuhusu kama tuhuma hizo za Epa ni kweli.
[MENTION]
Ndallo[/MENTION] bila ya kuutazama upya mfumo wa uwajibikaji ndani ya hili taifa hata hizi sensa ni kupoteza fedha bure....................................hakuna maendeleo kabisa ila ubabaishaji tu..........
 
KAMA KINACHOSEMWA NI KWELI, HAWA watu wanaotumia maamuzi ya BARAZA MAWAZIRI (BM) kujinasua wako sahihi kabisaaaaaa. KWA MUJIBU WA KATIBA, BM ni chombo cha kumshauri tu RAIS: RAIS hafungwi na maamuzi ya BM (IBARA 37). KWA lugha nyepesi maamuzi ya BM hayafungi (not bind) wana BM kwani maamuzi hayo si yao, ni ya RAIS. BM linashauri tu, RAIS ndiye anayeamua. KWA HIYO MTU PEKEE wa kushitaki kwa mujibu wa KATIBA YETU MBOVU ni RAIS siyo wajumbe wa BM: BABA LA MAFISADI MKAPA ndiye aburuzwe mahakamani.

HATA hivyo sasa, RAIS MSTAAFU hawezi kushitakiwa kwa mambo aliyofanya akitekeleza majukumu yake kama RAIS hata kama ni ufisadi. HAPA ndo umuhimu wa kuwa na KATIBA MPYA unapokuja. NASHAURI tutoe maoni kwenye TUME ya WARIOBA ya katiba ili tuepukane na tabia hii ya kubadirisha IKULU (MAHALI PATAKATIFU: JK NYERERE) kuwa pango la walanguzi na sinki la kutapikia mafisadi baada ya kunyonya damu zetu.

Tafsiri ya kama Raisi anaweza kushitakiwa au la chini ya sheria iliyopo ni tafsiri ambayo inapaswa iachiwe mahakama........................sheria inamlinda kwa maamuzi ambayo yana nia njema................sasa ufisadi huu ambao hata wao kwenye ushahidi wao wamejitia kitanzi kwanini sheria iwalinde?
 
Mkuu Rutashubanyuma Imeniuma sana kujua kuwa imekuchukua mda mrefu sana kugundua hili, Lakini nikwambie ukweli kabisa HAKUNA MTU MWENYE UELEWA MZURI ALIYEKO CCM AMBAYE ANAUCHUKIA UFISADI!. Kama alivyosema Mungu Mwenyezi juu ya SODOMA na GOMORA kuwa KAMA KUNA MWENYE HAKI MMOJA zaidi ya Rutu na familia yake, angeiponya. Lakini alikosekana. Basi na CCM ndivyo ilivyo na mbaya zaidi simuoni wakufanana na Rutu huko CCM.

Kyaiyembe ufisadi siyo ccm balki ni matunda ya mfumo mbovu ambao hata ukiwapa cdm leo watazalisha ufisadi mkubwa zaidi ya huu....................mfumo mbovu ni ule ambao hakuna uwajibikaji moja kwa moja kwa raia ambao ndiyo waathirika na ufisadi......
 
Last edited by a moderator:
Je inawezekana Rais Mstaafu Mkapa akapanda tena mahakamni kumtetea Yona na Mramba..(mawaziri wake wa zamani)...?..na jiuliza tu..?
mtu chake Mkapa ndiye ataenda kuwanasua....................wanachofanya akina YOna ni kumalumu Mkapa akija atasema yalikuwa maamuzi ya baraza la mawaziri ambapo huo ushahidi unatosha kumfikisha Mkapa na askari wake wa miavuli ya kifisadi kizimbani lakini utashi wa kisiasa haupo..................kisingizio ni kuwa analindwa na sheria wakati siyo kweli..........................hivi leo JK akichukua mtutu na akaua watu milioni moja hatumkamati kwa visingizo kuwa analindwa na sheria............................hakuna sheria inayolinda wezi na wabadhirifu............
 
Last edited by a moderator:
Ruta, tunacheza mchezo wa aina yake kweli...ngoja tuone mambo yanavyokwenda.Kikatia, kwani baraza la mawaziri liko juu ya sheria kwa maamuzi yake?
 
Michango yenu nyote ni mizuri ikionyesha upungufu unaojitokeza. Lakini michango ingetoa elimu bora ya uraia kama ingegusia vifungu vya katiba (pamoja na kuwa na viraka vingi) hususani mamlaka ya Rais na Baraza la Mawaziri. Mwalimu NYERERE alipoeleza kuwa Katiba ilikuwa inampatia Rais mamlaka makubwa ya hata kuweza kuwa dikteta wengi watu hatukutaka kumwelewa. Tatizo lipo hapo. Mengine tunayosema ni sawa na kupiga porojo tu kwa sababu hakimu kwenye uamuzi wake ataongozwa na katiba na sheria zilizopo. Tutafakari.
 
Kyaiyembe ufisadi siyo ccm balki ni matunda ya mfumo mbovu ambao hata ukiwapa cdm leo watazalisha ufisadi mkubwa zaidi ya huu....................mfumo mbovu ni ule ambao hakuna uwajibikaji moja kwa moja kwa raia ambao ndiyo waathirika na ufisadi......
Basi maamuzi ya Baraza la mawaziri na BORA zaidi na yatupasa tuyaenzi kwani hakuna na wala hutuwezi kuwa na BARAZA au MABARAZA mengine yaliyo bora zaid ya tuliyonayo au tuliyowahi kuwanayo!. (hii ni kutokana na msimamo wako kuwa CCM ni bora zaidi). Na kwa kuwa CCM hawataki kubadilika na hawatawahi kubadilika wakiwa madarakani!. Maoni yangu ni kuwa uache kulalamikia maamuzi yanayotokea kwani unakubaliana na watekelezaji wake.

By the way, Mfumo huu unaoutumia kama kinga kwa YOUR UNTOUCHABLE PART CCM umeshushwa na Mungu yupi?
na ni nani ataubadilisha na kwa utaratibu ipi?.
 
mtu chake Mkapa ndiye ataenda kuwanasua....................wanachofanya akina YOna ni kumalumu Mkapa akija atasema yalikuwa maamuzi ya baraza la mawaziri ambapo huo ushahidi unatosha kumfikisha Mkapa na askari wake wa miavuli ya kifisadi kizimbani lakini utashi wa kisiasa haupo..................kisingizio ni kuwa analindwa na sheria wakati siyo kweli..........................hivi leo JK akichukua mtutu na akaua watu milioni moja hatumkamati kwa visingizo kuwa analindwa na sheria............................hakuna sheria inayolinda wezi na wabadhirifu............

kwa jinsi ya maelezo ya Mramba ni kwamba yeye ni kama alibanwa kuwapa jamaa msamaha...nanukuu.."maagizo yote niliyachukulia kama ni ya rais alikua akiagiza watendaji wake kutekeleza majukumu yote"mwisho wa kunukuu..maelezo ya Mramba source gazeti la mwanachi uk 4
 
Mimi binafsi nimechoka kuijadili Tanzania na serikali yake na vilongozi wake maana wote ni waongo wanafiki wazembe wazee wafitina walevi..oops sorry i meant wezi nk nk nk nk wacha wafanye vile wanataka mwisho upo unakuja.. wamenichosha mimi hawa watu.
 
Jamani mkifuatilia sana haya mambo ya Ufisadi nchini mtajapata pressure bure..! This style is likely to the Jungle law so kila mtu aendelee kula kulingana na urefu wa kamba yake. Watz hatuna namna ya kuyaondoa haya zaidi ya kuendelea kuona usanii tu ukitendeka. Namkumbuka sana Darwin ninapoyaona haya! MUNGU ATUSAIDIE!
 
UWEZO WA KUFIKIRI UNAISHIA PALE AMBAPO MWANADAMU ANALAUMU BILA KUTOA SULUHISHO.iweje leo tuna chama kikuu cha upinzani CDM bado tuna mawazo mgando ya kuwa hawawezi kufanya lolote?Nchi zote zilizofanya mabadiliko ya kidemokrsia viongozi wake wastaafu wamewajibika.mf zambia,malawi.Sisi tunabaki tunaongea pumba kali about CDM. tAFAKARI CHUKUA HATUA ACHA KULALAMIKA.
 
kwa jinsi ya maelezo ya Mramba ni kwamba yeye ni kama alibanwa kuwapa jamaa msamaha...nanukuu.."maagizo yote niliyachukulia kama ni ya rais alikua akiagiza watendaji wake kutekeleza majukumu yote"mwisho wa kunukuu..maelezo ya Mramba source gazeti la mwanachi uk 4

mtu chake Unapoona mtuhumiwa hajitetei kuwa hakufanya ila utetezi wake ni kuwa alitumwa na bosi wake kwa hiyo hakuwa na jinsi basi bainisha yafuatayo:-

1) Anakiri kuwa kuna kosa alilifanya ila utetezi ni kuwa siyo kwa ridhaa yake.

2) Anakiri ni kiongozi dhaifu kwani vinginevyo angelikataa maagizo batili ya bosi wake

3) Anakiri yta kuwa ni mbinafsi vinginevyo angeliweka masilahi ya taifa mbele badala ya kujiangalia tumbo lake peke yake wakati anakubali kutekeleza maagizo ambayo yana madhara makubwa kwa taifa

4. Utetezi wa Mramba kuwa kama Waziri wa fedha asingeliweza kupingana na maelekezo ya BOT na Ikulu hayana nguvu ya kisheria kwa sababu mwenye mamlaka ya kusamehe kodi ni Waziri wa fedha na hakuna mahali sheria imetoa mwanya wa kuegemea mashinikizo ya Ikulu au BOT.......................kumbuka Bodi ya magavana wa BOT mteuzi wake ni waziri wa fedha..............sasa iwaje Mramba adai alikuwa akifanya maamuzi kwa mashinikizo ya mkataba feki kati ya BOT na Alex Stewart kama siyo utapeli...........................na ikumbukwe mtoto wa Mramba ni mmoja wa wamiliki wa hiyo kampuni feki...................na pia BOT Bodi ya magavana ipo pale kwa ridhaa ya waziri wa fedha..................huyu inavyoelekea atafungwa tu.........
 
Back
Top Bottom