Maamuzi ya baraza la mawaziri sasa ni kinga ya Mafisadi?

Inabidi kuwa kama nchi nyingine ,makatibu wakuu wanakuwa na mikataba ya miaka kadhaa hakuweza kumudu wizara basi anaondoka kimyakimya,na iwe hivyo kwa mawaziri waombe kazi kama nafasi nyingine za serikali.Na hata kupandishwa cheo,kiende kwa kufanyiwa udahili siyo sababu umekaa kwenye nafasi kwa muda mrefu upandishwe tu cheo.
 
Tanzania hii imeishanichosha na episode zilizo na mlengo wakuwaua wananchi wake kwa kuwaibia rasili mali.

Mimi naomba 2015 angalau tupate kuwatoa ila kilio cha wengi Mungu hukipa kipa umbele waache siku zao zinahesabika!
 
Iko siku Watanzania watesema basi inatosha! Kauli hii alishawahi kuisema Waziri Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba!
 
Kama Baraza lina ma--boya fulani na ambao ndo wanaushawishi mkubwa kwa mkulu aka M/kiti wa Baraza, kwa nini wasimnange mahakamani kuwa ndiye mhalalishaji wa ufisadi..Huu ni mchezo uleule kwa watu wale wale hapa TZ, siku yao yaja watakapolia na kusaga meno.. Mungu awajalie wao na watoto wao kuziona siku za ukombozi wa Tanganyika ili basi na wao waje watafune CHIPS DUME na MGAGANI maana tumeapa kuchukua kila kilicho chetu na kuwafukarisha kwa makosa waliyotutendea sisi WATANGANYIKA. Eh Mungu wawezeshe wazifikie siku hizo hasa hasa kina MSOGAz, LUSHOTOz etc
 
...Nilisamehe kodi kwa amri ya Rais Mkapa:Mramba

source :Nipashe ya Leo

na katika mashaidi wake yuko CHENGE..na anadai mmoja bado hajakubali..huyo mmoja ni nani?
 
Re: Maamuzi ya baraza la mafisadi, sasa ni kinga dhidi yao?
kichwa cha habari chahusika,.................

zumbemkuu........tatizo ufisadi ni saratani ya taifa...............mipaka yake siyo baraza la mawaziri tu............
 
Last edited by a moderator:
.
..Nilisamehe kodi kwa amri ya Rais Mkapa:Mramba

source :Nipashe ya Leo

na katika mashaidi wake yuko CHENGE..na anadai mmoja bado hajakubali..huyo mmoja ni nani?

mtu chake........... Tatizo la hawa wagagagikoko ni kuwa..........................baraza la mawziri kamwe haliko juu ya sheria sanasana wanachofanikiwa kufanya ni kuiumbua serikali yao kuwa fisadi mkuu na nambari one ni Raisi wa jamhuri wa Muungano ambao ni ukweli lakini je kisiasa huo ni utetezi kweli?

Kisheria yawezekana ukawa ni utetezi kwa kudai mbona kambale hamjakamata mmenikamata mie dagaa.......tu kwa hiyo mmenibagua......................................lakini utetezi wa kipumbavu kama huo unathibitisha ufisadi ulifanyika ila kuna hila y kumlinda bosi wao ambaye ndiye Raisi..............sasa hapo inaoonyesha ofisi ya DPP, AG na Takukuru haziko huru katika kufanya kazi zao..................vibosile pale hawana uhalali wa ofisi zao kwa sababu mbeleko za kuwabeba zinatoka kwa ridhaa ya fisadi mkuu ambaye ndiye Raisi na kawaweka pale ili wamsaidie kufunika maovu yako dhidi ya jamii.....
 
Last edited by a moderator:
Kama Baraza lina ma--boya fulani na ambao ndo wanaushawishi mkubwa kwa mkulu aka M/kiti wa Baraza, kwa nini wasimnange mahakamani kuwa ndiye mhalalishaji wa ufisadi..Huu ni mchezo uleule kwa watu wale wale hapa TZ, siku yao yaja watakapolia na kusaga meno.. Mungu awajalie wao na watoto wao kuziona siku za ukombozi wa Tanganyika ili basi na wao waje watafune CHIPS DUME na MGAGANI maana tumeapa kuchukua kila kilicho chetu na kuwafukarisha kwa makosa waliyotutendea sisi WATANGANYIKA. Eh Mungu wawezeshe wazifikie siku hizo hasa hasa kina MSOGAz, LUSHOTOz etc

usijali sana masatujr1985.......kilio chetu dhidi ya hizi dhuluma kipo mezani kwa Muumba na atawaadhibu hivi karibuni............................watakapochungulia makaburi yao watadai ni saratani lakini siye tunajua ni laana imewashukia kwa sura ya miwaya................
 
Last edited by a moderator:
Iko siku Watanzania watesema basi inatosha! Kauli hii alishawahi kuisema Waziri Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba!

Ndallo........................tatizo la Warioba naye ana ufisadi wake pale...........................kwenye EPA alilamba hela hadi leo hajawahi hata kutuomba msamaha wala kuzirejesha na leo ndiye anaaminika kutuandikia katiba mpya ya kutunyongelea mbali akidai ndiyomatakwa ya wadanganyika................
 
Last edited by a moderator:
Tanzania hii imeishanichosha na episode zilizo na mlengo wakuwaua wananchi wake kwa kuwaibia rasili mali.

Mimi naomba 2015 angalau tupate kuwatoa ila kilio cha wengi Mungu hukipa kipa umbele waache siku zao zinahesabika!
[MENTION]
Kakakiiza[/MENTION] 2015 ni balaa tupu....................atakayekamata dola atakuwa fisadi asiye na upinzani..............cha kufanya tuendelee kujililia nafsi zetu na za watoto wetu......
 
Inabidi kuwa kama nchi nyingine ,makatibu wakuu wanakuwa na mikataba ya miaka kadhaa hakuweza kumudu wizara basi anaondoka kimyakimya,na iwe hivyo kwa mawaziri waombe kazi kama nafasi nyingine za serikali.Na hata kupandishwa cheo,kiende kwa kufanyiwa udahili siyo sababu umekaa kwenye nafasi kwa muda mrefu upandishwe tu cheo.

Tetty na tudadasi hivi hawa maharamia ni vigezo vipi hutumika kuwateua kwa usiri mkubwa..................mbona raia waote hawapewi fursa sawa ya kuziomba nafasi husika?

mbona ushauri wa TISS na vyombo vingevyo haujaweza kutuletea viongozi bora......................tatizo liko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Siku nyingi wananchi tumekuwa tukiambiwa kuwa pesa za serikali zimeibiwa au zimejenga bara bara lakini sio kweli naomba slaa na mnyika tafadhali waelezeni wananchi kwenye m4c kuwa pesa zinazojenga bara bara na kuibiwa ni zile wanazokatwa kwenye mishahara na wanazonunua kila kitu dukani bank kiberiti .....kuna pesa iakatwakitu inaitwa kodi ndio hizo.

ukisema za serikaki hakuna raia atakuwa na uchungu nazo anajuwa ni za jk au za ccm
 
KAMA KINACHOSEMWA NI KWELI, HAWA watu wanaotumia maamuzi ya BARAZA MAWAZIRI (BM) kujinasua wako sahihi kabisaaaaaa. KWA MUJIBU WA KATIBA, BM ni chombo cha kumshauri tu RAIS: RAIS hafungwi na maamuzi ya BM (IBARA 37). KWA lugha nyepesi maamuzi ya BM hayafungi (not bind) wana BM kwani maamuzi hayo si yao, ni ya RAIS. BM linashauri tu, RAIS ndiye anayeamua. KWA HIYO MTU PEKEE wa kushitaki kwa mujibu wa KATIBA YETU MBOVU ni RAIS siyo wajumbe wa BM: BABA LA MAFISADI MKAPA ndiye aburuzwe mahakamani.

HATA hivyo sasa, RAIS MSTAAFU hawezi kushitakiwa kwa mambo aliyofanya akitekeleza majukumu yake kama RAIS hata kama ni ufisadi. HAPA ndo umuhimu wa kuwa na KATIBA MPYA unapokuja. NASHAURI tutoe maoni kwenye TUME ya WARIOBA ya katiba ili tuepukane na tabia hii ya kubadirisha IKULU (MAHALI PATAKATIFU: JK NYERERE) kuwa pango la walanguzi na sinki la kutapikia mafisadi baada ya kunyonya damu zetu.
 
Dili inakuwa hivi:
"Wanangu, nendeni mkaibe kwa niaba yangu halafu mlete nikugawieni chenu. Baadaye nitakupeleka mahakamani ambako majaji nimewateua mimi."

Hapa tuone jinsi Wadanganywa na Wadanganyika tunavyopigwa changa la macho. Mkuu wa nchi mwenye madaraka ya kuchagua mahakimu, Mkuu wa nchi ambaye ana madaraka ya kusamehe waliohukumiwa mahakamani, Mkuu wa nchi ambaye ana kinga ya maisha ya kutoshitakiwa hata baada ya kutoka madarakani....tutarajie nini?

Hata huu mchakato wa Katiba Mpya ni changa la macho, kwa sababu mwisho wa khabari Serikali/CCM imekamata mpini...imeteua Kamati ya Katiba, ina wabunge wa kutmiza akidi ya kupitisha ikitakacho, ina Raisi ambaye ndie mwenye neno la mwisho katika uamuzi wowote....tutarajie nini?

Kwa mfumo na uoza wa sasa tumebaki Wadanganywa na Wadanganyika hatuna chochote cha kujivunia: Hata hili pande la ardhi linaloitwa Tanzania sio letu tena: linagawanywa, linahongwa, linakodishwa, linauzwa, linachimbuliwa mashimo na kufukuliwa vyote vya aridhini na majini...Ah! na angani, madege ya kijeshi yanaingia na kutoka na madini na wanyama kaam kwamba nchi haina wenyewe. Ni msiba mkubwa! Yupo anayepata picha nchi itakuwa vipi miaka 10, 20, 30...50 ijayo?
Hivi hadi yatokee kama yaliyotokea Rwanda na Kenya ndio tuingie akili? Tunadhani Mungu atakuwa na huruma nasi kutoifanya TZ kuwa kama DRC?

Sipati picha nzuri zaidi ya
Majuto, mjukuu wa Uoza mwana wa Udhaifu!
 
.

mtu chake........... Tatizo la hawa wagagagikoko ni kuwa..........................baraza la mawziri kamwe haliko juu ya sheria sanasana wanachofanikiwa kufanya ni kuiumbua serikali yao kuwa fisadi mkuu na nambari one ni Raisi wa jamhuri wa Muungano ambao ni ukweli lakini je kisiasa huo ni utetezi kweli?

Kisheria yawezekana ukawa ni utetezi kwa kudai mbona kambale hamjakamata mmenikamata mie dagaa.......tu kwa hiyo mmenibagua......................................lakini utetezi wa kipumbavu kama huo unathibitisha ufisadi ulifanyika ila kuna hila y kumlinda bosi wao ambaye ndiye Raisi..............sasa hapo inaoonyesha ofisi ya DPP, AG na Takukuru haziko huru katika kufanya kazi zao..................vibosile pale hawana uhalali wa ofisi zao kwa sababu mbeleko za kuwabeba zinatoka kwa ridhaa ya fisadi mkuu ambaye ndiye Raisi na kawaweka pale ili wamsaidie kufunika maovu yako dhidi ya jamii.....

Je inawezekana Rais Mstaafu Mkapa akapanda tena mahakamni kumtetea Yona na Mramba..(mawaziri wake wa zamani)...?..na jiuliza tu..?
 
Hata mimi nimeshangaa kuwa mzee wa visenti aende kutoa ushahidi wa Mramba na wenzake! Hakika haiingia akilini hata chembe. Watanzania tumeliwa labda aje masiha duniani kwa mara ya pili hivi karibuni kutukomboa!
 
Wala usipoteze muda na Ikulu kwani hilo ni tawi tu la ufisadi. Mzizi wa ufisadi upo CCM hapa ndipo genge la mafisadi linapokaa na kuamua ni yupi kati yao akabidhiwe dola.

(i.e. aende Ikulu) ili aendelee kulinda mirija ya ufisadi waliyokwisha ianzisha tangu mwaka 1992 walipolitupia Azimio la Arusha baharini. Vita ya kweli dhidi ya ufisadi itaanza rasmi CCM itakapong'olewa madarakani. Vinginevyo kutegemea kuwa vita hii itapigawa sasa ni sawa kabisa na kuota ndoto za alinacha.
 
Mkuu Rutashubanyuma Imeniuma sana kujua kuwa imekuchukua mda mrefu sana kugundua hili, Lakini nikwambie ukweli kabisa HAKUNA MTU MWENYE UELEWA MZURI ALIYEKO CCM AMBAYE ANAUCHUKIA UFISADI!. Kama alivyosema Mungu Mwenyezi juu ya SODOMA na GOMORA kuwa KAMA KUNA MWENYE HAKI MMOJA zaidi ya Rutu na familia yake, angeiponya. Lakini alikosekana. Basi na CCM ndivyo ilivyo na mbaya zaidi simuoni wakufanana na Rutu huko CCM.
 
Back
Top Bottom