Maamuzi ya baraza la mawaziri sasa ni kinga ya Mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maamuzi ya baraza la mawaziri sasa ni kinga ya Mafisadi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Aug 23, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Katika khali inayoonyesha kuwa serikali ya ccm inaoongozwa na taswira za upofu usio na tiba, sasa utetezi wa vinara wa kesi za ufisadi wamekuja na mbinu mpya kabisa........... wanatumia ubatili wa maamuzi wa vikao vya baraza la mawaziri na hata kumwita mahakamani kasisi wao Mkuu wa ufisadi Ben Mkapa kama ni kinga ya maovu waliyoyafanya dhidi ya raia wasio na hatia wa taifa hili!

  kesi ya mahalu na wenzie ilifutwa kwa mbinu hizi chafu ambazo ni kinyume na sheria na ile ya Pesambili Mramba na wenzie inaonyesha mwelekeo uleule.........utetezi wenyewe una sura inayoshahibiana na hivi................kuwa serikali iliruhusu tuibe sasa kosa letu ni lipi..............na kama mnabisha iteni hata jemedari mkuu wa ufisadi ben Mkapa na hata wasaidizi wake wa karibu watawathibitishia hakuna rushwa kwa sababu baraza lote la mawaziri liliafiki tule na pengine hata baadhi yao ndiyo waliotutuma tuwaibie watanzania wanyonge...............kwa hiyo kama baraza zima la mawaziri liliweka tiki sasa sisi watekelezaji wa ufisadi tuna makosa gani kama wahariri wake hawaguswi siye tuna makosa gani...............................kwa lugha nyingine ni kuwa kama kweli taifa limeazimia kupambana na ufisadi inabidi tuanze kuliwajibisha baraza la mawaziri hususani mwenyekiti wa vikao hivyo..................kabla hatujawafikia dagaa kama hawa akina Pesambili, Mahalu na wenzao..............

  wakiona hakimu hapokei rushwa wanamkataa na kutumia ushawishi wao kwa msajili wa mahakama kupata hakimu ambaye atatoa maamuzi wayatakayo........................

  huu ni ushahidi tosheleza ya kuwa ufisadi unaanzia Ikulu na kutitirika hadi kwa balozi wa nyumba kumi na baadaye kwa kila raia kujivunia dhuluma................

  Waswahili hulonga........"mwiba uingiliako ndiko utokeako."..............kwa vile ufisadi wote huanzia au kichocheo chake ni ikulu basi tuanzie huku kuushughulikia vinginevyo...................the war against graft is a huge distraction............................what do you think?
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma inaonekana wanakaa pamoja kupanga mipango ya kifisadi na then kwa kesi kama hii akiitwa aliyekuwa mkuu wao anasema ilikuwa maamuzi ya baraza la mawaziri na waliamua kwa pamoja. Kwa maana nyingine hakuna makosa yaliyofanyika. Na hapo jamaa anakua ameokoka kwenda jela.
  Huu ni usanii wa hali ya juu sana na ndo maana toka mwanzo watu walisema hizi kesi ni kiinimacho hakuna atakayefungwa kwa maamuzi haya. Na ndiko zinakoelekea kwa sasa kesi za akina Mramba na Yona na Mgonja.
  Tanzania hii full usanii na kulindana kwa viongozi hawa ambao wanajua hata wakifanya madudu yupo wa kuwatetea na sheria na kanuni walizojitungia zinawalinda kwa kila hali na hawatafungwa kwa maamuzi waliyoyafanya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Mr Rocky khalafu utetezi ni kuwa tusiongelee kesi za ufisadi kwani ziko mahakamani ambako ni michoro tu ndiyo inaendelea...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  akina ngeleja zama zao zikifika watamtaja kikwete,,,,siku zinasonga,kwani umesahau ya mzee wa TICTS,KARAMAGI
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  huku watanzania wanakenua kuwa kuna haki za kupelekana mahakaman,naanza kuhisi kwamba hata mpango wa kuwalaza mahabusu alina yona ulikua ni dili,,,si bure
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  MKAPA na CHENGE vinara wa ufisadi!hao ndio wanaomtetea mramba!
   
 7. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wale majaji fasta fasta kazi yao kubwa mahsusi ni kutumika kwenye kesi kama hizi
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tanzania kuna SCRIPT NZURI ZA UFISAD
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Bajabiri hii inaonyesha usanii wa DPP na Takukuru............kuilinda Ikulu ili itumike kiuliza hivi baraza la mawaziri lipo juu ya sheria?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  Bajabiri[/MENTION] unapoona mahabusu inakarabatiwa ili viongozi wa ufisadi wawe na mahali pazuri pa kujaamiana na hawara zao.......ujue hakuna haki hapo ila kiini macho.............
   
 11. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mzani wetu wa haki(scale of justice) ndo unazidi kuota kutu hivyo na mashaka kama utaweza kuhimili uzito wa kesi hizi mambo yanavyoelekea tayari umeshaelemewa kila kitu ni kiini macho tu hakuna kinachoendelea hapo.
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  BONGOLALA[/MENTION] lakujiuliza kwanini DPP na Takukuru hazkuwafikisha Mkapa & CO.............na kujificha kwenye kichaka cha watekelezaji badala ya kuwaburuta waasisi wa ufisadi ambao baadaye ndiyo huwa vinara wa kuhubiri....rada siyo ufisadi lakini hela za ufisadi zirudishwe ni mali ya watanzania..............................ikija RIchmond/Dowans.............walisema waliovunja sheria ya manunuzi ni baraza la mawaziri kwa hiyo Dowans hawana hatia...........................ilipokuja Kashfa ya ubalozi wa Italia................Mkapa ambaye ndiye mtuhumiwa nambari one akageuzwa kuwa shahidi..........na akajichoma kizimbani eti anatushangaa siye tunaolia na ufisadi wakati Ikulu ilibariki tuliwe...........................na sasa Mramba & CO> weanfuata nyayo..................swali hivi mshtakiwa nambari one Mkapa na JK kwanini hawaburutwi mahakamani wakajibu kama baraza la mawaziri lipo juu ya sheria?
   
 13. k

  kanewi JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 214
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  hata magereza kwenyewe hawakuwa nalala ilikuwa geresha tu,mbwembwe nyingi na ving'ola eti anaenda segerea ikifika saa tano V8 tinted inamchukua mpaka home then asubuhi anarudi,.inakuwa kama anaamka asubuhi anaenda kazini na kurudi usiku,.hii ndo TEENTZ
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  Kijereshi[/MENTION] inabidi tuendelee kuhoji jinsi taasisi ya DPP na takukuru ikiwemo idara ya usalama zinaundwa vipi na kama kweli zina mchango wowote katika maendeleo ya taifa...............au tumerundika watu kutafuna helza za umma ili kushamirisha dhuluma tu?
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  [h=2][/h]
  [MENTION]
  vipik2[/MENTION] ukiona katiba mpya bado raisi na tume yake fekki ya kimahakama ndizo zinaendelea kuteau majaji ujue ya kuwa tumetapeliwa.........................................ajira zote za umma lazima zitangazwe kwenye vyombo vya umma na zitoe fursa sawa kwa wote kuziomba siyo huu utamaduni wa kupeana ugali kwa kujuana halafu kazi inakuwa kuteteana.................................katika ufisadi............
   
 16. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Re: Maamuzi ya baraza la mafisadi, sasa ni kinga dhidi yao?
  kichwa cha habari chahusika,.................
   
 17. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  kasisi maana yake nini mkuu?
   
 18. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Narudia tena jamani, tusitarajie serikali kumaliza baadhi ya matatizo yanayoonekana kwa wananchi wa kawaida nje ya mfumo wa viongozi wa serikali, kwa kuwa kwa upande wa serikali linaloonekana tatizo kwa mwananchi kwa kiwango kikubwa ni fursa kwa serikali na wale wanaoiendesha. Hivyo tusitarajie watu wanaofaidika na mfumo huo watukombowe na ndiyo maana wakati mwingine ni vigumu kumwondoa mtu ambaye amefika ngazi ya juu ya uongozi wa serikali kwa urahisi zaidi ya kumuhamisha kwa kuwa ukimtoa anaweza kutoa siri ya jinsi serikali inavyofaidika na mfumo uliopo au miundo iliyopo. Kwa kuwa serikali haiwezi kubadili fursa hizo ambazo sisi tunaziona ni matatizo, suala kubwa hapa ni sisi wananchi kubadilika na kufunguka kuona mwanga na giza ili kuanza kujikomboa na siyo kuisubiri serikali ikuletea neema mabayo hutakaa uione. Badilika mwananchi.
   
 19. m

  mharakati JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ukiona harufu ya ufisadi huwezi kuacha kazi na kuresign? lazima ung'ang'anie tu madudu kwa sababu umeaambiwa na boss, wewe mwenye signature ndiyo unaenda jela na kufilisiwa kwa sababu kama ulikua mjinga kuona au siyo mzalendo kuona madudu yale kwa nini haukujitoa kwa kujiuzulu. Haya ndiyo haya haya ya EL anataka kusafishwa kwa kusema Richmond ni ya JK, sasa yeye hakuona madudu? aliona, hakuona kama taifa litaenda gizani na kupoteza hela? aliona, sasa analalamika nini kama ameonewa...hii tamaduni ya kutochukua personal responsibility katika uongozi ni ujinga mtupu
   
 20. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa namna uelewa wa watanzania juu ya haki zao unavyoongezeka kwa kasi ndogo ndivyo CCM watakavyozidi kuwahadaa na kuzoa kura za watz wasiojua haki zao. Kwa hali hii naomba wanaCDM waongeze juhudi za kuwafumbua macho watz wajue namna fedha zao zinavyoliwa. Kwa baadhi ya wanakijiji ninaongea nao wanasema acha CCM wale hela maana si zao bali ni za Serikali! Inasikitisha!
   
Loading...