Maamuzi ni yako

Maamuzi ni yako

Kila nikifikiria MKUBWA FELLA Sasa anaomba MSAADA NAPATA ukakasi kuandika ninacho KUSUDIA, anyway
 
Pesa ni Siri kubwa sana na kua na pesa nyingi inabidi ufanye mambo mengi ya siri yasiyokubarika na [jamii] na uwe msiri kiasi cha kujifanyia siri wewe mwenyewe sio tu kumwambia mtu hata wewe usijiambie siri zako maana ukifanya hivyo ni namna moja wapo ya kujisariti.. kua na pesa nyingi kuna hitaji ukwepe vikwazo vya wanyonyaji wa pesa ambao wamejitungia vijisheria vya kukukwangua pesa huku wewe unateseka wao wanakuja tu kuzipakua wakati unazitafuta walikua wamejiweka pembeni.. mifano ni mingi ila kua na pesa nyingi sio lazima uwe hao wote uliowataja kuna formula ndogo sana ukiitumia unakua na rundo la maburungutu ya pesa ila siwezi kukupa hio nitakupa mfano mdogo tu wengi unaowaona wana pesa nyingi wanatumia kanuni ya kumkwepa adui wa kuzikwapua pesa zao kwa mbinu na namna yoyote iwe kwa kuroga (wabongo na waafrika wengi hufanya hivyo) au kwa kutumia ukatiri ilimradi tu wawe na pesa nyingi na ili uwe na pesa nyingi kanuni kuu ni kutokua na roho ndogo au roho nyepesi wenye roho ndogo au roho nyepesi hawana pesa nyingi wana pesa za kutimiza mahitaji yao ya kila siku tu.. ili uwe na pesa nyingi inakubidi uwe na roho ngumu ya kuweza kulinda himaya ya pesa zako maana utakua unamiliki vitega uchimi vingi sio kawaida km ni kampuni basi utakua una miliki si chini ya kampuni 20+ sasa ku-control hivyo vitega uchumi ili pesa zisikukimbie roho ngumu lazima ihusike na hapa simaanishi kulinda himaya kwa kuzirasimisha kwa mamlaka za kiutawala yaan unaweza ukarasimisha ila kinachoendelea nyuma sivyo km kinavyoonekana mbele au kuzihifadhi bank la hasha pesa zako.. mfano wachezaji mpira/mabondia wa ngumi za kulipwa ukiangalia utaona wanavunjwa miguu/kupasuka vichwa na kufumuana misuli ya mapaja na kubakia na makovu na maumivu ambayo hayafutiki mpaka kufa kwao still bado mtu anajiuguza baada ya muda mfupi utamuona yupo tena uwanjani au kapanda ulingoni sio kwamba amesahau kilichompata uwanjani ila sababu ni roho ngumu ya kuweza kulinda himaya ya pesa zake usipofanya hivyo pesa zinakukimbia.. kingine cha mwisho na cha umuhimu ni muda mwenye pesa nyingi anatumia muda mwingi kutafuta pesa kwa kila namna na kila jinsi ili kupata pesa nyingi.. na kingine cha mwisho ambacho sio cha umuhimu hakuna pesa tamu km pesa isiyokua na makato yoyote yaan unauza bidhaa pesa unayopokea inakua vilevile bila kua na mtu wa kati kupiga panga lake mfano unauza kitu laki unapata laki km ilivyo bila kua na panga la kukatwa elfu 20 ukabakia na 80 hio pesa ndio tamu zaidi nakwambia nikiwa na experience
Sawa mkuu ila acha nafasi kwenye maandishi yako ili madini tuyapate kwa uzuri zaidi
 
Sawa mkuu ila acha nafasi kwenye maandishi yako ili madini tuyapate kwa uzuri zaidi
Sawa mkuu ila kuna kitu cha kuongezea hapo nilisahau kukiweka na kukielezea nitaelezea kwa uchache sana na kurudiarudia sababu [repetition is the father of learning] unaporudia na kurudia na kurudia na kurudia ndio unavyozidi kujifunza zaidi, kua na pesa nyingi maana yake ni kutumia muda mwingi kuwekeza kwenye pesa.. hapo unielewe ninachomaanisha kwa ufasaha muda ni pesa, muda wako mwingi unavyouwekeza kwenye pesa ndivyo hivyo hivyo unavyojiongezea uwezo wa kua na pesa nyingi.. swali linakuja unafanya kitu gani ambacho kinakutengenea pesa nyingi? yaan sio unafanya kitu ilimradi upate pesa hapana kuna watu wana pesa na kuna watu wana pesa  nyingi.. hawa wenye pesa nyingi wamewekeza muda wao mwingi kwenye utafutaji wa pesa ambao huu muda ulikuja kuwalipa baadae, hapa namaanisha unaweza kufanya jambo lenye kuweza kukuingizia pesa nyingi leo ukatumia muda wa [miaka 10] mbele ndio ukafanikiwa kupata pesa nyingi watu wanaokuangalia ukiwa unaingiza faidi nyingi baada ya miaka 10 wengi hudhani umeanza jana leo ukafanikiwa kufika ulipofika kumbe wewe umetumia [muda] wa zaidi ya miaka 10 kufika hapo ulipofika.. mfano ni huu wewe anzisha kitega uchumi kimoja kisha weka [muda] wako hapo baada ya miezi 6 ukiona kinafanya vizuri na kinakuingizia faida kiasi kwamba kinaweza [kujiendesha] chenyewe hata wewe ukiwa haupo au umelala au umelazwa anzisha kitega uchumi kingine papohapo bila kuchelewa na hicho pia kipalilie taratibu kikue kikianza kuchanganya ndani ya miezi 6 kwamba kinaweza kukuingizia faida [maradufu] pasina kutetereka pale wewe utakapokua haupo au unaumwa au umelala kinaweza [kujiendesha] chenyewe bila kukutegemea wewe papohapo bila kuchelewa anzisha kitega uchumi kingine kisha anza kukipalilia taratibu taratibu kipe [muda] wako kipalilie taratibu ndani ya miezi 6 kikianza kukuonyesha kwamba kinaweza [kujiendesha] chenyewe bila kutegemea uwepo wako na kukupatia faida maradufu na chenji ikabaki papohapo usichelewe anzisha kitega uchumi kingine..

Ili unielewe inabidi akili yako iwe imetulia km maji ndani ya [mtungi..]
 
Back
Top Bottom