Maamuzi magumu sana

Maamuzi magumu sana

BEST ONE BOY

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Posts
309
Reaction score
221
Habari za siku wadau wa MMU ..
Poleni na majukumu ya kimaisha ..

Ngoja niende direct kwenye mada

Mwezi wa tatu mwishoni mwaka huu
Nilileta mada isemayo kwamba
"Ushauri kwa huyu Ex-wangu"
KWA kufupisha kwamba huyu binti nilimpenda sana na bado nampenda

Nirudi nyuma kidogo..nilikua naye kwenye mahusiano ya awali almost for three-year
Baadae akaja kunisaliti alipewa ujauzito na
Mwanaume mwingine bila ya Mimi kujua kwaio Mimi nilikua naendelea kumpa pesa ya matumizi na huku kahamia kwa siri kwa huyo jamaa na hata baada ya kujifungua hapo ndipo akaniambia ukweli kuwa Ana mtoto wa mwanaume mwingine niliumia sanaa mana .
Alikua furaha wa moyo wangu ..

But nikawa busy na kitabu mana mwaka huu ndio nimemaliza chuo kwaio nilikua napiga shule na sikupendaaa kabisa kujihusha na masuala ya relationships kwa muda huo since mwaka juzi ..

Kulingana na type ya maisha anayoishi kule kijijini na huyo mwanaume maisha yalikua hayaendi vizuri basi full shida kwa Mimi kulia kila siku kuwa nimekosa sanaa nisamehe siwezi kurudia naomba nisamehe ...

Mana hata baadhi ya watu walitumwa kuja kumuombea msamaha kwangu ..
Na Mimi nikasema ngoja nilete wazo hapa JF nipokee mawazo ya wadau halafu baadae nikaja na conclusion ya kusamehe na nikakubali kumrudia but chini ya sheria

-kuhusu mtoto ntamsaidia kumtunza
Mana mwakani mtoto anafikisha miaka miwili na nusu kwaio nikamwambia kuwa ataanza pre-school Kwanzaa

"""ILA """"
SHERIA YA PILI HII

nikamwambia kuwa Mara nikijua tuu una mahusiona na bwana wa huyu mtoto basi mahusiano yetu yanakatika hapohapo na hata ikiwa mwanaume mwingine yoyote yule nikijua tuu uhusiano wetu unakuta hapohapo ... mwanamke huyu kaapa kabisa kuwa hatorudia makosa yake .....
ILA na yeye nimempa kamtaji kidogo cha biashara yake ndogo..

Kwangu nimeamua hivi wana jukwaa
Wewe..
 
Umeishaamua tayari mie sina la kuongeza ila nakupongeza una upendo sana
 
Hongera kwa kuwa na true love. Kiukweli wazazi huwa hawaachi kuwasiliana na wakati mwingine hukumbushiana lkn inategemeana na walivyoachana ila lwa huyu waliachana kwasbb ya shida ila walikuwa wanapendana. Ila mkuu kwann usingetafuta mwanamke fresh ukaanza naye maisha?
Ok! Hongera kwa huo moyo ila mm nisingeweza lbd km angekuwa hana mtoto
 
Unaamini kiapo?? Wakati rais tuu anaapa kuiheshimu katiba akishaingia anasahau kiapo...watu wanaapa wakati wanafunga ndoa na soon wanasahau viapo vyao...

To me I think ujifunze kukubali kumwacha aende. Huyo mwanamke kamkimbia mwanaume wake aliyemzalisha kutokana na shida za maisha kaja kwako kwenye auheni siku ukifulia ataenda kwa mwingine.

Usipende kusikiliza misamaha ya watu, utakuja kulia
 
Hongera kwa kuwa na true love. Kiukweli wazazi huwa hawaachi kuwasiliana na wakati mwingine hukumbushiana lkn inategemeana na walivyoachana ila lwa huyu waliachana kwasbb ya shida ila walikuwa wanapendana. Ila mkuu kwann usingetafuta mwanamke fresh ukaanza naye maisha?
Ok! Hongera kwa huo moyo ila mm nisingeweza lbd km angekuwa hana mtoto
Waliachana kisa mwanaume hawajibiki home full misele hawa vijana
 
Mkuu sijamzuia mawasiliano mana hata saizi sikai naye nyumba moja yeye kwake na Mimi kwangu ila kwa masharti hayo tuu akiweza fresh
 
Waliachana kisa mwanaume hawajibiki home full misele hawa vijana
Kwa hapo sitashangaa kuona mwanamke ana iba. Ogopa shida, shida humfanya mtu kukubali kila kitu lkn hamaanishi itabadilisha moyo wa mtu.
Aliyekuwa naye, akaenda kuolewa kisiri, akapata mtoto na baadae wakarudiana.
Watu wote wangekuwa km mtoa uzi, usaliti usingekuwepo.
 
Mkuu najua sana hiloo kuiba kwa siri ila nilikaa naye na kuzungumza within three month's up to now almost five month's inakimbilia Mimi nikamweleza ukweli huo kuwa nikijua tuu umeanza kuchepuka basi kila mtu na time yake
 
Ila hongera kwa upendo wa dhati. Binadamu wote tungekuwa hivi hakika usaliti ktk mapenzi usingekuwepo.
Nakushauri, vitisho na ukali hamvimfanyi mtu kutokusaliti ila kuna wakati inasaidia.
Jenga mazingira yatakayomfanya asikusaliti, na muoneshe upendo wa kweli hii itamfanya hashindwe kukusaliti. Akikumbuka tu hata km yupo na mwanaume wa mtoto anahailisha na kuvaa nguo.
Hakuna kitu wanachomiss wanawake km upendo wa dhati na hii ndiyo fimbo ya kweli kwa mwanamke.
 
Ndio mana mtoto wake nataka kumpeleka pre school mwakani Mungu akijalia
 
Mkuu sijamzuia mawasiliano mana hata saizi sikai naye nyumba moja yeye kwake na Mimi kwangu ila kwa masharti hayo tuu akiweza fresh
Safi.
Usimbane mkuu sana. Mpe true love na unapokutana usiongelee masuala ya usaliti wake. Ongelea mambo ya maendeleo
Upendo wa dhati ni fimbo kwa mwanamke yyte.
Ukitaka kuona angalia wanawake waliopendwa kwa dhati kisha wakasaliti ndoa zao huwa wanajuta, unaweza tamani uombee msamaha.
Nimesoma shuhuda nying sana zinazohusiana na usaliti. Huyu hata akikusaliti (ikitokea ila siombei hivyo) usimtukane wala kumngimbeza ww ondoka taratibu km upo
 
Back
Top Bottom