Maamuzi magumu sana

Maamuzi magumu sana

Mkuu huyu mwanamke Mara ya kwanza nilikua naye kwenye mahusiano sikujua kumbe mwanamke huyu akatongozwa na jamaa ambaye amezaa naye na kuanza kuishi naye kwa siri mpaka akashika mimba wakati huo Mimi mambo ya shule kukutana naye ilikua nadra kila baada ya miezi mitatu ndio kurudi nakuta demu ana mimba ya jamaa kwaio jamaa ikabidi akatunze mzigo ila demu akaja kurudi kwao kwa sababu jamaa haeleweki na pia amemfumania na wanawake wengine
Si kila mahusiano lazime yawe ndoa,
Kwa minzani yake mwewe alipima kati ya wewe na huyo jamaa, akamuona jamaa anafaa

Sasa igeuke ije kuwa kwako, hapa kuamini ni vigumu


LABDA KAMA MNAANDA SINEMA SIO NDOA ASEE!!!
 
Pale unaporuhusu hisia zitangulie ufahamu/akili
 
Mkuu wew unamoyo wa chuma na nikuambie tuu kitu huyo mwanamke atakuja kukusaliti tena na tena kwanza mungu amekupenda sana amekuonyesha mapema kwamba huyo sio wa kuoa hebu kuwa na moyo wa kiume vip vingine havihitaji ushaurii jamani ndio maana ukazaliwa mwanaumee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakupa ushauri huu ambao kama mtoto wangu akikumbwa na ili tatizo ndio ungekuwa msimamo wangu:

Achana na huyo mwanamke hana mapenzi na wewe ila anaangalia maslai yake tu. Jiulize kama huko alikoenda mambo yangekuwa mazuri je angerudi kwako? Mapenzi ya kweli hayana masharti unapoweka masharti tayari utaishi kwa kifungo mapenzi ni kujiachia kwa roho moja. Kama amezaa na huyo m/ume lazima awasiliane nae na kuonana nae maana wameshachangia damu hivyo ilo likitokea utaishi kwa jakamoyo na utajutia maamuzi yako. Bado una nafasi ya kutafuta mtu mwingine wa kuanza nae mahusiano nae mapya linalokusumbua hapo ni kumuwaza m/mke mmoja tu wakati duniani wako mabilioni. Mapenzi sio huruma wala hisani, mapenzi ni kupendana huyo dada hakupendi umeshaonyeshwa trela subiri movie kamili pale ambapo umeshajiingiza mazima utajuta sana na utakumbuka huu ujumbe wangu
 
Back
Top Bottom