Maamuzi magumu sana

Maamuzi magumu sana

Sijui nikupongeze au la, ila umepotea. Mwanamke kahamia kwa mtu, kapokea pesa zako naza jamaa kisha akakufungukia ukweli kwamba ana mtoto na siyo wako.

Halafu umejua wazi huu msamaha anaokuomba ni kwa vile maisha hayamuendei sawa, yakianza kumuendea sawa je? Huyo aliyezaa naye akiamka tajiri je?

Dah
 
Sijui nikupongeze au la, ila umepotea. Mwanamke kahamia kwa mtu, kapokea pesa zako naza jamaa kisha akakufungukia ukweli kwamba ana mtoto na siyo wako.

Halafu umejua wazi huu msamaha anaokuomba ni kwa vile maisha hayamuendei sawa, yakianza kumuendea sawa je? Huyo aliyezaa naye akiamka tajiri je?

Dah
Mkuu nimempa Kwanzaa mda wa matizamio k wanzaaa
 
Aliyependa kama wewe unadhan unamshauri nini akuelewe zaidi ya kukuombea kila lenye kheri tu
Uzuri umefanya kitu moyo unapenda hujalazimishwa.
Anyway love is beautiful don't be too emotional.Enjoy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za siku wadau wa MMU ..
Poleni na majukumu ya kimaisha ..

Ngoja niende direct kwenye mada

Mwezi wa tatu mwishoni mwaka huu
Nilileta mada isemayo kwamba
"Ushauri kwa huyu Ex-wangu"
KWA kufupisha kwamba huyu binti nilimpenda sana na bado nampenda

Nirudi nyuma kidogo..nilikua naye kwenye mahusiano ya awali almost for three-year
Baadae akaja kunisaliti alipewa ujauzito na
Mwanaume mwingine bila ya Mimi kujua kwaio Mimi nilikua naendelea kumpa pesa ya matumizi na huku kahamia kwa siri kwa huyo jamaa na hata baada ya kujifungua hapo ndipo akaniambia ukweli kuwa Ana mtoto wa mwanaume mwingine niliumia sanaa mana .
Alikua furaha wa moyo wangu ..

But nikawa busy na kitabu mana mwaka huu ndio nimemaliza chuo kwaio nilikua napiga shule na sikupendaaa kabisa kujihusha na masuala ya relationships kwa muda huo since mwaka juzi ..

Kulingana na type ya maisha anayoishi kule kijijini na huyo mwanaume maisha yalikua hayaendi vizuri basi full shida kwa Mimi kulia kila siku kuwa nimekosa sanaa nisamehe siwezi kurudia naomba nisamehe ...

Mana hata baadhi ya watu walitumwa kuja kumuombea msamaha kwangu ..
Na Mimi nikasema ngoja nilete wazo hapa JF nipokee mawazo ya wadau halafu baadae nikaja na conclusion ya kusamehe na nikakubali kumrudia but chini ya sheria

-kuhusu mtoto ntamsaidia kumtunza
Mana mwakani mtoto anafikisha miaka miwili na nusu kwaio nikamwambia kuwa ataanza pre-school Kwanzaa

"""ILA """"
SHERIA YA PILI HII

nikamwambia kuwa Mara nikijua tuu una mahusiona na bwana wa huyu mtoto basi mahusiano yetu yanakatika hapohapo na hata ikiwa mwanaume mwingine yoyote yule nikijua tuu uhusiano wetu unakuta hapohapo ... mwanamke huyu kaapa kabisa kuwa hatorudia makosa yake .....
ILA na yeye nimempa kamtaji kidogo cha biashara yake ndogo..

Kwangu nimeamua hivi wana jukwaa
Wewe..
Maumivu mengine mnayatafuta tena kwa udi na uvumba kabisa. Unampenda ndio hatubishi lakini hakupendi kwake wewe ni FURSA. Kwa mujibu wa maelezo yako mwenyewe kwako zimemrudisha DHIKI. So kama alivyoweza kwenda kwa laazizi asali wake wa moyo kipindi kile ndivyo atakavyorudi pindi huyo waubani wake akirekebisha mambo ukizingatia wana mtoto. Mimi nikutakie kazi njema ya kumtunzia jamaa goma lake wakati huu akitafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa kuwa na true love. Kiukweli wazazi huwa hawaachi kuwasiliana na wakati mwingine hukumbushiana lkn inategemeana na walivyoachana ila lwa huyu waliachana kwasbb ya shida ila walikuwa wanapendana. Ila mkuu kwann usingetafuta mwanamke fresh ukaanza naye maisha?
Ok! Hongera kwa huo moyo ila mm nisingeweza lbd km angekuwa hana mtoto
Huu uamuzi alio ufanya kijana nimuite ni uamuzi wa KIPUMBAVU samahani kwa neno kali kidogo


Kwanza umeitafuta furaha yako kwa kukatisha furaha yake,
Hili bomu sikufichi siku likiripuka humu ndani hapatatosha.

Ujue kabisaaa
KWAKO kafuata mtaji, akiupata atarudi kuitafuta furaha yake
Umempokonya mwanaume waliependana mpaka Mungu kawatunuku tunda la kazi yao yaani mtoto halafu ukaenda mbaaaaaali sana ukajimilikisha na mtoto, Mungu wangu, fikiria yule mwanaume kule anaishije na analiaje??
Kumbuka chozi la mwanaume mwenzio halitokuacha salama
 
Mkuu najua sana hiloo kuiba kwa siri ila nilikaa naye na kuzungumza within three month's up to now almost five month's inakimbilia Mimi nikamweleza ukweli huo kuwa nikijua tuu umeanza kuchepuka basi kila mtu na time yake
Unataka kutwambia aliamua kuolewa na baba mtoto wake ukiwa hujamwambia kuhusu hatima ya mahusiano yenu??
 
Ila hongera kwa upendo wa dhati. Binadamu wote tungekuwa hivi hakika usaliti ktk mapenzi usingekuwepo.
Nakushauri, vitisho na ukali hamvimfanyi mtu kutokusaliti ila kuna wakati inasaidia.
Jenga mazingira yatakayomfanya asikusaliti, na muoneshe upendo wa kweli hii itamfanya hashindwe kukusaliti. Akikumbuka tu hata km yupo na mwanaume wa mtoto anahailisha na kuvaa nguo.
Hakuna kitu wanachomiss wanawake km upendo wa dhati na hii ndiyo fimbo ya kweli kwa mwanamke.
Hivi itatokea kwa miujiza gani huyo binti aipate furaha yake wakati anaishi na mtu si kwa mapenzi bali kwa shida??

Kunamikakati gani tofauti na vitisho vitakavyotenga ile nguvu ya mzazi mwenzie isimuandame??


Hapa mtamdanganya tuu ni bora mara mia angeolewa hafu akaachika aka kaa muda hata miaka mitano angekuwa amejifunza kitu. Lakini kamkimbia mume wake halari kisa ugumu wa maisha,
AMESAHAU RIZIKI HUPANGWA NA MUNGU, NA MUDA WA KUTOA HUPANGA MUNGU PIA.

Siku ikitokea Mungu akamnyooshea mkono wake huyu mume wake na baba wa mwanae na yeye akapata gooood life, Akikukimbia utamlaumu??
 
Unataka kutwambia aliamua kuolewa na baba mtoto wake ukiwa hujamwambia kuhusu hatima ya mahusiano yenu??
Mkuu mwanzoni kipindi nilikua na mahusiona naye yeye kumbe alikua na Mtu mwingine mana Mimi mda mwingi shule sana kwaio ndio akashika ujauzito wa huyoo jamaa na ndio demu akahamia kwa jamaa baada ya mwaka mmoja demu karudi kwao mana walishandana mambo mengi Mara matunzo hamna Mara jamaa yupo na wanawake WENGINE mwanamke ndio akaamua kurudi kwao na kuomba msamaha kwangu
 
Safi.
Usimbane mkuu sana. Mpe true love na unapokutana usiongelee masuala ya usaliti wake. Ongelea mambo ya maendeleo
Upendo wa dhati ni fimbo kwa mwanamke yyte.
Ukitaka kuona angalia wanawake waliopendwa kwa dhati kisha wakasaliti ndoa zao huwa wanajuta, unaweza tamani uombee msamaha.
Nimesoma shuhuda nying sana zinazohusiana na usaliti. Huyu hata akikusaliti (ikitokea ila siombei hivyo) usimtukane wala kumngimbeza ww ondoka taratibu km upo
Hivi mbona mnamdanganya huyu kijana.

Swali la kizishi

Hivi huyu mama kamsaliti nani hasa??
a)huyu tunaemshauri humu
b) mumewe ambaye kamkimbia tena na damu yake??

Hapa utagundu huyu tunaemshauri ndio kasababisha binti kusaliti ndoa yake, na mwisho wa siku
 
Hivi mbona mnamdanganya huyu kijana.

Swali la kizishi

Hivi huyu mama kamsaliti nani hasa??
a)huyu tunaemshauri humu
b) mumewe ambaye kamkimbia tena na damu yake??

Hapa utagundu huyu tunaemshauri ndio kasababisha binti kusaliti ndoa yake, na mwisho wa siku
Mkuu huyu mwanamke Mara ya kwanza nilikua naye kwenye mahusiano sikujua kumbe mwanamke huyu akatongozwa na jamaa ambaye amezaa naye na kuanza kuishi naye kwa siri mpaka akashika mimba wakati huo Mimi mambo ya shule kukutana naye ilikua nadra kila baada ya miezi mitatu ndio kurudi nakuta demu ana mimba ya jamaa kwaio jamaa ikabidi akatunze mzigo ila demu akaja kurudi kwao kwa sababu jamaa haeleweki na pia amemfumania na wanawake wengine
 
Back
Top Bottom