Maamuzi gani nichukue dhidi ya ndoa yangu?

Maamuzi gani nichukue dhidi ya ndoa yangu?

Je mumeo anakufanyia vitendo vya kikatili km kukupiga na kukutukana?na umesema anakunywa pombe ni mara moja moja au kila siku kiasi kwamba hana muda na ww?
 
There is a bad smell that, seems you are confusing yourself. Ulifunga ndoa na mtu ambaye moyo wako haukumpenda! Kwa sababu gani? I dont mean to blame the victim..fanya hivi..

Kwa kuwa umefunga ndoa, u have nothing to do but UMHESHIMU MME,hapo pia uambie moyo wako umpende bila sharti,na amani utaipata

Huwezi kuvunja ndoa, huna sababu hiyo,maana unaishi kwa kiapo hapo uliopo

Acha kunywa pombe, na tangaza mabadiliko hayo kwa mmeo (nifuatilie hapa chini)
 
Andaa mafungo ya kuomba rehema kwa Mungu,jitakase...then funga na kumwombea mmeo afunguliwe na utumwa alionao wa tabia zake


Naona kama vile unajiharibu mwenyewe, hujajikabidhi kwenye ndoa haswa, basi jikabidhi kwa kukiri moyo wako kuwa huyo ndio mme uliopewa.


Iwapo akili na hisia zako umeziweka rehani kwa kuamini kuwa mpaka unywe pombe ndio ufanye tendo la ndoa,probably hapo ndipo ulianzia kujiharib maana it is now a condition that you must drink so that you can have sex, hili kosa lako kubwa sana

Otherwise i pray for you that God can stand before you right now..
 
my dear sijawahi kutafuta faraja yoyote ,tangu nimebakwa huwa nahisi bado naendelea kubakwa sijui kwa nini
unataka tukusaidie nn funguka unapewa ushauri hueleweki unahisi kubakwa wakati umefunga ndoa wewe huna matatizo
 
Daa Dada pole sana
Ila sis wanawake tunajidanganya sana juu ya mapenzi cjui tatizo ni akili or ndo mkumbo

From mwanzo ulikuwa ushaona huyu mwanaume sio ila uliamua kusonga mbele had unafunga ndoa...pia sipend kauli ya kusema yy kakufundisha kunywa pombe its means wewe unsound or.kwann jaman ungemwacha let it go ona sasa 7 yrs unaishi kwa kupritend that's bad sana.ni mateso sana wen u choose wrong person for ur life.

Watu wanasema ukaombewe tataixo ni wewe hayo maombi hayatafanya kazi kama hujabadili.yawezekana bdo ishu ya kubakwa unayo kwenye akili hiyo imebakia kama historia .simama songa mbele
aje kwangu nfanyie maombi atasahau kubakwa
 
Hata sijui nikushauri nini isee lkn endelea kuvumilia so long jamaa hana tatizo na wewe
 
Pole sana mama kwa matatizo... ushaur jaribu kusahau yaliyopita na mambo mengine yataenda sawa.
Jaman wana jf kuuliza c ujinga. Huwa nackia tu ingia pm ndio nn hiyo pm?
 
Sass unaempenda utampata lini
Na hao watoto ndo kabisaa
Tulia tu dada Mungu atakusaidia
 
Poleni na majukumu ya kila siku wana JF, ikiwa ni mara yangu ya kwanza kuweka post, nahitaji msaada sana kutoka kwenu wazoefu kwenye ndoa, wana dini kimaombi zaidi .

Mimi ni mama wa watoto wawili, nimefunga ndoa miaka saba iliyopita, mwanzo kabisa maisha yangu ya mahusiano hayakuwa mazuri hata kidogo, first of all niliwahi kubakwa nikiwa na umri wa miaka 15, baada ya hapo niliishi maisha ya tabu sana mpaka nilipokuwa mkubwa na kuweza kujitambua.

Nillianza maisha ya mahusiano nikiwa na miaka 21 na mwanaume niliyetokea kumpenda na kuamini yeye ndio atakayenifuta machozi na huzuni zangu.

Mambo hayakuwa hivyo kwani miaka miatatu ya mahusiano yetu alienda oversizi na kuniacha na pia kuamua kukata mawasiliano kabisa. Nilibaki na kovu na maumivu niliyokosa tiba. Nilimtafuta bila mafanikio na kuamua kumove on na maisha yangu,ingawa ilikuwa ni ngumu sana.

View attachment 169831

Baada ya hapo nilikutana na mwamaume ambaye sikujua kama ni kweli nampenda kwani siku zote nilipokuwa nae nilikuwa namuwaza X wangu aliyeniacha bila kusema neno lolote.

Mwanaume huyu mwanzo sikumuelewa kabisa kwanza alikuwa mgomvi na mkorofi kwa watu dakika mbili alishabadirika haeleweki kama kinyonga ,police kwake ilikuwa ni kama nyumbani.

Nyimbo zake mara nyingi zilikuwa ni za kina Tupac ,Snopy D na wale aina ya magang star Ingawa alikuwa msomi na kazi nzuri,na maisha yake mpaka sasa bado miziki yake ndio hiyo ,starehe kwake hataki kuacha wala kupunguza.

Niliamini atabadilika ingawa nilikuwa nakwazika sana kuwa nae alinifundisha kunywa Pombe ,Ok nikawa mnywaji mzuri na ili niwe nae Kimapenzi niliona ninywe kwanza ndio nakuwa huru na hayo ndio yakawa maisha yangu..Tuliendelea na mahusiano ya muda mrefu hatimaye nilianza kumzoealakini si kumpenda ,

Tukiwa tayari ndani ya mahusiano nilishika mimba na tukakubaliana kuanza kukaa pamoja ,taratibu za mahali zilifanyika na nikahama rasmi lakini kwa sababu jamaa alikuwa mtu wa starehe alikuwa akiniacha na kurudi usiku wa manane amelewa mara anitukane na sikuona kama alikuwa ananithamini na hali yangu ya ujauzito chuki moyoni ikawa inazidi siku hadi siku.

Ingawa kuna wakati nilikuwa naona kama ananipenda .Baada ya kujifungua tulianza taratibu za ndoa lakini moyoni mwangu nikijua kabisa mwanaume huyu sina mapenzi nae hata kidogo.Na nilikuwa najiuliza kwanini nafunga ndoa?

Ingawa kuna vitu vingine vilikuwa kama najifosi kufanya. Tulifunga ndoa takatifu nakuanza kuishi kama mke na mme ,na mungu akatujaalia kuongeza mtoto mwingine wa kiume lakini system yangu ni mpaka ninywe ndio nakuwa na hisia za kuwa na mme wangu.

Ndani ya ndoa yangu nimekuwa nikiishi kwa kujifanya nampenda mme wangu ingawa hizo hisia sijawahi kuzipata hata kidogo ,nimekuwa nikilia na kujutia maamuzi yangu sina furaha ,ni mnyonge ,for the sake of my kids ndio napata faraja kidogo.

Kila siku zinavyoenda nazidi kuchanganyikiwa mwenzenu nitaishi hivi mpaka lini nifanye nini ili nipate amani ya roho,? maana hii pretend sasa imenichosha. Nakosa usingizi usiku kucha.
Ni mengi ya kuelezea lakini kwa hapa moyo wangu unazidi kuwa mnyonge :angry:

Nisaidieni juu ya hili ,niombee

Biashara ya kuolewa just because its fashion ndio hiyo. Na ukome.

Mumeo inaonyesha anakupenda ila wewe hujali.Feelings zako zipo kwa " X".

Umebarikiwa kupata watoto wawili, ila unawapenda watoto lakini baba wa watoto hao humpendi. Acha upumbavu.

Tafakari mama.
 
Halafu ajifunze kufanya maamuzi sahihi.... na kujisimamia
Ndoa ni zaidi ya kucheza kwaito

Na huo mchezo wa wanawake kuolewa wakiamini mwanaume atabadilika sijui watauacha lini
wanauacha wakishaolewa
 
Mpaka unaolewa unazuga humpendi? Au umepata mchepuko?ndo wako wamaisha huyo jilazimishe tu.
 
umeshapata mwingine yani nyie wanawake ni pasua kichwa uhuniuhuni hamumalizagi ndio maana ulibakwa
 
my dear sijawahi kutafuta faraja yoyote ,tangu nimebakwa huwa nahisi bado naendelea kubakwa sijui kwa nini

pole..wewe una psychological problem na unahitaji mshauri nasaha. tafuta mshauri nasaha utapona (ila sio wa angaza) huyo mumeo hana tatizo ww ndo una negative atitude towards him
 
The Boss nina kazi na mshahara mzuri tu ,ndio maana nikaomba kama kuna maombi nifunguliwe sijielewi na huu ni ukweli toka moyoni,Na kumwambia mme wangu simpendi kwa miaka yote hiyo hatonielewa hata kidogo

Tatizo ,lako ni kuubwa kuliko unavyo fikiri......je umewahi kumpenda mtu mwingine? umewahi ku fall in love ?
 
nenda hospitali ya Tumaini umuulizie psychologist sijui kama bado yupo uanze therapy ya tatizo la kubakwa kwanza....
 
Biashara ya kuolewa just because its fashion ndio hiyo. Na ukome.

Mumeo inaonyesha anakupenda ila wewe hujali.Feelings zako zipo kwa " X".

Umebarikiwa kupata watoto wawili, ila unawapenda watoto lakini baba wa watoto hao humpendi. Acha upumbavu.

Tafakari mama.

kuna wakati unaweza kujaribu kuvaa viatu vya mwingine? yaani kuwa empathetic? Mbona amejieleza sana vya kutosha na inaeleweka wazi shida yake inatokana na kubakwa utotoni? Upumbavu wake unatokea wapi hapa? Kuomba msaada wa namna ya kuondokana na shida yake au? Ungekuwa unajua saikolojia kidogo ungejua kitendo cha kuolewa na mwanaume mkatili si kwa sababu alikuwa anataka ndoa kama fashion. Ni akili ilikuwa inamsukuma unconsciously kwa sababu ilishahusianisha mapenzi na ukatili. Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini kuna wanawake wanapigwa sana mpaka kuzimia au kulazwa karibu kila wiki lakini hawaondoki na wakiondoka baada ya muda wanarudi? Ni kwamba akili zao zinamisi vipigo. Kwao vipigo ndo mapenzi. Matatizo kama haya hayawezi kwisha kama mtu hatapata kufunguka kwenye utumwa wa hisia. Huyu dada anataka kufunguka, kwa hiyo, msaidieni badala ya kumzidishia machungu. Ni hayo tu.
 
Pole dada nimeamini sio wote wanaoolewa ama kuoa wanapendana ka dhati 7 years?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom