Maamuzi gani nichukue dhidi ya ndoa yangu?

Maamuzi gani nichukue dhidi ya ndoa yangu?

Humpendi inamaana hata akufanyie nini huwezi ku-appreciate hata siku moja. Ungekuwa unampenda ningesema jaribu kumjenga au kumfinyanga vile unataka awe ili uweze kuishi kwa amani


Utalazimisha mengine yote lakini si mapenzi, si kumpenda mtu!! Nahisi harufu ya watoto kulelewa na single parent hapa

ndio maana naomba ushauri hata kama ni msaada kimaombi najua JF hakuna kinachoharibika
 
Jikabidhi kwa Bwana Yest omba na kufunga kwa imani..km mkristo lakn....utampenda baba wa watoto wako, nae pia atabadilika atakuwa mwanaume anae behave vizuri

thanks mamy nimejitahidi sana kufanya hivi sijui imani yangu ni haba??
 
my dear sijawahi kutafuta faraja yoyote ,tangu nimebakwa huwa nahisi bado naendelea kubakwa sijui kwa nini

sasa hilo ndilo tatizo na siyo humpendi mumeo. hata ukimpata mwingine utakuwa hivyo hivyo baaada ya muda fulani. hayo ni matatizo ya kisaikolojia unapaswa kuendelea kuyavumilia
 
vitabu vya Mungu vinaweza kukusaidia juu ya jambo lako, visome, nje ya hapo humpendi gangster, ina maana yule wa mwanzo alikuwa sharo? miaka 7 hujawahi mpenda mume wako na umeolewa nae na umezaa nae? kweli wale waliosema mapenzi ni hisia walikosea kabisa kwako.
 
sasa hilo ndilo tatizo na siyo humpendi mumeo. hata ukimpata mwingine utakuwa hivyo hivyo baaada ya muda fulani. hayo ni matatizo ya kisaikolojia unapaswa kuendelea kuyavumilia

hapo nimeshajiuliza mbona yule aliyeniacha akaenda Ovasizi nilikaa nae confortabe kabisa
 
Halafu ajifunze kufanya maamuzi sahihi.... na kujisimamia
Ndoa ni zaidi ya kucheza kwaito

Na huo mchezo wa wanawake kuolewa wakiamini mwanaume atabadilika sijui watauacha lini

Hahahaha, nmekumbuka kuna mwalimu wetu wa dini aliwai tuambia, hakuna mkombozi wa mchumba.( yani mkiwa kwenye uchumba kama mmoja wenu ana tabia za ajabu ni mara chache sana unaeza kumkomboa) akabadili tabia kbs.
 
Una tatizo kwa kweli.

Sijui kama mumeo ni muelewa kiasi gani? Na anajali kiasi gani?

Ulishawahi mwambia ulibakwa?

Unahitaji kutembelea maumivu yako, ulie, uomboleze kwa muda, then utaweza kusamehe/kijisamehe/kusahau.

Kuhusu kumpenda mumeo, hapo ndio tatizo, sababu kama humpendi mtu kimapenzi, ni humpendi tu. Tena akiwa anakukwaza ndio kabisaaaa. Angekuwa hakukwazi sana ungeweza kujifunza kumpenda.

Ulishawahi fikiria kuchukua likizo ya ndoa? Je, mumeo ni kuelewa kihivyo? Ujitafakari wewe binafsi kama binadamu?

Point kubwa: Mwondoe aliyezamia masomoni katika fikra zako, anaweza kuwa sababu ya kushindwa kuwa na furaha na ndoa yako. Kisa tu, unalinganisha.

Ngoja nikuitie Asha Mashauzi na Khadija Kopa King'asti na snowhite respectively.
 
Last edited by a moderator:
Halafu ajifunze kufanya maamuzi sahihi.... na kujisimamia
Ndoa ni zaidi ya kucheza kwaito

Na huo mchezo wa wanawake kuolewa wakiamini mwanaume atabadilika sijui watauacha lini


Kweli kabisa

Eti nitambadirisha?
Ww ni Mungu?
Na hii ndo imezicost ndoa nyingi sn.
 
Kuna vilaza wengi humu huyu Mama kachukua story FB kaona na yeye aje ku post

sio Story kakaangu muhusika mwenyewe ni mie ndio maana nimeomba msaada wa ushauri na maombi zaidi
Nataguliza shukrani
 
hapo nimeshajiuliza mbona yule aliyeniacha akaenda Ovasizi nilikaa nae confortabe kabisa

kingine jaribu kutandika shuka na foronya za mito zenye rangi ya "purple". Pili hakikisha unabadili style za tendo la ndoa na mumeo hasa zile ambazo zinakukumbusha ulipobakwa.kama kuna picha ua kitu chochote mpenzi wako wa zamani alikuachia na bado unakitunza basi kitupe. Ondoa picha zote chumbani zilizopo ukutani- bakisha picha zako na mumeo tu.

Barola_Plum_photo.jpg
 
my dear sijawahi kutafuta faraja yoyote ,tangu nimebakwa huwa nahisi bado naendelea kubakwa sijui kwa nini

Unahitaji mtaalamu wa psychology akusaidie.Halafu kitu kingine, humpendi mumeo au tabia zake?au vyote?Kwa sababu ulishaamua kumkabidhi moyo wako jaribu kufanya yafatayo

1)Muombe Mungu msamaha kwasababu ulikula kiapo cha uongo( kama ni mkristu)
2)Mwambie Mungu pamoja na yote unahitaji maisha mapya ya mumeo na wewe.
3) Shirikisha wasimamizi wa ndoa kwa mashauri zaidi.
4) Usikate tamaa maisha lazima yaendelee.
 
Tatizo liko hapo, inawezekana wala si mumeo saana.

Kubakwa kwa mwanamke sio kitu kidogo. Mipini hii tunaipenda sana, ila likifosiwa uwiii, ni aheri kuliwa na simba. Usidhani ni kitu kidogo kabisa hicho, ungeweza pata msaada wa kisaikolojia ungepata ahueni.


Hata kwa mzee kama mie, bado naogopa dhahama kama hii, seuse at 15? Labda ulikuwa bado na ka bikra kako, unakapenda na kukatunza, then mtu akakupoka just like that. Kwangu, wewe ni kashujaa kuliko unavyojichukulia, wengine wanaobakwa wanajiua, lakini wewe umeweza kuendelea na maisha hadi kuwa na courage ya kufunga ndoa.

Talk abiut it, mara nyiingi sana ila na mtu unayemwamini hadi uone ni kawaida, ni sehemu ya therapy.

Inawezekana hata kusema hapa leo kukakupunguazia mzigo kwa asilimia kubwa.

Hatuna huduma za ushauri saana wa kisaikolojia, nafasi hii imechukuliwa na dini zetu. Kama huko unakoamini unaweza kupata huduma hii, nenda kaitafute, ni kwa ajili yako na amani ya moyo wako.

Ila mwisho wa siku, kumshirikisha mumeo ni jambo la muhimu, asipokusaidia basi, umefanya sehemu yako. Huwezi jua, inaweza kuwa suluhu.

Hapa duniani, furaha yako inaanzia kwako, usimtegemee mtu mwingine akupe furaha, bali akamilishe pale panapopungua. Sasa basi, kufurahia mchakato wa uumbaji, anza kwa kujiponya kovu lako la kubakwa.

Unaweza simulia ilikuwaje ulipobakwa? (sio lazima lakini)

my dear sijawahi kutafuta faraja yoyote ,tangu nimebakwa huwa nahisi bado naendelea kubakwa sijui kwa nini
 
Uwiii, I have been coned, anyway hasara yake, mie akili yangu huwa haiishi kwa kushauri, bali huchaji zaidi.
Ila kujisingizia kubakwa lazima uwe sterling.

Kuna vilaza wengi humu huyu Mama kachukua story FB kaona na yeye aje ku post
 
acha kuweka past katika maisha yako focus .... kumbuka historia ni historia tu huwezi kubadilisha kitu... unalloweza kufanya stop pretending be you and make decision
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom