Pole dada. Nakuelewa sana. Hata kama ni story ya facebook bado inaweza kusaidia mtu. Narudia na kusisitiza alichosema Snowhite. Kubakwa kwako kumechangia kwa kiwango kikubwa kama si chote kuchagua wapenzi wanaokuumiza kwa sababu akili yako inahusianisha mapenzi na ukatili. Yule aliyeenda ulaya pia alikuwa na elements za ukatili ila hukuziona au kuzitambua mpaka alipokutelekeza na kukuachia maumivu.
Suluhisho ni moja tu: kukabialiana na zamani yako (your past). Kubali ukatili uliotendewa, kubali kuwa hukuwa na uwezo wa kudhibiti kisha umsamehe kila mwanaume aliyekukosea - hasa hasa huyo mbakaji. Kufanya mwenyewe hutaweza maana unaweza kukata tamaa kama ambavyo ushaanza kuhisi una imani haba. Tafuta mtu unayeamini anaweza kukusikiliza, umwage yote yaliyomo moyoni, akuongoze katika mchakato wa kupona. Kwa kuwa umesema uko dar nakushauri umtafute Mchungaji Profesa Masalakulangwa. Ni mtheolojia na profesa wa medical psychology. Anapatikana chuo cha tiba kairuki. Anafanya vizuri sana huduma ya ushauri kwa watu kama wewe. Mtaweza kungalia tatizo lako from spiritual and psychological perspective kulingana na atakavyoona.
Ukikimbilia kwa hawa wachungaji wetu "wajasiriamali" usishangae kuambiwa una roho ya hili na lile, sijui jini mahaba na mwishowe watakuombea na kukemea pepo ambaye hayupo, hali yako itaendelea hivyo hivyo au kuzidi kuwa mbaya na kujikuta unatanga tanga kutafuta watumishi mpaka ufilisike. Pia kama unapenda kusoma tafuta kitabu cha "Joy comes in the morning" cha hopolang phororo. Amepitia hali hii na amepona majeraha yake. Viko bookshops kubwa hapa dar kama pale mlimani city. Pia kipo kitabu cha "are you the one for me" cha prof. barbra de angels kinaweza kukupa mwanga kwenye hiyo ndoa.
Kwa kuwa uko kwenye ndoa na tatizo lako linakuathiri wewe binafsi na likitatuliwa litamuathiri na mume wako na ndoa yako kwa ujumla, mume wako lazima umshirikishe maana haitakuwa na maana unatoka kwenye therapy halafu unaenda kukutana na mtu yule yule kufanya kitu ambacho unataka kukiacha. Hapa lazima hekima itumike. Mumeo kwa tabia zake ulizosema na yeye ana psychological issues zinazomfanya awe hivi. Kama atapenda kukupa ushirikiano mkaangalia upya maisha yenu mnaweza kuwa na ndoa moja matata sana. Yaani nzuri. Asipotoa ushirikiano, nachelea kusema huna budi kuachana na mtesi wako, kwani ukipona majeraha utakuwa mtu mpya anayetaka kupenda na kuonyeshwa upendo, na mumeo hatakuwa na hivyo vigezo. Naamini mshauri wako (kama utaenda kwa professional) atakuwa na uzoefu katika maswala kama haya. Nakutakia heri, Mungu akutie nguvu.