Sidhani,anyway ni tabia ya mtu binafsi. Mimi nimelelewa na mama(mzee alirip nikiwa kwa tumbo),alafu ni last born ila hakukua na kudeka wala nini,maza alitulea kwa mkono wa chuma maana tulikua madume tu vinginevyo tungemshinda.
Niko strong sio lege lege,sinuni nuni ila nina hasira nyingi sana. Hao mashemeji zako ni tabia yao tu. Kuhusu kujali na kuthamini mke sijui maana sijaoa.
Hebu niambie kuna tatizo gani kwenye hili au mfano ulio utoa? Kwanini Mama aliye nilea asiwe wa kwanza halafu wa kwanza awe MTU niliye kutana nae ukubwani?
Si kila mama ana dekeza mtoto
Hata Mimi nimelelewa na Mama na yeye ndiye huwa anakuwa wa kwanza wengine wanafata na katika hili huwa sina mjadala kabisa!
Dedication
Nani kama Mama-Christian Bella
Hapo kwenye hasira.. Ni nini kimekufanya uwe na hasira??
Mama ndo kila kitu,nampenda sana!namuombea aishi miaka mingi nikikumbuka hasa alipokuwa akifanya vibarua kwenye mashamba ya watu ili tu nipate riziki na shule.umenikumbusha mbali sana!
Habari wandugu wa jukwaa hili!
Wajameni nimeambiwa na kusikia tabia walizonazo wanaume wengi waliolelewa na mzazi mmoja hasa Mama!
kuwa ni wanaume wanaojali na kuthamini Wake zao japo sijathibitisha hili!
Wengi Wao nimegundua ni watu wakudeka sana, wapo legelege sio wakamavu Pia wanasumbuliwa na tabia ya kununa kuna! Hili nimelithibitisha hata kwa mashemeji zangu! Naomba nilete hili mezani tuchangie kwa pamoja nifahamu nisiyoyajua mengine!
Asanteni
Sio wote ila wengi wako hivyo. Na wanaume waliozaliwa peke yao kwenye familia huku wakizungukwa na wadada wengi wakoje?.
Nashauri usome Edwin Mtei's From Goatherd to Governor (Mchunga Mbuzi hadi Gavana wa Benki Kuu) . Mwasisi wa CHADEMA, chama kinachotarajia kuchukua DOLA, naye alilelewa na mama tu. Nimempigia simu kumwaririfu na kumsomea thread hii, akanijibu HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE ifikapo Oktoba 2015.
Pamoja na ukweli kwamba wapo strong women wanao lea watoto vizuri bila kudekeza ila bado huwa upungufu unakuja kuonekana tu. Malezi ya baba yana nafasi yake pia hata mama akiwa smart vipi. Mimi nilishaona tatizo la kutokuwa na msimamo as a man. Mara nyingi hawa watu huyumbishwa na saa nyingine huwa hawawezi kutoa final decision yeye kama yeye bila kushauriana na watu wengine. Na sometimes hawa watu hukosa sauti kama watawala katika familia zao. Ila hii si applicable kwa wote ila wengi wao ambao nimeshawahi ishi nao na kuwashuhudia wana hivyo vi chembe chembe