afrique
JF-Expert Member
- Jun 28, 2012
- 509
- 136
Hio bible ya undengerekoni hebu weka huo mstari umeutoa wapi
Mhubiri 10:19
Hio bible ya undengerekoni hebu weka huo mstari umeutoa wapi
Nimeipenda hii,wanaume wengi ambao sasa tunatafuta mwenzi wa ndoa tuna taabika sana,kama hauna elimu kubwa na hauna hela utaishia kuwatazama wadada hatakama ungekuwa na nia nzuri kiasi gani na ndio wengine wanasema kama hauna peza wdada wazuri utaishia kuwaita shemeji.lakin wangelijua kesho itakuweje?
Siyo kweli! Mnapenda mambo makubwa wakati uwezo wenu mdogo!
Wako wa Dada wa kusuit kila aina ya uchumi na elimu ya mwanaume!
Cha msingi wale wa size yenu mnawakimbia! mnang'ang'ania viatu vikubwa akati miguu yenu midogo!
hivi unajua upendo hauna macho? unaweza kumpenda mtu kumbe mtu mwenyewe ni maringo, ooh sio type yangu,mara hajasoma mara hana pesa,na wakati huo umempenda.tunapata sana taabu na wadada haswa waliona kijielimu walivyopata,hamuwezi kufikiria wazee wetu waliishije mpaka mkafikia hapo mlipo nyinyi BADILIKEN WADADA HAYA NI MAISHA JAMANI,MUNGU NI MWEMA.
Mhubiri 10:19
Sasa kama mtu hajawa tayari kiuchumi kwa nini aoe? Kuoa ni kuanzisha familia, ni jukumu zito. Kuna makabila kama langu linazingatia sana uwezo wa kiuchumi kwenye swala zima la ndoa na ninakubaliana nalo. Kuna makabila mengine hayajali. Hata kijana akiolea nyumbani poa tu ilimradi ana godoro. Yeye na mkewe watakula kwa baba na mama mkwe. Watoto kila mmoja atakuja na rizki yake.
Kukubali kuolewa/kuoa mtu kwa kuamini kichwa kichwa kuwa kesho atakuwa rais au mkurugenzi ni kucheza patapotea isiyo na mashiko. Mimi lazma niangalie uwezo wako kiuchumi. Hata akija mwenye hela lazima nichunguze anazipataje na akili kiasi gani ili niangaalie kama huo uchumi wake unaweza kuwa ni endelevu au la ili niamue kama naweza kuthubutu au la. Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kwenye hili swala. Hebu fikiria anakujia mtu ana miaka kuanzia 35 kwenda mbele anataka kuoa halafu kiuchumi bado anaishi kwa matumaini. Upande wa mapato haujakaa sawa, halafu anataka aongeze matumizi kwa kuwa na familia!
Nikimkataa mtu leo, kesho akaja kuvunja rekodi ya bakhresa mi ntajipa tu moyo wa plastiki kuwa hakuwa wangu. Na yeye anatakiwa anishukuru maana nisingemkataa asingepata changamoto ya kutafuta hela. Kwa nini nichague mtu ambaye bado anajitafuta, niishi kwa shida nikisubiria miezi na miaka atoke kiuchumi wakati wakaka waliokwishajitafuta na kusimama na ni "husband material" na wanatafuta wake wapo? Mi naishi leo, ila nachokijua ni kuwa vigezo vya kuzingatia wakati mtu anatafuta mchumba havifanani. Vigezo hutegemea sababu za mtu kutaka kuoa au kuolewa. Kama nia ni kuanzisha familia, itategemea ndoto zako kuhusu hiyo familia. Kama ni "kuondoa nuksi" utaoa au kuolewa na chochote kitachokuja mbele ya macho n.k.
na ukiolewa na mwenye pesa leo na kesho akaishiwa itakuwaje?
Security ipo kwa JESUS pekee
"Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote"
Sante Mtumishi Afrique!
Acha ujinga ww yaani maneno yoooote hayo unashindwa kujitambua hata kidogo, umekalia kulisingizia Kabila, Kabila gani linachangulia mtu mke, we huoni hio kitu sasa hivi anaaply both side I mean hata mwanamke unatakiwa uzitafute na kama hauna basi ungana na mwenzio mzitafute, acha vya ubwete mkiombwa 0713 mnalalamika, fata ushauri wa mkuu hapo