Maalum kwa wadada wote ambao hamjaolewa

Maalum kwa wadada wote ambao hamjaolewa

Ni kwel lakini siku hizi mambo yamebadilika!
 
Wadada wengi, hata waliookoka, wana tabia ya kuchagua wachumba au wenzi wa maisha kwa kutazama hali ya maisha ya wakati huo ya kijana husika
**JIFUNZE KUMUULIZA MUNGU*
NI HAYO KWA LEO WADAU
Aah hapo kwenye kolezo huwa hawakukatai labda usiwe mwenzao ktk ulokole.Kwani ukimwambia umeongozwa na roh..mtak.. hawakatai au hukusikia waumini kwa asikofu Kaakobe enzi zake?
 
Wakati mwingine ni kweli na kwa upande mwingine unaeza mpenda mtu kwa moyo wote na majanga yake yote bila kujali hali ya uchumi aliyonayo kwa wakati huo. Na siku akifanikiwa hata jina lako analisahau na kuhama njia kabisaaa. Pesa mara nyingi inambadilisha mtu na tabia yake.
 
Sio dhambi kupenda pesa! After all Biblia inasema fedha ni jawabu la mambo yote! She is very correct!

Kuna Biblia mpya siku hizi? Hebu utafute huo mstari utupe na "muktadha" wake na sisi tupate kuutafakari. Nilifikiri biblia imesema tutafute fedha lakini tusizitumainie/tusizipende kuliko Mungu.
 
Mh!Wanawake tubadilike jamani,zama za kutegemea men kila kitu zilipitwa,tunadai haki sawa zipo wapi,what are u studying for,maisha ni kusaidiana,tusifanye kuoa iwe badden,money is nothing what matters is love na kuelewana.
Kama mm ni man nakupitia mbali mwanamke wa dizain hii...
 
Aah hapo kwenye kolezo huwa hawakukatai labda usiwe mwenzao ktk ulokole.Kwani ukimwambia umeongozwa na roh..mtak.. hawakatai au hukusikia waumini kwa asikofu Kaakobe enzi zake?

wewe umepotoka au hujui unachokieleza mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe,nani alikuambia binti mlokole akiambiwa na mwanaume tu kuwa Roho amemfulia anakubali? Neno linasema zichunguzeni kila roho mengine matapeli yaliyo jichanganya humo,binti aliye kiroho ataongozwa na Roho na si kwa kuambiwa neno tu na mwanaume".........basi nasema enendeni kwa Roho....."

 
wewe umepotoka au hujui unachokieleza mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe,nani alikuambia binti mlokole akiambiwa na mwanaume tu kuwa Roho amemfulia anakubali? Neno linasema zichunguzeni kila roho mengine matapeli yaliyo jichanganya humo,binti aliye kiroho ataongozwa na Roho na si kwa kuambiwa neno tu na mwanaume".........basi nasema enendeni kwa Roho....."

ni kweli kabisa!!
 
Wadada wengi, hata waliookoka, wana tabia ya kuchagua wachumba au wenzi wa maisha kwa kutazama hali ya maisha ya wakati huo ya kijana husika.

Akina kaka wengi wameambulia matusi, au hapana za nguvu, kwa vile tu hawana maisha mazuri at the moment.

Tahadhari yangu kwako ewe dada ni kwamba, kabla haujampa jibu kaka aliyekufata, Muulize Mungu. Usiamue kwa macho, huenda huyo kaka ana hali mbaya ya uchumi sasa, lakini kumbe miaka 2 tu mbele anakwenda kuwa Influencial person, Future is in God's hand. Usikurupuke, utalia kesho, utatamani ku-rewind muda hautaweza.
**JIFUNZE KUMUULIZA MUNGU*
NI HAYO KWA LEO WADAU

Kweli kabisa
 
Sasa kama mtu hajawa tayari kiuchumi kwa nini aoe? Kuoa ni kuanzisha familia, ni jukumu zito. Kuna makabila kama langu linazingatia sana uwezo wa kiuchumi kwenye swala zima la ndoa na ninakubaliana nalo. Kuna makabila mengine hayajali. Hata kijana akiolea nyumbani poa tu ilimradi ana godoro. Yeye na mkewe watakula kwa baba na mama mkwe. Watoto kila mmoja atakuja na rizki yake.

Kukubali kuolewa/kuoa mtu kwa kuamini kichwa kichwa kuwa kesho atakuwa rais au mkurugenzi ni kucheza patapotea isiyo na mashiko. Mimi lazma niangalie uwezo wako kiuchumi. Hata akija mwenye hela lazima nichunguze anazipataje na akili kiasi gani ili niangaalie kama huo uchumi wake unaweza kuwa ni endelevu au la ili niamue kama naweza kuthubutu au la. Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kwenye hili swala. Hebu fikiria anakujia mtu ana miaka kuanzia 35 kwenda mbele anataka kuoa halafu kiuchumi bado anaishi kwa matumaini. Upande wa mapato haujakaa sawa, halafu anataka aongeze matumizi kwa kuwa na familia!

Nikimkataa mtu leo, kesho akaja kuvunja rekodi ya bakhresa mi ntajipa tu moyo wa plastiki kuwa hakuwa wangu. Na yeye anatakiwa anishukuru maana nisingemkataa asingepata changamoto ya kutafuta hela. Kwa nini nichague mtu ambaye bado anajitafuta, niishi kwa shida nikisubiria miezi na miaka atoke kiuchumi wakati wakaka waliokwishajitafuta na kusimama na ni "husband material" na wanatafuta wake wapo? Mi naishi leo, ila nachokijua ni kuwa vigezo vya kuzingatia wakati mtu anatafuta mchumba havifanani. Vigezo hutegemea sababu za mtu kutaka kuoa au kuolewa. Kama nia ni kuanzisha familia, itategemea ndoto zako kuhusu hiyo familia. Kama ni "kuondoa nuksi" utaoa au kuolewa na chochote kitachokuja mbele ya macho n.k.

Acha ujinga ww yaani maneno yoooote hayo unashindwa kujitambua hata kidogo, umekalia kulisingizia Kabila, Kabila gani linachangulia mtu mke, we huoni hio kitu sasa hivi anaaply both side I mean hata mwanamke unatakiwa uzitafute na kama hauna basi ungana na mwenzio mzitafute, acha vya ubwete mkiombwa 0713 mnalalamika, fata ushauri wa mkuu hapo
 
Back
Top Bottom