Maalum kwa wadada wote ambao hamjaolewa

Maalum kwa wadada wote ambao hamjaolewa

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Wadada wengi, hata waliookoka, wana tabia ya kuchagua wachumba au wenzi wa maisha kwa kutazama hali ya maisha ya wakati huo ya kijana husika.

Akina kaka wengi wameambulia matusi, au hapana za nguvu, kwa vile tu hawana maisha mazuri at the moment.

Tahadhari yangu kwako ewe dada ni kwamba, kabla haujampa jibu kaka aliyekufata, Muulize Mungu. Usiamue kwa macho, huenda huyo kaka ana hali mbaya ya uchumi sasa, lakini kumbe miaka 2 tu mbele anakwenda kuwa Influencial person, Future is in God's hand. Usikurupuke, utalia kesho, utatamani ku-rewind muda hautaweza.
**JIFUNZE KUMUULIZA MUNGU*
NI HAYO KWA LEO WADAU
 
Wamekusikia kama masikio yao yapo kwa ajili ya kusikia.
BTW 'influential' is the corrct spelling.
 
Tatizo kuna wanaume wenzi wetu wanakuwa na adabu na kumfuata dada wa watu mikono nyuma wakiwa hawana pesa. Pindi mpunga ukipatikana basi na tabia hubadilika. Vile vile tusisahau kuwa tunaishi in a material world. So Im not saying that I condone this habit but I understand.
 
Hatufuati uchumi tu! na nyie msituchague kwa uzuri wa sura na umbo tu, Beauty fades with aging! Tukizeeka uzuri unapotea inabaki uzuri wa nafsi! utajuaje uzuri wa nafsi ya mtu? ni kumuomba Mungu akupe mke mwema!
Wengi wenu wanajuta na kupata stroke kwa kukosea kuoa!
 
Sasa kama mtu hajawa tayari kiuchumi kwa nini aoe? Kuoa ni kuanzisha familia, ni jukumu zito. Kuna makabila kama langu linazingatia sana uwezo wa kiuchumi kwenye swala zima la ndoa na ninakubaliana nalo. Kuna makabila mengine hayajali. Hata kijana akiolea nyumbani poa tu ilimradi ana godoro. Yeye na mkewe watakula kwa baba na mama mkwe. Watoto kila mmoja atakuja na rizki yake.

Kukubali kuolewa/kuoa mtu kwa kuamini kichwa kichwa kuwa kesho atakuwa rais au mkurugenzi ni kucheza patapotea isiyo na mashiko. Mimi lazma niangalie uwezo wako kiuchumi. Hata akija mwenye hela lazima nichunguze anazipataje na akili kiasi gani ili niangaalie kama huo uchumi wake unaweza kuwa ni endelevu au la ili niamue kama naweza kuthubutu au la. Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kwenye hili swala. Hebu fikiria anakujia mtu ana miaka kuanzia 35 kwenda mbele anataka kuoa halafu kiuchumi bado anaishi kwa matumaini. Upande wa mapato haujakaa sawa, halafu anataka aongeze matumizi kwa kuwa na familia!

Nikimkataa mtu leo, kesho akaja kuvunja rekodi ya bakhresa mi ntajipa tu moyo wa plastiki kuwa hakuwa wangu. Na yeye anatakiwa anishukuru maana nisingemkataa asingepata changamoto ya kutafuta hela. Kwa nini nichague mtu ambaye bado anajitafuta, niishi kwa shida nikisubiria miezi na miaka atoke kiuchumi wakati wakaka waliokwishajitafuta na kusimama na ni "husband material" na wanatafuta wake wapo? Mi naishi leo, ila nachokijua ni kuwa vigezo vya kuzingatia wakati mtu anatafuta mchumba havifanani. Vigezo hutegemea sababu za mtu kutaka kuoa au kuolewa. Kama nia ni kuanzisha familia, itategemea ndoto zako kuhusu hiyo familia. Kama ni "kuondoa nuksi" utaoa au kuolewa na chochote kitachokuja mbele ya macho n.k.
 
Well said!
 
okey wewe utakuwa ni money oriented person
 
Back
Top Bottom