Maalim Seif: Nimekusanya matokeo kutoka vituo vyote ninaongoza, aitaka ZEC imtangaze mshindi

lHata hivyo ushindi huu wa CUF haujanifurahisha sana maana naona wameshinda kwa tofauti ya kura kama 122,000 tuu wakati tulitegemea ushindi mkubwa zaidi ya hapo.
Hata hivyo nitoe pongezi zangu kwa Maalim Seif, CUF na Ukawa kwa ujumla kwa ushindi huu na kumtakia kila la kheri Maalim Seif katika kutekeleza majukumu yake mapya.
 
attachment.php



Muda mfupi uliopita, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni.


Amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein, na kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye fomu zinazotoka vituoni.

Chanzo: DW
Jaman nisomeeni hizo kura no million au laki sielew
 
Mimi ningeomba labda wenye uwelewa wa sheria ya uchaguzi inasemaje katika hali kama hii....!
  1. Je, kama matokeo halali ni yale yatakayotolewa na Tume ya Uchaguzi, kauli hii inapewa credit gani?
  2. Iwapo lengo la kuzuia jambo lililoko mahakamani kujadiliwa na vyombo vingine ni kulinda uhuru wa mahakama, Je, Maalim Seif atakuwa hajaingilia mamlaka/uhuru wa Tume?
  3. Je, ikitokea na Shein akafanya hivi, nini kinaweza kutokea, na kimsingi itakuwa imesababishwa na nani?
  4. Je, katika akili ya kawaida kabisa, ni sawa mgombea kufanya hivi?
Nahitaji tu kueleweshwa....!
 
Kunya anye kuku akinya bata kahara January keshatangaza habari za magufuli mapemaaaaaaaaaaaaaaa yeye ni tume?
 
shein nae akitangaza yake sijua kama wataelewana. atulie asitake lazimisha tume itangaze anavyotaka yeye.

maalim seif kakusanya karatasi zote za vituo na ndivyo zinavyosomeka. hata kama shein naye akikusanya karatasi zote matokeo yatabaki hivyo hivyo na maalim seif atatangazwa kuwa rais. wewe ulitaka matokeo yaweje ndipo uridhike?
 
Sasa Dr.shein akitoa ya kwake yanayoonesha ameshinda, maalim atatoa uthibitisho gani ili watu wamuamini? Hii kazi ya kutangaza matokeo itakuwa ni busara kubwa kuiachia mamlaka husika jukumu hilo ili kuepusha kutokea fujo.
 
Jaman nisomeeni hizo kura no million au laki sielew

Hizo ni laki, kwani jumla ya waliojiandikisha Zanzibar yote ni 500,000. Wapiga kura Zanzibar siyo wengi, kwa ujumla Zanzibar haina watu wengi ni kama 1.3m hivi.
 
Sasa Dr.shein akitoa ya kwake yanayoonesha ameshinda, maalim atatoa uthibitisho gani ili watu wamuamini? Hii kazi ya kutangaza matokeo itakuwa ni busara kubwa kuiachia mamlaka husika jukumu hilo ili kuepusha kutokea fujo.

Zanzibar wapiga kula wachache, na vituo viko karibu. inakuaje mpaka sasa watangaze matokeo ya maeneo manner tu?
 
Back
Top Bottom