Maalim Seif: Nimekusanya matokeo kutoka vituo vyote ninaongoza, aitaka ZEC imtangaze mshindi

washauri ndugu halafu mwambie makongoro ajifunze kuheshimu watu mbona wewe una heshima?
 
12193404_134089400280813_9033041387360113242_n.jpg
 
Sheni kashaletewa matokeo yake mkuu ndio hizo kura 178,363. Hapa hamna ujanja ujanja tena. Na kwa kitendo hiki alicho fanya Seif ni cha kishujaa na kuwaandaa wale walio mchagua kwa matokeo yoyote yatakayo tangazwa kinyume.Na shauri Shein akubaliane na hali.
Zanzibar inaelekea kwenye mgogoro wa kikatiba.Bila pande zote mbili kuridhia matokeo hamna undwaji wa serikali.(katiba inatambua serikali ya umoja wa kitaifa)
 
Unguja ni kisiwa kimoja
nchi ni Zanzibar
Ni kweli Zanzibar inajumuisha Pemba na Unguja, sasa kama Maalim kapata kura zote upande wa Pemba, akiongeza za Unguja kwa nini siwe Mshindi ilhali mwenzake hakupata kitu Unguja.
 
Maalim angetoa na vielelezo pia badala ya kusema tu amepata kura ngapi dhidi ya mpinzani wake.

Vv
 
Mbowe yuko wapi atuwekee zetu, hapa hakuna kuzidiana akili.
Dada yangu nilikuwa nakuamini na nakufuatilia sana ila tangu kampeni za uchaguzi zianze nilianza kukudharau sana. Bora uchaguzi uishe nadhani utarudi kwenye akili zako za kawaidaulizozipeleka likizo.
 
Kiongozi mbona unajionyesha utupu wa bongo yako, sisi hatuhitaji kuona bwana ficha kidogo.

Tume inatangaza mshindi kwa mamaka ya kisheria haitoi taarifa, Maalim katoa taarifa zilizkusanywa na mawakala wake, ana haki ya kusema ni nini kimepatikana. Hii so siri ndo maana matokeo wanapewa mawakala na mengine yanabandikwa vituoni ili yajulikane. Kusema kapata kura kadhaa na mpinzani wake kura kadhaa linakukwaza kitu gani. Kama ni uongo na CCM waseme si walikuwa na mawakala wao vituoni.

Acha kuwa mfinyu hivyo bwana umeshakua mtu mzima wewe.

Hilo ndio tatizo anatoa wapi power ya kujitangazia ushindi? Ikiwa CCM na wao watachukua hatua ya kumtangaza mgombea wao hali itakuwaje? Mimi na wewe wote tunajiuliza nini maana ya kuundwa tume?
 
Na Mhamed khamis Pemba.


Wakati mgombea Urais kupitia mwevuli wa Ukawa Zanzibar ambae anatoka CUF Maalim Seif Sharif Hamad leo hii amevieleza vyombo vya habari na waangalizi mbali mbali wa kimataifa kuwa kwa mujibu wa fomu zilizobandikwa vituo vya kupiga kura zinaonesha ameshinda kwa 52.87.


Hatua hii imewafanya wafuasi wa Chama hicho maeneo mbali mbali Unguja na Pemba kuingia barabarani kushangiria ushindi.


Wakati wananchi wakiendelea kuhamasika zaidi eneo la Machomane wilaya ya Chake mkoa wa kusini Pemba ghafla Jeshi la Polisi liliwatawanya wafuasi hao kwa kutumia mabomu ya machozi.


Huku hayo ya kijiri kisiwani hapa kwa upande wa Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba wananchi wanaendelea kufurahia bila ya kutawanywa.


Lakini kwa upande wa Unguja hali si shwari maeneo mengi ya mji huo kunasikika sauti za mabomu ya machozi.


Wakati haya yakiendelea Tume ya uchaguzi wamesitisha kutoa matokea mbali mbali kwa sasa.


Katika hutuba yake kwa wanahabari mchana wa leo Maalim Seif aliitaka Tume hio (ZEC) kutangaza matokea halali yaliobandikwa vituoni.


Lakini pia alimuomba Rais kikwete kuingilia kati suala hili ili kuepusha nchi na matatizo.
attachment.php
 

Attachments

  • IMG-20151026-WA0014.jpg
    IMG-20151026-WA0014.jpg
    37 KB · Views: 178
Back
Top Bottom