Maalim Seif: Mwalimu na nahodha

Hilo ndilo wangepaswa kuelewa wale wanoamini kwamba maalim Seif angepaswa kwenda Chadema,kwenda kwake ACT ni kufungua front nyingine ya demokrasia ya vyama vingi sio tu kwa Zanzibar bali kwa Tanzania nzima kwenye Kanda za pwani na kusini ambako yalikuwa ni ngome za cuf iliyokuwa imara na moja.
View attachment 1048612

Ukweli umedhihiri kwa taratibu sana kuwa chama si majengo bali ni imani ya chama ndani ya nyoyo za wanachama wake.

Ghafla CUF mchana huu imetoweka.

Bendera zimeshushwa kwa kasi ya ajabu na rangi za ofisi kukwanguliwa na kupakwa rangi mpya za ACT Wazalendo.

Waliopata ushindi mahakamani imewadhihirikia kuwa hawana walichovuna isipokuwa kubebeshwa mzigo mzito wa misumari ndani ya gunia.

Imewadhihirikia kuwa hawajaweza kupata wanachama wa kuwaunga mkono lakini kubwa ni ule ukweli kuwa waliokuwa wabunge kwa kuhama chama na kwenda CCM safari yao ya siasa imefika mwisho.

Walio ndani ya CUF safari yao imefika tamati kwani wamechukua chama kilicho dhaifu kisichokuwa na wanachama, haiba wala mvuto si Bara wala Visiwani.

Aliyeshinda ni Maalim Seif kwa kushusha tanga na kupandisha tanga kuendelea na safari.

Maalim Seif kaandika historia nyingine ambayo haina mfanowe.

Baada ya kushindwa mahakamani haikupita hata nusu siku Maalim ameipa demokrasia nguvu mpya kwa kupeleka mamilioni ya wanachama ACT-Wazalendo.

Hii imepanua wigo wa demokrasia na kufungua "front mpya," kwa Wazanzibari.

Nahodha katoa kauli mbiu mpya: ''Shusha tanga pandisha tanga safari iendelee.''

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Mkuu Matola, kwa vile tunahimizwa sana tusichanganye dini na siasa, na kwa vile Chama cha CUF kiliwahi kunasibishwa na dini fulani, please usitumie maneno ya maudhi kwa watu wa dini nyingine, mfano wa neno " said ya kafir", sote tunaelewa ni watu wa dini gani huwaita wengine kafir na hao wanaoitwa kafir ni watu wa dini gani, hivyo ningeomba tuziepuke comments za aina hii ili hata sisi ambao tuko very comfortable na ACT, tuendelee kuiona ACT Wazalendo ni ile ile na sio CUF imebadili jina.
P
Mkuu Pascal hakuna dini inayoitwa Kafir, ni mtu anakuwa Kafir kama vile hakuna chama kinaitwa cha Wapumbavu lakini wafuasi wa chama huenda wakawa Wapumbavu.

Kafir ni mtu yeyote nayekwenda kinyume na maamrisho ya Mungu muumba hata kama atakuwa ni Muislamu. Ukafiri hauna dini. Kwa hiyo usilishirikishe hili neno na dini fulani.
 
Asante kwa tafsiri mpya ya kafir. Tafsiri rasmi ya kafir ni mtu asiyeamini Mungu anayetumia jina la Allah kwa hoja kuwa hakuna Mungu isipokuwa Allah. Mtu yoyote asiyemwamini Allah ni kafir.
P
 
Asante kwa tafsiri mpya ya kafir. Tafsiri rasmi ya kafir ni mtu asiyeamini Mungu anayetumia jina la Allah kwa hoja kuwa hakuna Mungu isipokuwa Allah. Mtu yoyote asiyemwamini Allah ni kafir.
P
Not quite mkuu. Unaweza kuamini kuwa Mungu ni Allah na ukawa kafir. Kwa mfano kwa waislamu wanaamini kuwa ukijinyonga ama ukifa ukiwa na pombe mwilini ama ukifa guest na mwanamke asiyekuwa halali kwako kwa ndoa basi unakufa ukiwa ni kafir. Hope thats clear
 
Mkuu Matola, kwa vile tunahimizwa sana tusichanganye dini na siasa, na kwa vile Chama cha CUF kiliwahi kunasibishwa na dini fulani, please usitumie maneno ya maudhi kwa watu wa dini nyingine, mfano wa neno " said ya kafir", sote tunaelewa ni watu wa dini gani huwaita wengine kafir na hao wanaoitwa kafir ni watu wa dini gani, hivyo ningeomba tuziepuke comments za aina hii ili hata sisi ambao tuko very comfortable na ACT, tuendelee kuiona ACT Wazalendo ni ile ile na sio CUF imebadili jina.
P

Kwenye jukwaa hili la JF SIASA bro Mayallah, kutoa ushauri kama huu ni kazi bure.....

Wengine kauli za udini ama hata matusi ya nguoni ndiyo hoja zao, hawajui kunyamaza wanapokuwa hawana hoja juu ya hoja fulani iliyo mezani...

Ili waridhishe nafsi zao kwenye hoja zinazogusa maslahi yao, kamwe hawawezi kupita tu....

Ni lazima wajaribu kukutoa kwenye reli kwa kushambulia personality yako na siyo kuishambulia hoja yako....

Na wa kulaumiwa kwenye hili ni Nape Mwana wa Nnauye ambaye ndiye mwasisi wa Team LB7 kwenye mitandao ya kijamii nyakati zile ktk jaribio la kurejesha uhai wa CCM wakiwa na mzee Kinana...!!

Na huo ndiyo ilikuwa mwanzo wa kushuka kwa hadhi ya jukwaa hili na badala JF Siasa kuwa uwanja wa viongozi kuja kuchukua mawazo mbadala ktk kurekebisha baadhi ya mambo ktk jamii, ikawa uwanja wa matusi na watu wenye heshima zao wakaandoka zao....!!
 
Not quite mkuu. Unaweza kuamini kuwa Mungu ni Allah na ukawa kafir. Kwa mfano kwa waislamu wanaamini kuwa ukijinyonga ama ukifa ukiwa na ,pombe mwilini ama ukifa guest na mwanamke asiyekuwa halali kwako kwa ndoa basi unakufa ukiwa ni kafir. Hope thats clear
No kafir has to do with imani, kuamini Mungu Allah na sio matendo.

Kafiri akufaaye si Islam asiyekufaa
Mtumikie Kafiri upate mradi wako
Msafiri Kafiri

Neno Kafiri ni derogatory, linatumiwa na watu wa dini fulani kuwalenga dini fulani. Naombeni msitake kulipamba.
Yaani ni jana tuu watu wamejiunga leo tunaanza kunyoosheana vidole na kuitana kafir?!

Si unaona mkafiri.kafiri. Kwa hiyo muislamu hawezi kuwa msafiri? Hahaha
 
Mkuu Matola, kwa vile tunahimizwa sana tusichanganye dini na siasa, na kwa vile Chama cha CUF kiliwahi kunasibishwa na dini fulani, please usitumie maneno ya maudhi kwa watu wa dini nyingine, mfano wa neno " said ya kafir", sote tunaelewa ni watu wa dini gani huwaita wengine kafir na hao wanaoitwa kafir ni watu wa dini gani, hivyo ningeomba tuziepuke comments za aina hii ili hata sisi ambao tuko very comfortable na ACT, tuendelee kuiona ACT Wazalendo ni ile ile na sio CUF imebadili jina.
P
Well said.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndivyo siasa ya Tanzania ilivyo. Tuliona kwa Slaa, Shibuda, Seif, Lowassa, kabla ya hapo Mrema, Malima na majuzi tumeona wabunge wa chadema na cuf.

Wote walihama vyama na kuchaguliwa huko walipohamia bila yeyote kujali itikadi zao.

Tanzania bado tuna "discuss" na kufata watu na si "ideas".

Hata ndani ya utawala ni hivyo hivyo.
Kwa Leo naomba nikuamkie mama yangu

Shikamoo Mama Faiza Foxy

Mi nakuheshimu sana ila tuendelee kuwa wapinzani wa mitizamo na itikadi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No kafir has to do with imani, kuamini Mungu Allah na sio matendo.

Kafiri akufaaye si Islam asiyekufaa
Mtumikie Kafiri upate mradi wako
Msafiri Kafiri

Neno Kafiri ni derogatory, linatumiwa na watu wa dini fulani kuwalenga dini fulani. Naombeni msitake kulipamba.
Yaani ni jana tuu watu wamejiunga leo tunaanza kunyoosheana vidole na kuitana kafir?!
P
Hata ww unaweza kuwa kafiri haijalishi upo dini gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom